Mfumo wa Elimu ya juu nchini, Mwingiliano wa siasa na Uzembe katika Tanzania ya leo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa Elimu ya juu nchini, Mwingiliano wa siasa na Uzembe katika Tanzania ya leo.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Calnde, Jan 31, 2009.

 1. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikitafakari kwa muda juu ya mfumo wa elimu ya juu kwa nchi yetu na mchango wake katika kuleta maendeleo ya Mtanzania wa sasa.Ni dhahiri katika elimu ya juu ndipo ambapo taifa hili linajengwa kwa misingi ya kutoa wataalamu ambao watafanya kazi kwa maslahi ya Taifa. Mfano kwa hali halisi ya sasa ni dhahiri kwamba viongozi wengi aidha kwa kupenda au kwa lazima watayaacha madaraka yao na hivyo kuacha pengo ambalo ni dhahiri litahitaji kujazwa. Changamoto iliyopo ni namna gani wasomi waliopo chuoni ambao wengi wao wana corrupt mind,waliopo under corrupt system watakavyoweza kutoka na kuingia in a more corrupt system (Government with its department plus private sectors),waweze kuleta tija kwa Taifa.Hapa tuna mengi ya kufanya
  1. ADMINISTRATION AND MANAGEMENT REFORMS
  Kwa mtazamo wangu tunahitaji mabadiliko makubwa sana katika mfumo wa utawala unaosimamia elimu ya juu.Kuanzia waziri mhusika,mpaka kwa wakurugenzi wa taasisi mbali mbali zihusikazo na elimu(mf Bodi ya mikopo) mpaka wakuu wa vyou vyenyewe naona kuna tatizo.Hapa yanahitajika mabadiliko ambapo watu watakaowekwa kushika nafasi hizo pamoja na mabadiliko yatakayofanyikayalenge kuboresha elimu ya juu.

  2.SEPARATION BETWEEN POLITICS AND EDUCATION SYSTEM
  Kwa sasa siasa na elimu vinalazimishwa kuwekwa pamoja.Eneo linalohitaji mabadiliko ya kisera zinaingizwa siasa.Kwa makusudi kabisa vyama vya siasa vimeamua kuibaka elimu ya juu ili kurecruit members.At last watu wanasoma kwa lengo la kukitumikia chama fulani watakapomaliza badala ya kutumikia taifa.

  3.MIND TRANSFORMATION AMONG STUDENTS
  Kwa sasa hali ni mbaya katika minds za wanafunzi wa elimu ya juu. wengi wanasoma ili kushika fedha soon watakapomaliza and how to become famous. mbaya zaidi mahusiano na ukosefu wa maadili vinawasumbua wawapo chuoni. hapa mabadiliko ni ya muhimu.Ni vizuri wanafunzi wasome wakijua wanalengo moja tuu...KULITUMIKIA TAIFA KWA UAMINIFU na mengine yatafuta. Bila nafsi za wanafunzi kukomboka tutakuwa tunazalisha wasomi wajinga kuliko walivyokuwa wakati wanaingia vyuoni!

  4.SERIOUS GOVERNMENT EFFORTS TO IMPROVE OUR EDUCATION
  Lazima kwa makusudi kabisa serikali iweke mpango wa kuinua elimu yetu....na kwa hapa msingi uwekwe kuanzia elimu ya msingi ili kuepuka kuwa na wasomi wasioweza kujieleza. Ni dhahiri wakati nchi nyingine zikipiga hatua sisi tumesimama.Ndo maana udsm iliyotamba enzi hizo na shule kama mzumbe,ilboru,tabora boys, kibaha, na msalato zimezikwa na vyuo na shule mpya na za kisasa. Serikali ikusudie kuzalisha wasomi hata kwa kuwapeleka nje wale wanaofanya vizuri ili wewe walimu wa wenzao waliobakia hapa. Naamini tikitaka akina Baregu,Shivji,Nditi,Luhanga,othman na wengine wengi wanaweza kuzaliwa tena.

  5.SEMINA MAALUMU KWA WANAVYUO
  mwisho nionavyo mimi kuwepo na mfumo maalumu wa semina katika vyou vyetu.Mathalani semina za uongozi bora( nadhani zingesaidia kupunguza migomo) na makongamano yatakayo wakutanisha na wataalamu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.Hii ita wa-inspire na kuweka moyo wakujituma ili wafikie walipo wao. Exchange programmes na study tour kwa vyuo vya nchi zilizoendelea nadhani zitasaidia pia kama zikifanyika kwa umakini.

  Wanafunzi wakiondo dhana ya kulalamika kila wakati na kuamua kujituma,watawala wakiamua kukatiza likizo ya kufikiri na kuanza kufikiri katika misingi ya kulitumikia taifa, bajeti ya kutosha ikitengwa kwa swala la Elimu, na wahadhari waliopo wakaamua kwa moyo kufanya kilicho wafanya wawe wahadhiri.........Naweza kuona mafanikio,si katika elimu tuu bali hata ndege ya uchumi itapaa kweli na si yale Maigizo ya Lowass.

  Kwa uchache nawasilisha kwenu wakuu......
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inabidi nitulie; na haka kawikiend maana analysis imekwenda shule;

  Tanzania tatizo wengi tu mabwege ( ingawa Mwakyembe alisema sasa tumebadilika)
  2.SEPARATION BETWEEN POLITICS AND EDUCATION SYSTEM
  Kwa sasa siasa na elimu vinalazimishwa kuwekwa pamoja.Eneo linalohitaji mabadiliko ya kisera zinaingizwa siasa.Kwa makusudi kabisa vyama vya siasa vimeamua kuibaka elimu ya juu ili kurecruit members.At last watu wanasoma kwa lengo la kukitumikia chama fulani watakapomaliza badala ya kutumikia taifa.

  Hili si jambo baya kama unafanya hili kwa nia ya kuwakomboa watu sio kuwalaza; ukimpata mtu kutoka chuo kwa rushwa/na uongo hapo unaharibu; ila kama ni kwa nia ya ukombozi; kote duniani mifumo inaruhusu siasa ktk level hiyoo maana kijana sasa amekomaa anajiandaa kupigania wananchi wake after school; (nimeseme tu kumbuka bado na kawikiend kamenishika so huenda sijafike palee...)
   
 3. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  tatizo ni kwamba wanapoingiza siasa hizi lengo linakuwa si kuwaandaa vijana bali ni kama vile kuwalaza. Inakusudia kuwafanya watoke chuoni kutumikia chama tena kwa maslahi binafsi wala si ya chama.
   
 4. M

  Mkubwa Dawa Member

  #4
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tatizo na suluhisho zuri ni kwa wanasiasa wetu kuwapa Uhuru wasomi ili wawe changamoto kwa taifa letu katika kuleta maendeleo,na sio kuwaingilia kwani hilo litasababisha wasomi ambao watakuwa hawachangii vilivyo katika kuikosoa serikali itakapokosea.
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu Calnde, mabadiliko unayopendekeza ni ya mfumo, watu au vyote?
   
 6. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama umenisoma vyema nasisitiza juu ya mabadilko yanayolenga kurekebisha mfumo mzima ambao kwa sasa unapwaya. Hili linajumuisha watu na vingine vilivyopo mfumoni pamoja na sera zinazo weka mifumo hiyo.
   
 7. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wakati mwalimu aliposisitiza sera ya elimu for self reliance watu walisoma kwa bidii (na of course elimu ilikuwa bora) wakijua wanatoka kwenda kulitumikia taifa maana hata Taifa limejitahidi kuwasomesha wao kwa mazingira mazuri. Hakuna mtu aliyekuwa anamaliza first degree kama amefanya vizuri asiwezeshwe kuadvance. Tatizo la sasa Elimu imekuwa ni jukumu la mzazi na mtoto sasa anakuwa ni parents assets and not public assets. Anapotoka anawaza namna ya kijitajirisha yeye na familia yake and at last tunakuwa tunazalisha mafisadi na si wazalendo
   
 8. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Matokeao ya kidato cha nne yametoka. Ukiyatazama kwa makini utaona ni kuongezeka kwa shule za kata na vile vile kuongezeka kwa kiwango cha kufeli. Katika hali ya namna hii tutegemee vipi kuzalisha wasomi watakaoweza kusimama kwa dhati kutetea maslahi ya taifa?
   
  Last edited: Feb 12, 2009
 9. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa mfano, utakuta shule ya kata imehitimisha wanafunzi 90. Matokeo yake yapo hivi,
  Div 1=0
  Div 2=0
  Div 3=1
  Div 4=9
  Div 0=80.
  hapa ni lazima tujiulize atakayeweza kupata elimu ya juu ni yupi,atasomeshwa na nani na kwa maslahi ya nani?
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sidhani kuwa mwanafunzi akisoma kwa lengo la kushika pesa hapo baadae ni kosa. Kosa linaweza kuwa aina ya ndoto zake za jinsi atakavyoshika hizo pesa. Nadhani changamoto yoyote inahitajika ili kumfanya mtu asome zaidi na hatimaye kufanikiwa ki-elimu. Kama pesa atakazopata baada ya kumaliza masomo itakuwa ni changamoto muhimu, basi na iwe hivyo. Sidhani kuwa kuna mtu atakaefanya jambo bila malengo yanayowezekana. Ukweli unabaki kuwa, sio kila atakaejitahidi ki-elimu atapata nafasi za kujenga nchi kama ndoto zake zinavyomtuma (kwa kiwango anachotaka). Nafasi hizo ni chache kwa sasa. Nadhani umefika wakati wa wanafunzi kufikiria jinsi watavyoendesha miradi itakayowasadia kiuchumi na wakati huo huo kulisaidia taifa kujikwamua.

  4.SERIOUS GOVERNMENT EFFORTS TO IMPROVE OUR EDUCATION
  Lazima kwa makusudi kabisa serikali iweke mpango wa kuinua elimu yetu....na kwa hapa msingi uwekwe kuanzia elimu ya msingi ili kuepuka kuwa na wasomi wasioweza kujieleza. Ni dhahiri wakati nchi nyingine zikipiga hatua sisi tumesimama.Ndo maana udsm iliyotamba enzi hizo na shule kama mzumbe,ilboru,tabora boys, kibaha, na msalato zimezikwa na vyuo na shule mpya na za kisasa. Serikali ikusudie kuzalisha wasomi hata kwa kuwapeleka nje wale wanaofanya vizuri ili wewe walimu wa wenzao waliobakia hapa. Naamini tikitaka akina Baregu,Shivji,Nditi,Luhanga,othman na wengine wengi wanaweza kuzaliwa tena.[/QUOTE]

  Jitihada kubwa ya Serikali inayohitajika hapa ni kuwekeza zaidi katika maendeleao ya shule kwa kuongeza majengo, maabara, na vifaa vya kufundishia, kuendeleza walimu (kuongeza idadi, na uwezo wa kila mwalimu na kutoa motisha kwa walimu kufanya kazi kwa bidii na maarifa) na Kusimamia utekeleza, utunzaji na maendeleo ya shule zote nchini.

  Vile vile, serikali inabidi iwe na watu wenye ubunifu wa kubadilika kutokana na wakati kwa kubuni mitaala (syllabus) zinayoendana na mahitaji ya ulimwengu wa sasa. Kufundisha kiholela hakusaidii. Lazima malengo ya ukuaji wa nchi yaendane na uwekezaji katika elimu.

  Tuache kuiga wenzetu kwa kila kitu (tuchambue). Tunatakiwa kubuni yanayowezekana kwetu ambayo si lazima yawezekane kwa wengine. Kwa maana yanayowezekana kwa wengine si lazima pia yawezekane kwetu.
   
 11. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jitihada kubwa ya Serikali inayohitajika hapa ni kuwekeza zaidi katika maendeleao ya shule kwa kuongeza majengo, maabara, na vifaa vya kufundishia, kuendeleza walimu (kuongeza idadi, na uwezo wa kila mwalimu na kutoa motisha kwa walimu kufanya kazi kwa bidii na maarifa) na Kusimamia utekeleza, utunzaji na maendeleo ya shule zote nchini.

  Vile vile, serikali inabidi iwe na watu wenye ubunifu wa kubadilika kutokana na wakati kwa kubuni mitaala (syllabus) zinayoendana na mahitaji ya ulimwengu wa sasa. Kufundisha kiholela hakusaidii. Lazima malengo ya ukuaji wa nchi yaendane na uwekezaji katika elimu.

  Tuache kuiga wenzetu kwa kila kitu (tuchambue). Tunatakiwa kubuni yanayowezekana kwetu ambayo si lazima yawezekane kwa wengine. Kwa maana yanayowezekana kwa wengine si lazima pia yawezekane kwetu.[/QUOTE]


  Sawa mkuu,
  nakubaliana nawe hasa kwenye ukweli kwamba inabidi tufanye mambo yanayowezekana kwetu hata kama kwa wengine ni magumu. Mfano Waziri anasema sisi ndo tunaongoza East Africa kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wengi(around 50000) hivyo haipaswi kuongezwa, binafsi naona ni tatizo kufanya au kutokufanya jambo flani kwa vile wengine wamefanya au hawajafanya. Ikiwezekana tuanze sisi, dunia nzima ituige
   
 12. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni dhana kuwa Chuo Kikuu ni mahali pa kufundisha wanafunzi tu! Kwa mtaji huu wanafunzi wanaonekana wao ni watu wa kuambiwa, kuelekezwa na kutii. Chuo Kikuu nifaamivyo mimi ni mahali ambapo wale wote walio pale ( wanafunzi, wakufunzi, watafiti n.k.) wanakuwa challenged kufikiri. Mwalimu kazi yake si kumfundisha mwanafunzi bali ni kumuongoza katika kujipatia uelewa zaidi. kipimo cha mwalimu mzuri si kiasi gani mwanafunzi hajui bali ni kiasi gani anajua baada ya kupitia kwake! Kutokana na hili, si sahihi kusema kuwa wanafunzi wataharibiwa na siasa. Wanafunzi wanatakiwa wapewe uhuru wa kuangalia, kuchambua na kukubaliana na siasa ya chama chochote halali. Kuanza kuwawekea mipaka ni kudumaza na kuua udadisi katika wanafunzi. Ni mawazo kama haya ndiyo yanayotufanya tufukuze wanafunzi 2000 waliodiriki kujifikiria bila kuangalia athari zake kwa jamii! Hivi kweli tunaamini kuwa kwa kuwatendea hivi ndiyo tutajenga uzalendo kwao? Mimi naamini ni kuwa tunajenga badala yake wataalamu watakaogopa kufikiria wenyewe. Wataalamu wanaongoja kuongozwa katika kila kitu.

  Amandla......
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Clnde , what you have pointed out are more or less the symptoms of not having a coherent policy in many areas , education included.While your observations are correct the heart of the matter is what the masses desire to attain in the educational ststem.This sounds like an abstract but it will go a long way into solving some of the issues that are arising every now and then, especially in the higher education field.
   
 14. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sawa mkuu,
  Tatizo jingine ninaloliona ni kutaka kufanya vyuo kuwa kama seminari jambo ambalo haliwezekani. Katika jamii ya watu zaidi ya 15000,kutaka wote wawe kama malaika ni kujilisha upepo.when students decide to reason( which of course is an impact of their course work), wanaitwa wahuni. Why do we then lecture them if we dont want rhem to reason? serikali iache kutafute sababu zisizo za msingi, instead,from the base, in primary schools to university level,tufanye mabadiliko yatakayopelekea kuboresha elimu yetu.
   
 15. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Sir/Madam
  its true that masses may desire things of no importance in the national level basing on selfishness ideologies. But can that discourage us from viewing our education system in a more positive sense of improving it? We can, if serious with this business, start by changing peoples's mind especially students and education stakeholders. Thereafter, education offered will be for the national and individual interest. the problem is who cares in the system? Minister? Maghembe?
   
 16. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Na ni lazima wizara ya Elimu ipewe kipaumbele maana inasimama kama msingi kutoa wataalamu watakaosimama katika wizara nyingine
   
 17. S

  SNAKE HOUSE Member

  #17
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vizuri wanafunzi wasome wakijua wanalengo moja tuu...KULITUMIKIA TAIFA KWA UAMINIFU na mengine yatafuta. Bila nafsi za wanafunzi kukomboka tutakuwa tunazalisha wasomi wajinga kuliko walivyokuwa wakati wanaingia vyuoni!..........................
  ............. Hiki Kipande Kimekwenda shule ....... I suggest all the wasomis read,understand,and do something about this..... It is really amusing
   
Loading...