SoC02 Mfumo wa elimu nchini ujikite zaidi kufundisha UKIMWI shuleni

Stories of Change - 2022 Competition

Edjm

New Member
Mar 6, 2017
1
0
MFUMO WA ELIMU NCHINI UJIKITE ZAIDI KUFUNDISHA UKIMWI SHULENI

Na Edson Joel

UGONJWA wa Ukimwi ni miongoni mwa magonjwa hatari na yanayosumbua dunia kwa muda mrefu Sana kutokana na kuhathiri kwa kiwango kikubwa maisha ya watu wengi hususani Vijana hivyo kupelekea wataalam wa afya duniani kuendelea kufanya utafiti wa namna ya kupata Kinga na tiba ya ugongwa huo

Ugonjwa huo wa Ukimwi nchini umekuwa ni changamoto kubwa sana kutoka na kuteketeza nguvu kazi ya Taifa ambayo ni vijana ambao ni kuanzia kati ya umri wa miaka 25 na kuendelea

Kwa mujibu wa takwimu za ugonjwa huo nchini zinaonyesha vijana wa miaka hiyo 25 mpaka 45 ndiyo wameambikizwa virusi vya ukimwi na wapo kwenye hatari ya kuambukizwa virusi hivyo vya ukimwi kwasababu ya wengi wao kutokuwa na Elimu na uelewa mpana kuhusu ugonjwa huo

Kutokana na Ugonjwa huo kuahatarisha maisha watu wengi kwenye jamii Idadi ya mikoa yenye maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi nchini nayo imeongezeka ambapo miongoni mwa mikoa hiyo ni pamoja na Njome, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Tabora, Dare Es Salaam na Shinyanga

Ni ukweli kuwa mfumo wetu wa elimu nchini umekuwa hautilii mkazo kuhusu elimu ya ugonjwa wa Ukimwi ndiyo maana wananchi wengi hususani vijana wameathirik na ugonjwa huo hatari ambao hauna dawa wala tiba

Kwenye mitaala ya Elimu yetu nchini inatambua zaidi masomo mengine lakini elimu ya Ugonjwa wa Ukimwi haijapewa kipaumbele zaidi ambapo ni kipengele kidogo tu kilichowekwa kwenye somo la Biology na sanyansi kuelezea maana ya HIV na Ugonjwa wa Ukimwi, jambo ambalo haliwapi uelewa mpana wanafunzi darasani

Vijana nchini ndiyo wapo kwenye hatari kubwa ya kuambikizwa Ugonjwa huo hatari kwa maana vijana hao wengi wao wapo sekondari na wengine vyuo vikuu, ambao kimsingi ndiyo wanatakiwa kupewe elimu kubwa kutokea hatua za darasa la kwanza kwa maana serikali kuwaandalia mazingira ya kufundikishwa kwa upana madhara ya Ugonjwa huo

Kutokana na mfumo wetu wa elimu kufundisha wanafunzi kuhusu Virusi Ukimwi kama sehemu ya ziada darasa jambo hilo linapelekea vijana kuchukulia ugonjwa huo ni wa kawaida kwao na katika jamii pia, hivyo kushindwa kujali na kuamini sio rahisi kuambukizwa

Mfumo wetu wa elimu nchini ukitambua zaidi na kukazania kufundisha wanafunzi shuleni ikiwa ni pamoja na kuwaonyesha wanafunzi hao namna ambavyo ugonjwa wa ukimwi umeathiri jamii kwa kiwango kikubwa na umeua vijana, wazee, ndugu na jamaa zetu wanafunzi hao wanaweza kutambua na kuwa balozi wazuri kwa vijana wengine wa mtaani

Madhara ya Ugonjwa huo yakitambuliwa angalau kwa asilimia 80 kwa wanafunzi darasani inaweza kupungunza maambuzi ya Ugonjwa huo miongoni mwa vijana ambayo ni nguvu kazi ya Taifa

Katika kuhakikisha maambukizi yanapungua kwenye jamii kama sio kuisha kabisa katika jamii yetu zinatakiwa ziwepo mbinu nyingi za kukabiliana na ugonjwa huu nchini ambapo mbinu hizo zianzie shule ya msingi kwa maana darasa la kwanza, Sekondari na Vyuo vikuu kwani wanafunzi wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa Virusi vya Ukimwi

Takwimu pia zinaonyesha vijana wengine wanaosoma shule na ambao wameishamaliza shule wanapata ugonjwa huo kwa kiwango kikubwa mno hiyo ina maana kwamba vijana hao wanapokuwa shule hawapati elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa wa Ukimwi jambo linalopelekea kufanya ngono zembe na kuchangia vifaa, hivyo kukosa hofu dhidi ya ugonjwa huo

Mfumo wa elimu uanze kutoa elimu kuanzia darasa la kwanza badala ilivyo sasa elimu ya ugonjwa huo kuanza kufundishwa darasa la nne

Kuanza kufundisha madhara yatokanayo na ugonjwa huo kuanza kufundishwa darasa la kwanza ni muhimu Sana kwani mwanafunzi anapoanza shule anaanza kutambua madhara ya ugonjwa huo hivyo mwanafunzi husika kupata uelewa mapema kuhusu ugonjwa huo jambo ambalo litamjengea hofu ya kutoshiriki ngono zembe kwa kuwa wanatambua ngono zembe na namna ya kumhudumia mgonjwa mwenye maambuki ya virusi vya Ukimwi bila kufuata utaratibu wa afya mhusika anaweza kuambizwa

Wataalam wa Afya duniani kila siku wanagundua njia nyingine zinazosababisha maambukizi ya virusi vya Ukimwi ambapo wanadai hata mate ya mdomoni kuna chembe chembe ambazo mwenye ukimwi akipeana denda na ambaye hana ukimwi kuna uwezekano mkubwa naye akapata ukimwi hiyo ina maana kwamba ugonjwa wa Ukimwi una uwanja mpana wa kufundishwa

Ifike hatua mamlaka za elimu nchini zionyeshe kuwa na mifumo thabiti na yenye uwezo wa kuwezesha wanafunzi Shuleni kuanzia darasa la kwanza hadi vyuoni kuwa uelewa mpana juu ya ugonjwa huo na pia mifumo hiyo pia ijikite kuwaza namna ya kuanzisha Somo linalojitegemea darasani tofauti ilivyo sasa somo la Ukimwi kuchanganywa kwenye somo lingine

Somo hilo la Ukimwi likianzishwa kwa maana ya kujitegemea darasani kama ilivyo kwa masomo mengine itasaidia Sana kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo hatari nchini kwa ugonjwa huo utachambuliwa kwa ndani kabisa

Kupitia mfumo huo wa elimu kujikita zaidi kufundisha elimu ya Ukimwi kuanzia shule ya msingi kwa maana darasa la kwanza mpaka chuoni itatoa uwanja mpaka kwa mifumo yetu ya Elimu kufanya tafiti na kujua ni kwa kiwango gani ugonjwa huo umeathiri zaidi wananchi wanaoishi pembezoni mwa mito, bahari, vijijini na maeneo yenye muingiliano mkubwa wa watu

Lakini pia utafiti ukifanyika utakuja na majibu ya namna ya kufanya ili kupunguza maabukizi mapya ya ukimwi ambayo yanaathiri zaidi vijana nchini

Kuna uwezekano mkubwa Serikali imeshindwa kufanya utafiti kwasababu ugonjwa huo unachukuliwa kama wa kawaida katika jamii yetu jambo ambalo ni hatari Sana kwa kizazi kilichopo na kinachokuja

Ni kweli tunaweza kufikri kama taifa kuwa ugonjwa wa Ukimwi ni wa kawaida kuwa tunaweza kuishi nao lakini ikumbukwe kuwa Kila siku idadi kubwa ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kwa vijana yanaongezeka, hivyo nashauri Serikali iwekeze nguvu mpya katika kuboresha mfumo wa elimu nchini ambao utajikita zaidi kufundisha wanafunzi elimu ya Ukimwi shuleni tofauti na ilivyo sasa

MWISHO

rutashobya2014@gmail.com
0714838014
0746196320
 
Back
Top Bottom