Mfumo wa Serikali yetu ni wa MCHANYATO....haufai kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa Serikali yetu ni wa MCHANYATO....haufai kabisa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAMBLER, Jan 10, 2010.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mada hii ni muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu kwani inahusika moja kwa moja na namna tunavyojitawala na kujiongoza.
  Naamini mfumo wa kitawala wa taifa letu unahitaji maboresho. Kwa mfano haionekani kirahisi tofauti na Dola na Serikali; kiasi wengi hawajui kama ni vitu tofauti. Hii inatukwaza mno.
  Nchi nyingi inawezekana kuona tofauti hizi, kwa mfano Dola la Uingereza lipo chini ya Malkia wakati serikali ipo chini ya Waziri Mkuu. Hali kadhalika Uturuki na Israeli ambapo kuna Rais (Dola) na Waziri Mkuu (Serikali)
  Kwetu sisi tuna huu mfumo mchanyato, ambao naamini hautufai. Kwani majukumu ya viongozi / watawala mbali mbali hayawi wazi vya kutosha. Matokeo ni kuwa na viongozi wengi wanaoishia kuwa mzigo kwa taifa.
  Ushauri wangu ni kufanya mabadiliko ya kikatiba, ili watu wachague tu wabunge watakaokaa miaka 5. Wabunge watachagua serikali (Waziri Mkuu na mawaziri wengine) kutoka miongoni mwao au kuteua miongoni mwa wanachi wanaoonekana kufaa. Kila baada ya miaka 7 Wabunge wamchague Rais kutoka miongoni mwao au miongoni mwa wananchi atakayeonekana kufaa. Aidha Bunge liwe na nafasi ya kumwondoa Waziri Mkuu au yeyote atakayeonekana hatoshi kwa kura.
  Hii itasadia kupunguza gharama za uchaguzi wa mara kwa mara. Gharama za uchaguzi siyo pesa tu, ni pamoja na muda na mikingamo inayofanyika panapokuwa na uchaguzi kama wengi tunavyojua. Aidha, itasaidia kuongeza athari za wanachi wa kawaida kwa mwenendo wa Dola na Serikali. Aidha, itasaidia kuwajibisha wanaochaguliwa.
   
Loading...