Mfumo wa kompyuta wa tume ya uchaguzi ya Zambia waingiliwa

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
10,489
13,770
WanaJF katika habari za asubuhi redioni nimesikia kwamba mfumo wa kompyuta wa tume ya uchaguzi ya Zambia imeingiliwa na watu wanaoingiza matokeo yasiyo rasmi. Nilivyosikia nikakumbuka hapa kwetu malalamiko ya wapinzani hasa CDM walivyolalamikia tume ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu uliopita kwamba inatangaza matokeo ambayo siyo halali na wakawaomba wasitishe. Nikakumbuka pia habari ambazo zilikuwa zinaongelewa sana za mtoto wa mkulu ambaye aliyemleta rafiki yake ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kompyuta kutoka India. Hivyo nikahitimisha kwamba madai ya CDM yalikuwa na ukweli ukizingatia na hili lililotokea huko Zambia au nyie mnalionaje hili.
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
7,797
9,831
Mtikila alisema juzi kuwa Magamba ndo waalimu wa wizi wa kura East and Central Africa. It doesnt suprise me.
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom