Mfumo unatulazimisha kusomesha watoto shule binafsi au ni ujinga tu wa watu wachache kukwamisha shule za Serikali?

pablo5060

Member
Mar 22, 2022
33
50
Najiuliza maswali mengi kuhusu elimu yetu hapa Bongo, ni kwamba system inatulazimisha tusomeshe watoto wetu shule binafsi au ni upuuzi tu wa watu wachache kuna mambo yananishangaza sana kuhusiana na hizi shule za Serikali.

(1) Hivi kama tunalipa tozo kwenye simu hadi umeme serikali inachukua mikopo mbali mbali ni kwanini mpaka leo wanafunzi wanakaa chini wanakosa madawati na hapa nazungumzia baadhi ya shule jijini Dar es Salaam iv huko vijijini hali ipoje?

(2) Ni kwanini wanafunzi wanaosoma shule za serikali wanacheleshwa sana katika somo la kingeleza yani watoto wanaanza kusoma ilo somo darasa la 3 na nakumbuka kipindi mimi nipo shule tulianza mapema sana kupigishwa ngeli, ni kwamba walimu hakuna au?

Nna maswali mengi najiuliza nisaidieni ndugu zangu huenda mimi ndo sielewi mambo yanavyoenda na sipo apa kukosoa utawala
 
Back
Top Bottom