Uchaguzi 2020 Mfumo wa Majimbo wa Lissu na CHADEMA unatumika katika Mataifa na Taasisi kubwa duniani kuleta ufanisi wa kimaendeleo

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
31,617
37,815
Wanangwa,

Jana nilikuwa kanisani, mimi ni m- KKKT, na kama mnavyojua KKKT ni moja kati ya Taasisi kubwa sana hapa Tanzania ya kidini. Sasa wakati Mzee wa kanisa anasoma matangazo kikaja kipengele cha mapato, akasoma yote kisha akasema "Baki usharikani ni Tshs kadhaa", pia akataja asilimia iliyokwenda Jimboni.

Hapo hapo nikaikumbuka hoja ya Lissu, kumbe makusanyo yote ya sadaka hayaendi moja kwa moja Jimboni (Dayosisi) bali kuna asilimia tu ndiyo inakwenda na nyingine yote inabakia usharikani kutekeeza mambo ambayo wanaona bado hawajayamaliza kwa sababu matitizo ya usharika wetu si sawa na matatizo ya sharika zingine. Kwa mfano sisi tunaweza kuwa tunahitaji kujenga nyumba ya mchungaji lakini wenzetu wa sharika nyingine wao nyumba washajenga tayari ila wanahitaji gari la kanisa ama kujenga kituo cha kulelea watoto yatima nk.

Naungana na Lissu kwamba ukitaka kujenga Taasisi yoyote imara duniani ni lazima ukaimishe madaraka ya kibajeti katika kila ngazi ya kiuongozi. Na kwa kutumia mfumo huu wa Serikali za majimbo zenye mamlaka hata rushwa itapungua sababu tukitaka kumpa mtu atujengee barabara ama shule tunamjua fika hadi nyumbani kwake na kama akituzingua basi tunamshughulikia. Sasa huu ndiyo uhuru tulioulilia mwaka 1961 toka kwa mkoloni, kuamua nini kianze na kipi kisubiri kutokana na mapato yetu wenyewe.

Kwa hiyo maamuzi ya nini kifanyike kwenye Usharika wetu hatugonji Dayosisi kutuamulia hapana TUNAAMUA WENYEWE, wao tunawajulisha tu. Mahesabu ya hela zetu tunayo wenyewe.

Hiki ndicho Lissu cha ChademaDM wanamaanisha, na tangu jana nimekuwa muumini mkubwa wa Serikali ya majimbo.

 
Salamu kwako Tundu Antiphas Lissu, Shalom,

Leo napenda kukwambia rasmi kuwa, Kura yangu iko kwako! Na hii ndo sababu yangu kuu ya kukupa kura!

Katika maisha yangu nimekuwa nikifanya utafiti sana juu ya dhana ya umasikini wa watanzania na Tanzania kwa ujumla, Moja ya sababu ambayo niligundua kwenye utafiti wangu ni kuwa Tanzania tuna mfumo mbovu sana wa utawala ambao vyovyote vile hatuwezi kuendelea kwa mfumo huu!

Mfumo huu ninaousema ni mfumo kuwa fedha zote za watanzania zinakusanywa na kuwekwa chini ya mtu mmoja( raisi ambayo yeye ndo anayeamua kuwa hizo fedha zigawanywe kivipi).

Madhara ya mfumo huu ni kuwa umeondoa uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, umeondoa ubunifu kwa wananchi na viongozi na mwisho umepelekea tabia ya ombaomba na unafiki kwa wananchi na viongozi.

Mfumo huu pia umechochea ufisadi wa kiwango kikubwa sana kwa wananchi na viongozi na kama Kuna mtu anabisha Leo hii aniambie maisha ya ukwasi wanayoishi maraisi wastaafu yametokana na nini?

Hapa Tanzania hakuna raisi mstaafu mwenye maisha ya utajiri wa kuwaida. Wengi wana utajiri mkubwa wa real estate, kilimo kikubwa na hata pia makampuni makubwa ya uzalishaji. Na kibaya ni kuwa vyote hivi huwa wanavipata wakiwa maraisi. Sababu ya haya yote ni kuwa tumekuwa na mfumo wa kuziweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.

Leo hii raisi ni kama Mungu hapa Tanzania. Kila aendapo watu ni kulia shida, awafanyie hiki na awaletee hiki, haya yote ni kwa sababu ya mfumo mbovu tulionao ambao umeondoa uwajibikaji na ubunifu kwa watanzania na viongozi wetu.

Kwa nini Mfumo wa Majimbo ndo suluhisho wa haya yote?
1. Mfumo wa majimbo utafanya hela zote zinazokusanywa kwenye sehemu husika zitumike kwa matakwa ya wananchi wa sehemu husika mf. Kujenga barabara , hospitali, shule bora na huduma bora za Maji na umeme!! Hili litafanya wananchi wasiwe wajinga kwa viongozi wao na kamwe was iwe ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa viongozi wao.

2. Mfumo wa majimbo utachochea ubunifu kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali bora za uzalishaji ili majimbo yao yakusanye fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yao.

Kama jimbo husika linategemea kilimo basi wananchi wa hilo jimbo watafanya kilimo bora na watakifanya cha biashara ili wapate mapato mazuri ya kuendeleza jimbo lao kimiundombinu na Pia kimaendeleo. Hakuna sehemu watu watalala au kuwa wazembe na watakuwa wakali kwa viongozi wao kuwahamasisha wawe agressive kwenye kubuni miradi bora ya maendeleo kwa maendeleo yao.

Mfumo huu utatengeneza wananchi wanaojiamini na Kuwajibika kweli katika kutunza rasilimali zao ili ziwasaidie wao na uzao wao. Wananchi hawatakuwa wazembe na watawawajibisha kweli viongozi wasio wabunifu kwenye kutengeneza vyanzo vya mapato kwa sababu watakuwa wanajua bila vyanzo vya mapato bora na vya uhakika kwenye maeneo yao basi watakuwa nyuma kimaendeleo na hawataweza kunsurvive.

Mfumo wa majimbo utafanya kama sehemu Kuna mbuga za wanyama basi wananchi wa maeneo husika wazitunze rasilimali kweli kwa sababu watajua kweli bila mbuga hizo utalii utakufa na hawatapata mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao, kujenga barabara na mitaa bora, kuhudumia Bima za afya na madawa hospitali. Kwa iyo Kama jimbo litategemea utalii basi watautunza na kuuthamini kweli utalii.

Kama jimbo linategemea viwanda au biashara basi jimbo hilo litatunga Sera bora ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara kwa sababu wananchi wa sehemu husika watajua bila hivyo basi hawawezi pata mapato ya kununulia dawa, kupata Maji safi na salama na kujenga barabara nzuri!

Kama jimbo husika linategemea kilimo na migodi basi wananchi wa viongozi wa maeneo husika wataumiza kichwa kuweka Sera bora katika hayo maeneo ili kuhakikisha zinawapatia mapato makubwa ya kufanya miradi ya maendeleo. Watu watajiona kweli kuwa wao ni sehemu sahihi ya maendeleo husika.

Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!

Mfumo huu wa sasa umefanya watanzania tudharauliwe na viongozi na kuendeshwa Kama watoto wadogo kuwa tusipowachagua watu wao basi tusahau maendeleo kwa sababu wao ndo wanaamua hela zetu wazigawe vipi!! Hii sio sawa kabisa.

Mfumo huu wa sasa umesababisha watu kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao kuwa kila wakimuona Raisi basi wamnyenyekee kama Mungu n kumuomba hiki na kile. Kama Raisi tunaomba Maji, barabara, umeme na shule bora.

Kwa maendeleo ya kweli ni lazima Watanzania tuamue kwenye uchaguzi huu kumchagua Tundu Antiphas Lissu ili atubadirishie mfumo.

Hamasisha watu wengi zaidi kumchagua Lissu na Chadema kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania na Watanzania!

Sambaza kwa watu wengi zaidi waelimike pia!

Asanteni!
Lord denning.
 
SWALI NI: JE, MFUMO WA MAJIMBO UTALETA UKABILA NA KUFANYA BAADHI YA SEHEMU TANZANIA KUTOKUWA NA MAENDELEO?

Amani iwe nanyi wadau!

Leo napenda kuwajibu wana CCM wanaosema mfumo wa Majimbo utachochea ukabila na kusababisha baadhi ya maeneo kutokuwa na maendeleo,

Ukweli ni kuwa kamwe mfumo wa majimbo hautaleta ukabila na kamwe hautoleta kudumaa kwa maendeleo kwenye baadhi ya sehemu kama propaganda za CCM zinavyosema! Hii ni kwa sababu zifuatazo;

1. Jimbo la Kati- Mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora na Morogoro.
Mikoa hii ina utajiri mkubwa wa mazao kama Tumbaku, Zabibu, Alizeti, Karanga, Asali na Mtama, Mpunga,Ndizi na Mahindi(vya mkoa wa Morogoro) Haya mazao tukipata viongozi wenye akili sio hawa wa CCM yataendelezwa vizuri na kuingiza mapato makubwa kwenye jimbo hili la kati.

Kuna uhitaji mkubwa sana wa Karanga na Asali kwenye masoko ya Asia na Ulaya. Haya mazao yakiendelezwa kisasa na kibiashara jimbo hili litanyanyuka mno kiuchumi. Hata viwanda vya mvinyo tu Dodoma vikiendelezwa na kutangazwa vizuri na mvinyo ukitengenezwa mzuri mapato

Pia kwenye jimbo hili kuna maliasili mbalimbali za wanyama kutokana na mapori ya akiba kama swagaswaga, manyoni na mapori ya Tabora ambayo pia yana tembo wengi na mbao nyingi. Hivi vitu vikiendelezwa na kutangazwa vizuri vitakuwa source kubwa ya mapato kutokana na uwindaji na utalii. Haya pia ni mapato makubwa sana.

Mkoa wa Morogoro una mbuga za wanyama kama mikumi, udzungwa na nyingine nyingi ambazo pia zitaleta mapato ya utalii.

Pia Kuna madini Kama dhahabu mikoa ya Tabora na Singida na Morogoro ambayo yakiendelezwa vizuri yataketa mapato makubwa sana kwenye maeneo haya. Hapo sijaweka biashara za mifugo, wanyama na viwanda ambavyo navyo vipo na vitakuwepo kwenye jimbo hili.

Kwa hiyo dhana ya Jimbo la Kati kuwa masikini si kweli.

2. Jimbo la Mashariki- Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Pwani
Jimbo hili chanzo kikuu cha Maputo kitakuwa Bandari, Viwanda na Biashara. Kodi nyingi itakusannywa kutoka maeneo haya na kwa kweli itaendeleza kweli jimbo hili.

3. Jimbo la Kusini- Mikoa ya LINDI, Mtwara na Ruvuma
Jimbo hili lina utajiri mkubwa wa gesi na mazao ya korosho na mbaazi bila kusahau viwanda, bandari na uvuvi. - Hili jimbo litakuwa na na mapato makubwa sana ambayo yatajenga shule bora, hospitali, madawa, kujenga barabara nzuri na makazi bora.

Pia jimbo hili litakuwa na mapato ya utalii kutokana na hifadhi ya Selous na mapori ya akiba ya mkoa wa Ruvuma.

4. Jimbo la Nyanda za Juu kusini- Mikoa ya Iringa, Njombe,Songwe na Mbeya
Jimbo hili ndo mzalishaji mkuu wa chakula kinacholisha Tanzania, Afrika ya kati na Afrika mashariki. Kilimo na Biashara ya Chakula kitaingiza mapato makubwa sana kwenye jimbo hili. Biashara pia ya mbao na utalii kutokana na hifadhi za kipengele, Ruaha, Kitulo na Rungwe vitaingiza mapato makubwa sana kwenye jimbo hili.

Mipaka ya Zambia na Malawi pia itaingiza mapato makubwa kutokana na biashara bila kusahau viwanda na kilimo cha mashamba makubwa ya mpunga, maparachichi, nyanya, chai na miti.

5. Jimbo la Magharibi- Mikoa ya Katavi, Rukwa, Kigoma na Kagera- Mikoa hii ina utajili wa kilimo hasa cha mazao ya mahindi, tumbaku, mawese, miwa pamoja na miti pia. Pia ina uvuvi wa maziwa ya Tanganyika na Victoria.

Mikoa hii pia ina utalii wa mbuga za wanyama kama hifadhi za Gombe, Kimisi, Katavi, Mto Maragarasi pamoja na biashara kubwa na kodi katika mipaka ya nchi za Congo( Bandari) , Burundi, Rwanda na Uganda! Itoshe tu kusema kuwa jimbo hili pia litakuwa na mapato mengi sana ambayo yataboresha miondombinu ya barabara, hospitali , mashule na huduma za Maji safi na salama!!

6. Jimbo la Kaskazini- Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Mara.
Jimbo hili litakuwa na na chanjo kikuu cha mapato ambacho ni utalii na pia madini ya mikoa ya Arusha, Manyara na Mara. Utalii wa mbuga za kilimanjaro, Ngorongoro, Serengeti na Manyara utaingiza pesa nyingi sana za kuboresha miondombinu na huduma za msingi

Biashara pia na kodi kwenye mipaka ya Kenya kwa sehemu za holili,Silali na Arusha italeta mapato mengi Sana. Na hapa hujaweka kilimo cha ndizi, tangawizi na mifugo bila kusahau viwanda.

7. Jimbo la Kanda ya Ziwa (Victoria)- Mikoa ya Simiyu, Geita, Shinyanga na Mwanza.
Jimbo hili ndo kitovu cha madini Tanzania. Pia lina mbuga na mapori ya akiba mengi bila kusahau viwanda na biashara ambavyo vitaingiza napata mengi sana na kuleta impact kubwa sana kwenye uchumi. Uvuvi pia utaleta mapato mengi sana.

Dhana ya ukabila haiwezi kupata nguvu kwenye mfumo huu kwa sababu Kuna mchanganyo mkubwa wa makabila kwenye majimbo haya!

Pia chini ya mfumo huu kila mwananchi atawajibika kufanya kazi halali na kujituma kwa sababu atajua bila kufanya kazi hawezi endelea na sehemu yake haiwezi kufanya vizuri katika huduma za msingi.

Chini ya mfumo huu pia hakutakuwa na unyanyasaji wa wananchi kwa sababu wananchi watakuwa wanajua kuwa Mapato yao ndio yatakayowaletea maendeleo!

Viongozi pia watawajibika moja kwa moja kwa wananchi na kamwe hawatofuja mali kwa wananchi wala kuwagawa kwa misingi ya kikabila au kichama kwenye maendeleo.
 
Chukueni mtazamo mpana zaidi wa suala la ulinzi na usalama kwa taifa. Tusijilinganishe na Kenya ambayo bajeti yao uchumi wake pia hauwezi kuulinganisha na wakwetu. Mentality ya watz na uvivu na wizi je vitaondoka kwa kuweka majimbo?
 
Chukueni mtazamo mpana zaidi wa suala la ulinzi na usalama kwa taifa. Tusijilinganishe na Kenya ambayo bajeti yao uchumi wake pia hauwezi kuulinganisha na wakwetu. Mentality ya watz na uvivu na wizi je vitaondoka kwa kuweka majimbo?
Iyo mentality ya watanzania imetengenezwa na nani Kama sio CCM? Ndo mana tunataka tuwape uongozi watu wapya ili walete mentality za uwajibikaji na kuheshimu sheria.
 
Sasa hivi mapato yote ya hadi masoko ya vijiji yanaenda juu halafu mzee baba anagawa inavyompendeza maana hela ni zake! Akiamua kugawa mabarabarani huko sawa; akiamua eneo hili lisipate mgao kwa sababu hawakunipigia kura hewala!

Akiamua hapa wale mema ya nchi kwani siwezi kuwatupia mbwa chakula cha watoto hewala baba mamlaka ni yako; wewe ndiwe alfa na omega; nani kama wewe; uishi milele ee mfalme!
 
Sasa hivi mapato yote ya hadi masoko ya vijiji yanaenda juu halafu mzee baba anagawa inavyompendeza maana hela ni zake! Akiamua kugawa mabarabarani huko sawa; akiamua eneo hili lisipate mgao kwa sababu hawakunipigia kura hewala! Akiamua hapa wale mema ya nchi kwani siwezi kuwatupia mbwa chakula cha watoto hewala baba mamlaka ni yako; wewe ndiwe alfa na omega; nani kama wewe; uishi milele ee mfalme!
Mfumo wetu ni mbovu sana
 
Tungeangazia NCHI ZA KIAFRIKA zinazotumia mfumo huu,tuone ufanisi wake badala ya kuangazia vitaasis tu.

KKKT yenyewe unayoipigia chepuo ina migogoro kibao isiyoisha juu ya matumizi mabaya ya fedha.
Kesi ya Munga imeishia wapi?

Na sidhani kama CDM yenyewe (wapiga filimbi ya majimbo) kama wanatumia mfumo huo kugawa ruzuku ili kila kanda/jimbo lijisimamie lenyewe!
 
Back
Top Bottom