Mfumo wa siasa za Tanzania utamjenga Bi. Stagomena Tax au utabomoa historia ya mazuri yake?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Moja ya kitu kinachofanywa na mfumo wa siasa za Tanzania hasa kwa wanasiasa waliopo CCM na serikalini nikubomoa carrier zao na uzuri wao nakuwavisha maovu. Wanazuoni na wanasiasa walioonjeshwa mfumo wa serikali ya Tanzania wote wamebomoka badala yakujijenga zaidi. Ntatoa mifano michache.

Tukimtafuta Sospeter Mhongo katika ramani ya Dunia Toka alipokubali uteuzi na kuamua kuingia rasmi kwenye siasa hatuoni alipopotelea, amefutika nakubaki na CV Safi ya kabla yakuwa mwanasiasa. Baada ya kuingia kwenye siasa amechafuka na anashindwa kujisafisha badala yake ameamua kukaa kimya

Twende kwa Bashiru Ally, mwanazuoni na mchambuzi mahiri wa masuala ya kisiasa. Msomi aliyejitanabaisha kwa umahiri wa hoja na ushauri wa kesho ya Tanzania . Tumtafute wapi mtu huyu kwenye ramani ya wanazuoni wa Africa na hata Tanzania. Ametoweka, amechafuka na anajua wazi kwamba mguu alioingilia hakupaswa kuutumia katika umri alionao. Amefedheeahwa na siasa na kuamua kukaa kimya kwa ajili ya kesho asiyoijua. That's TZ politics

May be tumzungumzie Kabudi, alivyotamba UDSm akapambana bega kwa bega kuikomboa nchi kupitia Katiba mpya. Mara paap wakamwita, akapewa V8 na kukaa viti vya mbele na mfalme nakujiona mfalme na si Tena mwana wa asili ya Tembe. Akawadharau hata wapiga kura nakuridhika kwamba haitaji kura zao kuwa Mbunge. Mfumo umemchezea Leo hii anaogopa viti vya mbele nakuamua kukaa viti vya nyuma karamuni tusiona anavyotafuna. Too late hakuna kujijenga maaana msingi ulioubomoa haijengeki Tena kirahisi.

Tukimwangalia Masele Steven alivyojipambanua kimataifa na alivyozimwa na mtu mmoja tu kwa wivu nakuamini Masele anataka kujijenga beyond that man tayari bila hata Kutumia msingi wa hoja Masele kapotea kwenye ramani ya siasa vinginevyo aishi maisha ya watu si maisha yake.

Wapo vijana kama akina kafulila, Nassary, Mashinji, January, Nape na wengineo wa kariba hii. Wote hawa wamekaa kimya kusubiri zamu yao bila wao kujua muda hausubiri. Unalopaswa kufanya leo ukaacha kulifanya ni vigumu kulifanya kesho.

Kwa mifano hi na mingine mingi utabaini Taifa limejaliwa watu wenye maono lakini wanamezwa na mazingira ya siasa zisizotaka wenye maono bali zimejengwa kwenye misingi ya ukubwa wa umri, ukubwa cheo na ushirikina. Mazingira haya hata angeletwa Mzungu awezi kutoboa vinginevyo aungane na wazee wanavyotaka.

Hivi kwa mfano Januari Leo hii kwanini aonekani kwenye baraza la Mawaziri la Rais ambaye alikuwa bosi wake? Si kwa sababu Rais atambui mchango wake bali nikwasababu mfumo wa wazee ulitamka akae pembeni baada ya kuonekana anamikakati ya wazi kuwa Rais. Badala aachwe ashindane kuipata hiyo nafasi kwa kuijenga Tanzania na kuiacha kesho imshughulikie sisi tumemzima na kumwacha adumaze ubongo na kubaki na ningekuwa Mimi kichwani mwake.

Nimeeleza mengi lakini nataka tutafakari nakuona kama imani tuliyompa Stagomena Tax itadumu? Naamini alipoteuliwa tu ndipo kipenga kilipopigwa katika Jimbo lake kwamba Sasa Ni wakati wakujiandaa kwenda kugombea. Kipenga hiki akikiruhusu kimwongoze atapoteza CV yake ya nyuma na ataungana na akina Kabudi kustaafu siasa kwa fedhea badala ya furaha. Nimwombe mama yetu achange karata zake vyema, ni busara kuwatumikia Watanzania kuliko kuamua kuutumikia mfumo wa siasa ambao Leo hii umewashighulikia wanawake Kama Ndalichako, Tibaijuka, Migiro na watu wa aina hii ambao awali Dunia iliwaamini.

Nikutakie kila la kheri ndugu yangu Stagomena Tax katika kuimarisha au kubomoa carrier yako.
 
Siasa hizi za kilaghai kamwe haziwezi kumjenga mtu, wako wapi kina prof. Muongo, Prof. Tibaijuka, wallikuwa na heshima zao huko Ulaya, walipojiingiza tu kwenye siasa hizi chafu, wako wapi?!!

Kuna msomi mmoja ni mghana anafundisha chuo kikuu huko US, aliitwa na Rais wa Ghana kuja kuwa waziri, akasema hapana, siasa za kiafrika zitamharibia heshima yake aliyoijenga hapo Ghana na duniani kote!!!

Lazima pawe na ugumu tu pale akili ndogo ndio inataka kuongoza akili kubwa!!!
 
Kukubali teuzi ya serikali ya chama kile tayari kashaharibu credibility pamoja na CV yke,yan mtu anatoka SADC anakubali kuingia bunge moja na Kibajaji,Musukuma,slowslow na covid-19,,amekubali kuingia Kwenye futuhi😂...
 
Stagomena Tax awezi kutoboa kwenye mfumo wa Tozo, amemezwa na uteuzi na atatapikwa na meli ya siasa itakapomfikisha kwenye fukwe ya unafiki nakujipendekeza. Hakuna professionalism kwenye siasa za Tanzania Bali Kuna viumbe wachache ambao wamemiliki nchi. Tumewaruhusu waamue hatma ya wanasiasa wote nchini Jambo ambalo kutofautisha PHD na standard seven kwenye arguments hakuna tofauti.

Mfuate leo Stagomena Tax muulize unazungumzia mfumo wa serikali kwa Sasa atakuambia kila kitu kipo sawa na hakuna mapungufu......kwa sababu amekubali watu waondoe akili yake wamwekee akili yao kichwani. Natabiri kuporomoka kwa CV yake mara dufu
 
Umechambua vizuri ila kwa January umechafua hali ya hewa Labda Kama wewe ni mpiga debe wake.

Huyo January amekuwa Mbunge kwa miaka mingi hebu tuambie amefanya Mambo gani huko Bumbuli ya kuwashawishi Watanzania wampe urais?

Amekuwa waziri ktk wizara mbambali hebu tujuze alileta mabadiliko gani ya maana?

Hatutaki rais wa kaliba ya Kikwete na mwenye kujiona yeye ni mwerevu Sana kumbe alibebwa na jina la baba yake.
 
Ukishakua mwanasiasa roho yako inajawa na uongo uongo na usanii mwingi...

Inasikitisha sana...
 
Huyu mama kwanini siku hizi hatumii tena jina la Bamwenda?

Zamani akijulikana Kama Stergomena Tax Bamwenda
 
Back
Top Bottom