Mfumo wa kusaili wanafunzi wa VETA unahitaji kuangaliwa upya

Mr Kind

Senior Member
Mar 4, 2017
178
308
Sote tunafahamu kwamba VETA ni sehemu sahihi ya watu kuendeleza au kuibua vipaji vyao katika fani mbalimbali.

Ni bahati mbaya sana VETA haipewi kipaumbele kiasi kwamba vyuo vingi havinauwezo wa kuchukua wanafunzi wengi kulingana na mahitaji.

Ili kuendena na miundombinu waliyonayo, VETA huwapa mitihani wanafunzi wote wanaoomba kujiunga na fani mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa si kila mmoja mwenye uwezo na ujuzi na fani fulani ana uwezo pia wa kuyamudu masomo rasmi ya darasani. Hivyo kwa mfumo huu wa interview za masomo ya shuleni, vijana wengi hubaki mtaani kwa kushindwa kupata alama zinazohitajika.

Ni vema sasa serikali na wizara inayohusika na VETA waangalie upya namna ya kuwasaidia vijana wenye tamaa ya kujifunza ujuzi fulani lakini hawana uwezo wa kumudu mitihani wanayopewa ambayo kwa kweli haiendani na kile wanachotaka kufanya.
 
Back
Top Bottom