Mfumo wa Elimu Tanzania utakuwaje Juu ya janga hili la Corona au Covid-19

Pure Scientific

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
692
546
Wakuu habari za asubuhi.

Poleni sana na janga ili la Corona linalotusumbua Dunia nzima kwa sasa.

Kilichonileta hapa ni kwamba serikali ilitoa siku 30 kwa Wanafunzi kuwa kuanzia ngazi ya Awali hadi vyuo vikuu ambapo mpaka sasa zimesalia wiki mbili wanafunzi kurudi mashuleni. Nimekuwa nikijiuliza maswali yafuatayo

1. Je, ni kweli Serikali itawaruhusu wanafunzi kurudi ikiwa bado mlipuko wa Corona unaendelea

2. Na kama wataruhusu wanafunzi je wanaweza kujikinga pindi wawapo mashuleni na vyuoni

3. Ikitokea serikali itahitaji kuongeza siku nyingine za likizo hii kama ugonjwa utazidi kuongezeka si inaweza kuathiri mfumo wa elimu kama kwa level ya Advance ambao ilibidi wafanye mtihani mwezi wa tano tena na pia wanafunzi wa ngazi ya vyuo vikuu ambao wengi wao kuanza mitihani ya kumaliza mwezi wa tano na kuendelea

4. Je, na kama Ugonjwa hautaisha kwa kipindi kirefu si inapelekea mfumo wa elimu kwa Mwaka huu kuharibika.


ASANTENI WAKUU NAWASILISHA
 
Hili nalo neno... Kwa upande wangu naona kama hali haitokaa sawa! Tutakua na historia mpya duniani ya kuchupa mwaka wa masomo (yaani mwaka huu utakua hauna pirka za masomo hasa hasa kwa hizi nchi za dunia ya tatu, tusio tumia online platform kwaajili ya kusomea)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Euro 2020 imeahirishwa hadi mwakani.

Hali ikiwa tete sana itabidi waahirishe mwaka mmoja wa masomo kwa kila ngazi/darasa, uhai ndio kitu cha msingi vingine vinafuata.
 
Corona haitoisha.Labda huu ndio uwe mwisho wa kurundika wanafunzi sehemu moja muda mrefu,badala ya kutumia e- learning na muda wa mazoezi kwa vitendo tu ndipo wanafunzi wakutane vyuoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona haitoisha.Labda huu ndio uwe mwisho wa kurundika wanafunzi sehemu moja muda mrefu,badala ya kutumia e- learning na muda wa mazoezi kwa vitendo tu ndipo wanafunzi wakutane vyuoni

Sent using Jamii Forums mobile app
E learning kwa miundombinu yetu bado Kidogo ingawa naona Chuo Kikuu Huria wanajitahidi kwa sasa Walau wananchi ushamba umeanza kuwatoka wameanza kuelewa mfumo huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom