Mfumo unaongelewa sana lakini hulka binafsi ni tatizo pia

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Kuundwa kwa tume kwa ajili ya kufuatilia masuala fulani nyeti, umekuwa ni utaratibu wa miaka mingi hapa Tanzania.

Nakumbuka enzi ya awamu ya kwanza, ziliundwa tume kwa ajili ya kutatua utata kwenye shughuli mbalimbali za wizara. Na awamu zilizofuata mpaka hii ya tano, zimeuendeleza utamaduni huo wa kiutendaji.

Matokeo ya tume mara nyingi huakisi nia za yule aliyeiunda. Kwani anayepewa nafasi ya ukuu wa tume, hutegemea pia kuukuza wasifu wake na wa wenzake na wakati huo huo kuwa amejiwekea mazingira ya kupata neema fulani siku zijazo.

Lakini matokeo mengi ya tume ziundwazo huja na changamoto za kubadilisha mfumo mzima wa utendaji wa kazi ili ufanisi uweze kuonekana.

Matokeo ya tume hizi yameshindwa kuubomoa kabisa urasimu unaosababisha udhaifu ambao ndio chanzo cha kuundwa kwa tume yenyewe katika nafasi ya kwanza.

Wapo wanaosema mfumo mzima uliopo ndio chanzo cha umasikini kuendelea kuwepo. Lakini mfumo ili uweze kufanikiwa inabidi utashi wa watu uwepo kwanza.

Ninaiona awamu ya tano ikitengeneza utamaduni mpya wa uongozi, ambapo tume inayoundwa inaongozwa na msukumo wa rais katika kuwaona wajumbe wa tume wakiongozwa kwanza na uzalendo.

Ninaiona precedent mpya katika awamu ya tano, kwani tume inaundwa sio tu kwa nia ya kupaya majibu ya maswali au sintofahamu, bali wajumbe wa tume wanapewa uwanja mpana wa kuzitumia taaluma zao kwa faida ya leo na kesho ya Tanzania.

Mfumo wa uendeshaji nchi unaweza kuwa umejaa mianya ya udhaifu inayosababisha wapigaji wapige fedha ndefu. Lakini mfumo peke yake pasipo uwepo wa mabadiliko ya mienendo ya watu binafsi, kwa kweli ni kazi bure.

Unapokuwepo uzalendo na utashi wa kuifanya kazi kama inayahusu maisha binafsi ya mtu, hakuna kinachoshindikana chini ya jua.
 
Back
Top Bottom