Mfumo wa elimu yetu Tanzania

bheri

Member
Mar 1, 2018
98
78
Habari za leo wanajamvi, pole na majukumu ya kila siku ya kulijenga Taifa letu.
Nashauri wanafunzi wasome kuanzia darasa la 1 & 6, na wafundishe masomo matatu tu. Yaani Hisabati, Sayansi na Lugha.

Na wahakikishe wanapowafundisha wanafunzi mfano somo la Hisabati, wajitahidi wawe wameandaa karakana au chumba maalumu kilichojaa zana za kufundisha na kujifunzia Hisabati kwa kila level.

Somo la Sayansi vile vile waandae vitabu vya kutosha kwa maana kiada na ziada, zana zote za kisayansi kwa kila level na wanafunzi wapewe muda wa kutosha kwenda kwenye karakana hizo kukifunza na wao kujaribu kutengeneza zana zao nazo zitunzwe ziwe Ni sehemu ya kumbu kumbu.

Na kwa somo la Lugha vile vile wawe na zana za kutosha kufundisha na kujifunzia. Baada ya hapo wanafunzi watumie muda mwingi Sana kwenye kutenda kuliko nadharia.

Baada ya kumaliza mwanafunzi aseme yeye angependa anataka asomee Nini lakini kwa kuzingatia na ufaulu kwenye masomo yake hapo anaweza kusaidiwa na wazazi pia mwalimu wake. Kwa maana Kwanza akifika form one kule aende kuspecialize kwenye somo mojawapo kati ya Yale masomo matatu achague moja tu.

Na o level wanafunzi nashauri wangesoma miaka 3 tu. Na huko tuzingatie mwanafunzi atende zaidi kuliko nadharia maana kwamba zile karakana ziwe na zana za kutosha kwa mwanafunzi kujifunza.

Akimaliza aende Advance mwaka mmoja tu huku akiendelea kuspecialize kile anachokipenda kwa kufanyia practical za kutosha.

Mwisho mwanafunzi aende chuo huko atasomea kile ambacho ana msingi mzuri was kutoka chini. Huko chuo atasoma miaka kulingana na ugumu wa kozi husika huko akiendelea na vitendo zaidi kuliko nadharia.

Mimi nakuhakikishia huyu mwanafunzi akimaliza shule, chuo hawezi akarudi mtaani akawa hajui Cha kufanya. Naamini ikitolewa Elimu ya Aina hii tunaweza kupunguza utegemezi kwenye jamii kwa kiwango kikubwa Sana kuliko ilivyo Sasa. Vijana wataweza kujiajiri, kuajirika kiurahisi lakini ubunifu na ugunduzi kwenye jamii yetu utaongezeka Sana.

Mwisho tutakuwa na jamii Bora iliyokombolewa.

Naomba kuwasiliana.
 
Baada ya kumaliza form six, wasiende jeshi, wapangiwe vyuo vya ufundi veta, kwa miezi 4, then ndio waende vyuo vikuu.
Sahihi Sana Kaka, mi Nina vijana wawili mmoja yupo la darasa la 5 mwingine la sita, niliona wakitoka shule wanakuwa loose sana.
Nikawaelekeza kila mmoja atafute viroba viwili viwili wajaze udongo kwa juu wachanganye mbolea
Baada ya hapo nikaenda dukani nikanunua mbegu za mchicha na chainizi nikawapatia vipimo sawa wakaenda kupanda nikawaelekeza wahakikishe wanamwagilia maji kila asubuhi na jion, na nikawahaidi atayefanya vizuri zaidi nitampa zawadi

Walipanda baada ya hapo mi sikutata niwafuatilie, wakaendelea na zoezi la umwagiliaji, mwisho wakaja kuniambia mchicha wetu umekomaa, nikaenda nao wote kukagua, yule wa drs la 5 mboga zake ziko vizuri nikawa nawachallenge kwa kuwauliza maswali, wenyewe wakaainisha changamoto walizokutana nazo ikiwemo kutomwagilizia kwa wakati lakini uvivu. Pale nikajifunza hawa watoto wakiendelezwa katika kutenda wanakuwa vizuri zaidi kuliko wanavyosoma darasan
 
Nyie mmesoma ukuzaji mitaala,mmefnya utafiti au mnatumia common sense?
Fafanua kuhusu Hilo la ukuzaji wa mtaala, maana naona Kama haina faida Kama mwanafunzi anamaliza shule hawezi kufanya kujitegemea kwa chochote. Bali anasubiri kuajiriwa na serikali au taasisi binafsi. Hapo watu wa mitaala mnatusaidiaje ili kuikomboa jamii yetu.
 
Mleta mada, mimi naunga mkono hoja, na jambo hilo ni zuri sana!!

Ila hapo kwenye somo la lugha, una maanisha lugha ipi!? Au zote kwa pamoja!?
 
Hapo Lugha zote kwa pamoja inatengen ezwa ratiba itayowezeshwa wanafunzi wapate maarifa ya kiswahili na maarifa ya English lakini ndani ya somo moja ambalo litaitwa Lugha.
 
Kuna nyakati natamani nijue
Wachina,wakorea,waisrael,wamarekani,wajerumani silabasi zao zikoje!?? Lakini sina uwezo huo!!!
Hebu fikiria Tanzania silabasi ya hesabu ya kidato cha kwanza in mada ( topics) 19 au 20 kama sijakosea unaenda kumfundisha mtoto wa miaka 13 cjui mamlaka husika hufanya makusudi watu wafeli au VP!!! Hill ni somo moja na yapo 12 !!! Yani Tanzania bila kubadili stail yetu ya kuchagua watendaji hatutoki !!!hii kuwapa
Watu uwaziri kama feva ni nuksi tupu!! Watu hawana uwezo wa kua creative!!ifikie mahali Waziri aombe kazi na afanyiwe interview!!! Lakini huu mfumo wa kuwapa waskaji kisa tuu mmajuana tunapata mawaziri Mshahara !!!
 
Umenena kweli mkuu.Dr.Elii Vid Waminian(kama sijakosea jina lake) anasema kupokea taarifa nyingi mwisho taarifa hizo hugeuka kuwa kelele.Yaan kuna watu wanasumbuliwa na uwepo wa maarifa/taarifa nyingi kichwani.Sisi mfumo wetu wa elimu umetufanya tuathiriwe na mapokeo kuliko uzoefu.Mwisho tumeshindwa kutumia taarifa sahii katika utendaji.Ni vema tujifunze macheche ila yenye kutumika!
 
Habari za leo wanajamvi, pole na majukumu ya kila siku ya kulijenga Taifa letu.
Nashauri wanafunzi wasome kuanzia darasa la 1 & 6, na wafundishe masomo matatu tu. Yaani Hisabati, Sayansi na Lugha.

Na wahakikishe wanapowafundisha wanafunzi mfano somo la Hisabati, wajitahidi wawe wameandaa karakana au chumba maalumu kilichojaa zana za kufundisha na kujifunzia Hisabati kwa kila level.

Somo la Sayansi vile vile waandae vitabu vya kutosha kwa maana kiada na ziada, zana zote za kisayansi kwa kila level na wanafunzi wapewe muda wa kutosha kwenda kwenye karakana hizo kukifunza na wao kujaribu kutengeneza zana zao nazo zitunzwe ziwe Ni sehemu ya kumbu kumbu.

Na kwa somo la Lugha vile vile wawe na zana za kutosha kufundisha na kujifunzia. Baada ya hapo wanafunzi watumie muda mwingi Sana kwenye kutenda kuliko nadharia.

Baada ya kumaliza mwanafunzi aseme yeye angependa anataka asomee Nini lakini kwa kuzingatia na ufaulu kwenye masomo yake hapo anaweza kusaidiwa na wazazi pia mwalimu wake. Kwa maana Kwanza akifika form one kule aende kuspecialize kwenye somo mojawapo kati ya Yale masomo matatu achague moja tu.

Na o level wanafunzi nashauri wangesoma miaka 3 tu. Na huko tuzingatie mwanafunzi atende zaidi kuliko nadharia maana kwamba zile karakana ziwe na zana za kutosha kwa mwanafunzi kujifunza.

Akimaliza aende Advance mwaka mmoja tu huku akiendelea kuspecialize kile anachokipenda kwa kufanyia practical za kutosha.

Mwisho mwanafunzi aende chuo huko atasomea kile ambacho ana msingi mzuri was kutoka chini. Huko chuo atasoma miaka kulingana na ugumu wa kozi husika huko akiendelea na vitendo zaidi kuliko nadharia.

Mimi nakuhakikishia huyu mwanafunzi akimaliza shule, chuo hawezi akarudi mtaani akawa hajui Cha kufanya. Naamini ikitolewa Elimu ya Aina hii tunaweza kupunguza utegemezi kwenye jamii kwa kiwango kikubwa Sana kuliko ilivyo Sasa. Vijana wataweza kujiajiri, kuajirika kiurahisi lakini ubunifu na ugunduzi kwenye jamii yetu utaongezeka Sana.

Mwisho tutakuwa na jamii Bora iliyokombolewa.

Naomba kuwasiliana.
Apo tatizo ni lugha ya kufundishia inasababisha tuchelewe. Kurudia rudia tu. mfano shule ya msingi wanasoma sehemu kwa Kiswahili ukifika sekondari unasoma kwa kingereza. Uku moyo kwa Kiswahili kisha sekondari unasoma kwa kingereza.

ingekua lugha ni moja toka primary tusingerudia rudia

Sent from my Nokia 2 using JamiiForums mobile app
 
Sahihi Sana Kaka, mi Nina vijana wawili mmoja yupo la darasa la 5 mwingine la sita, niliona wakitoka shule wanakuwa loose sana.
Nikawaelekeza kila mmoja atafute viroba viwili viwili wajaze udongo kwa juu wachanganye mbolea
Baada ya hapo nikaenda dukani nikanunua mbegu za mchicha na chainizi nikawapatia vipimo sawa wakaenda kupanda nikawaelekeza wahakikishe wanamwagilia maji kila asubuhi na jion, na nikawahaidi atayefanya vizuri zaidi nitampa zawadi

Walipanda baada ya hapo mi sikutata niwafuatilie, wakaendelea na zoezi la umwagiliaji, mwisho wakaja kuniambia mchicha wetu umekomaa, nikaenda nao wote kukagua, yule wa drs la 5 mboga zake ziko vizuri nikawa nawachallenge kwa kuwauliza maswali, wenyewe wakaainisha changamoto walizokutana nazo ikiwemo kutomwagilizia kwa wakati lakini uvivu. Pale nikajifunza hawa watoto wakiendelezwa katika kutenda wanakuwa vizuri zaidi kuliko wanavyosoma darasan

Na kusifu sana, kwa hatua uliyo fanya..

Embu jaribu ku wanunulia hata vikuku wawe wanafuga, ili uwape uwezo zaidi , katika kujifunza,

Usisahau kuwapa zawadi kila point unayo ona wamefanya vizuri,

Kisaikolojia hii ni nzur sana,
 
Nitafanya hivyo natamani Sana Tena Sana kungelikuwa na shule kuanzia msingi zenye utaratibu wa kufundisha nusu nadharia nusu vitendo kwa gharama yeyote wanangu wangeenda kusoma huko mwanafunzi anaelewa zaidi akiwa anatenda kwa vitendo kuliko nadharia. Imagine amejifunza kulima mchicha kwa miezi 2 akagundua changamoto chache kwa kipindi kifupi inamaaana Kama Ni endelevu anakuwa na ujuzi wa kutosha na hawezi kuyumbishwa na hawa motivation speaker, sijui wekeza kwenye kilimo Cha mchicha na haujui changamoto zilizopo. Mwisho unaingiza mtaji na kujikuta unapoteza.
 
Mimi siafiki, dunia sio ya sayansi peke yake, mimi ningependa ku propose a mix match kati ya masomo yanayoendana/yanayohitajika kwenye mazingira yetu (Environment - specific), Kilimo, Computer/IT na vitu vinahitajika duniani na kwetu (General), Lugha, Business na Hesabu, vitu hivi vifundishwe basics, secondary ndio waspecialize.
 
Sawa ninaposema Sayansi humo Kuna package kubwa Sana, somo Kama agriculture Lina uhusiano mkubwa na Sayansi, somo kama Geography ile Ni Sayansi lakini someone Kama computer Lina uhusiano mkubwa na mathematics na Sayansi,
Ndio maana ukiangalia mtaala wa Sasa wa elimu, somo la sayansi linaitwa sayansi na teknolojia humo ndani wanafunzi wanajifunza Mambo mengi ya computer. So wakiweka mipango vizuri sioni Kama wanaweza kushindwa kinachoitaji Hapa Ni utashi wa watunga Sera.
 
Back
Top Bottom