Mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria wazima shambulio la makombora la Israel

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria wazima shambulio la makombora la Israel

Jeshi la Syria limetangaza kuwa, ngao ya ulinzi wa anga ya nchi hiyo imefanikiwa kuzima shambulio la makombora la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Kiarabu, Damascus.

Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Syria SANA, askari wa Kizayuni walifanya hujuma hiyo ya anga usiku wa kuamkia leo wakitumia anga ya Lebanon kinyume cha sheria, na kulenga maeneo ya kijeshi jijini Damascus.

Hata hivyo habari zaidi zinasema kuwa, ngao hiyo ya makombora ya Syria imetungua akthari ya makombora hayo ya utawala haramu wa Israel kabla hayajapiga shabaha.

Shirika la habari la al-Alam limeripoti pia kuwa, mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria umeamilishwa kwa ajili ya kuzima chokochoko hizo za maadui Wazayuni, katika mkoa wa Homs, katikati mwa nchi.

Utawala haramu wa Israel umekuwa ukitekeleza hujuma za anga dhidi ya Syria mara kwa mara, ambapo baadhi ya nyakati umekuwa ukifanya mashambulio hayo tokea kwenye Miinuko ya Golan ya Syria inayokaliwa kwa mabavu.

[https://media]Mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria

Mgogoro wa Syria uliibuka mwezi Machi 2011 baada ya makundi mengi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Saudi Arabia, Imarati, Marekani, utawala haramu wa Israel na washirika wao kuivamia nchi hiyo kwa lengo la kubadili mlingano katika eneo la Asia Magharibi kwa maslahi ya utawala huo wa Kizayuni.

Hata hivyo, msimamo imara wa serikali ya Damascus chini ya uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na washirika wake, umeweza kufelisha njama hizo za maadui sambamba na kuyashinda makundi hayo ya kigaidi.

Tags

SYRIA


4bvb025797037a1p108_800C450.jpeg
 
Back
Top Bottom