Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 892
- 1,226
A.alaykum wakuu,
Leo hii nimepata taarifa zilizonshtua kutoka kwa mtoto wa jirani yangu mmoja aliyehitimu darasa la saba na kufaulu kwa kiwango cha 'C'..Taarifa hii ni kwamba yeye na wahitimu wengine wenye kiwango cha ufaulu kisichokua wastani wa 'A' au 'B' watasubiri second selection ili kupangiwa shule mwezi february
Nadhani wenye kumbukumbu ama tuliopita zamani tunakumbuka huu mfumo wa second selection na adha zake ikiwa ni pamoja na;
1.Mtoto akiwasili shuleni baada ya chaguo la pili anawakuta wenzie wamesogea kimasomo kiasi flani kwahiyo inampa ugumu kwenda sambamba na wenzake.
2.Kuna baadhi watakaoahirisha masomo kabisa kwenye familia zenye wazazi wasio na msimamo wa elimu,taani wengine watakua washakabidhiwa biashara za kuisaidia familia.
3.Inamuathiri mtoto kiisaikolojia na kujiona looser na aliowakuta wamemzidi mno na hii inamtengenezea inferior state itakayomuathiri kwenye perfomance yake.
Mi nadhani huu mfumo hauna maana kama mtu ataweza kwenda shule february kwanini asipelekwe sasa hivi???
Mbona miaka kadhaa nyuma baada ya kuanzishwa shule za kata iliwezekana???