Mfumo wa kuendesha serikali yetu ni halali?

Kilamuluzi

Senior Member
May 20, 2014
116
170
Habari ndugu wana jamvi,

Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sana juu ya uendeshaji wa hii serikali yetu juu ya matumizi ya vyombo vya umma kama ni halali ama hapana!

Nianze na hivi vichache;mfano mtu anateuliwa kuwa waziri,je,ni lazima apewe nyumba ya kuishi na serikali?ni lazima ahudumiwe gharama za chakula,kusomesha watoto wake shule na serikali?kama ni sawa kuna sababu gani za kumlipa mshahara mtu anaehudumiwa na serikali namna hii?

Ndugu zangu naombeni mnisaidie kama haya ni matumizi sahihi ya kodi zetu kwa viongozi tulionao,na kama sio sahihi ni kwa nini tusibadili mfumo wa kuendesha serikali yetu?

Mfano mzuri upo hapa Rwanda,wakati waziri anateuliwa kuwa waziri alikuwa kwenye nyumba yake,hivyo serikali haiwajibiki kumpatia nyumba nyingine ataendelea kutumia hiyo hiyo aliyokuwa nayo kabla hajawa waziri.

Kingine matumizi ya magari ya serikali ni wakati wa kazi tu,baada ya hapo gari zote za serikali zinalala yadi ya serikali hakuna gari inalala nje ya hii yadi labda kwa kibali maalumu.

Kuna mambo mengi ambayo tunahitaji kuyabadilisha ili tuweze kuongozwa vizuri na hawa viongozi wetu bila kuathiri au kugharimu pesa nyingi za mlipa kodi wa Tanzania.

Tafadhali naomba mchango wako wa mawazo juu ya hii kadhia iliyopo hapa nchini kwetu Tanzania.
 

makubazi

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
2,048
1,195
Ooyooo Nahau penye kundi la vipofu chongo huwa mfalime na mwenye macho hambiwi tazama na haya yote ni yakujitakia sisi wenyewe na huku tunalalamika ya tumirogwa na kumbe tumejiroga sisi wenyewe lakini kila jambo huwa na mwanzo na mwisho wake
 

Kilamuluzi

Senior Member
May 20, 2014
116
170
Kitu ninachotaka,je tufanyeje,kuepuka matumizi yasiyokuwa ya lazima ili kuiondolea serikali matumizi makubwa?Ni njia gani itumike kuondoa hii kadhia,ama tuitumie katiba kuzuia matumizi yasiyokuwa na ulazima kwa serikali?
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Mkuu unazungumzia serikali tatu ya wapi sisi muundo wa serikali yetu ni serikali mbili haya wewe unayatoa.
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Mawazo mengine sijui mnayatoa wapi haya mambo ya serikali tatu au mbili yanafika tamati mwezi wa nane watanzania tunaubia na serikali mbili hizi tatu za ukawa na ulaghai wao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom