Mfumo uliotumika kumuondoa Mugabe madarakani ni sawa kuuita ‘coup detact’?

Unaitwa mfumo wa Maamuzi ya pamoja papo kwa papo huo hata ukitumika hapa tanzagiza lazima ukae.
 
huyu bila Shaka ni bavicha maana hata alichokiandika hakifahamu.
Coup de grace ni pigo la mwisho lililositisha hali ilioendelea kuwa mbaya. Palace Coup ni mapinduzi ya jopo la watawala yasiyokuwa na umwagaji damu. Hayo mawili yametokea Zimbabwe sio Coup d'etat.
 
Huu mfumo ndio ule ule uliomtoa Mubarak wa Misri kwenye uongozi - Jeshi lilikua lina mshinikiza kuondoka na kuachia wananchi kuandamana - lakini halikuingia moja kwa moja kumtoa Mubarak mpaka akajiuzulu alipoona hakuna anae msapoti.
 
wataalam wa maswala ya sayansi ya siasa naomba mniweke sawa katika ili, mfumo uliotumika kumuondoa mugabe madarakani kitaalam unaitwaje, mapinduzi ya kijeshi au ni kitu gani.
Panya ama mende anakuuma vidole vyako vya mikononi vyenye shombo huku anakupuliza usi amke
 
..Jeshi la Zimbabwe liliundwa kutokana na wapiganaji wa msituni wa vyama cha Zanu na Zapu.

..lakini Zanu ya Mugabe ndiyo waliotoa idadi kubwa zaidi ya askari waliounda jeshi la Zimbabwe huru.

..Zanu ni chama cha Washona na ndiyo kabila kubwa Zimbabwe. Zapu ni chama cha Wandebele na ni minority Zimbabwe.

..Zanu iliongozwa na Robert Mugabe. Zapu iliongozwa na Joshua Nkomo.

..Zanu na Zapu baada ya uhuru wa Zimbabwe viliungana na kuzaa chama tawala Zanu-PF.
 
huyu bila Shaka ni bavicha maana hata alichokiandika hakifahamu.
wewe unaefahamu mbona umeshindwa kuchangia zaidi ya taarabu tu...acha wenye fani yao watupe shule wewe ulikua unajua kama kuna kitu kinaitwa coup de grace au palace coup.
 
Actually hii ni muungano wa military efforts na political power sababu jeshi halikushika mamlaka bali transition ilifanyika kwa diplomatic approach na reconciliation terms kwamba mugabe hatashitakiwa na usalama wake na family upo guaranteed,

Procedures zilizokua zikiendelea kabla mugabe hajatoa official voluntary resignation ni za kikatiba kabisa hata katiba yetu inaruhusu waziri mkuu na speaker wa bunge wakiona mashaka na nafasi ya Rais wanaweza kuitisha kura bungeni ya kutokua na imani naye judiciary ikihusishwa na kura kutimia Rais anatoka.

A complete coup d'état ni jeshi mwanzo mwisho mkuu wa jeshi ndio anakua kiongozi wa nchi no constitutional procedures sababu hata njia yenyewe sio ya kikatiba.
umeeleweka sn mkuu sio wengine cha kuchangia hana au hajui kabisa ata kinachozungumziwa yeye anatafuta speling mistake.
 
najaribu kufikiria mugabe angekataa kung'atuka nini kingetokea...au ndio kama yaliyomkuta gadafi.
 
urafiki wa awali uliokuwepo kati ya mkuu wa majeshi chiwenga na makamo wa raisi mnangagwa umechangia kwa kiasi kikubwa kutoa kionjo kipya cha transfer ya mamlaka afika na kwengineko duniani. ni mapindizi kweli ila yalipambwa na sifa za kistaarabu au wansema bloodless coup. haikutegemewa jeshi likamate mamalaka halafu kirahisi tu liyasalimu kwa kipngozi wa kiraia. urafiki ulichangia na pengine mugabe hakutanabahi hilo mapema.
 
Hebu jikumbusheni ahadi za Trump wakati ana omba kura kule USA. Tusiwe wasahaulifu hivyo.

Lakini pia kiburi pengine sababu ya umri mkubwa wa Mugabe mwenyewe maana aliyakingia kifua mambo mengi ya hovyo yaliyo fanywa na mkewe Yako mambo ambayo hata mtoto wa chekechea hawezi ya fumbia macho na kujifanya kiziwi.

Lakini Matatizo ya Zimbabwe ya mekuwa yaki waadhiri sana SA ndio maana tunasikia mkuu wa jeshi lao akiwa na mawasiliano ya karibu na Zuma kipindi chote cha tukio zima.

Yote kwa yote jambo kubwa la kujifunza ni kuwa cheo ni dhamana, ukikengeuka ukashindwa kuitunza na kuipa heshima stahiki hiyo dhamana waliokuamini nayo wenzako "uta jiju"
 
Back
Top Bottom