Mfumo shirikishi wa ukusanyaji mapato.

sbikore

JF-Expert Member
Feb 13, 2015
535
191
Kama mjasiliamali mdogo,nimetafakari kwa kina sana juu mwekezaji/mfanyabiashara ndan ya nchi kama mlipa kodi mkubwa na kupata majawabu ifuatavyo:-

Kwa kuwa biashara ni ajira kama ilivyo serikalin,mashirika ya umma na binafsi,makampuni binafsi n.k.ningependa kuishauri serikali kuwatazama watu hawa katika jicho la 3.

Ikumbukwe kwamba uchumi wa taifa hauwezi panda au kushuka kama si juhudi hasi au chanya za watu hawa mhm sana.Kodi hizo ztokazo kwao ndizo hizo baadaya huwarudia watu wa nchin kwa kuwezesha huduma za msingi kabisa za kielimu,kiafya na kimiudombinu.Lakini uwepo wa watu hawa kwa maeneo tofauti wanawezesha huduma za kijamii za kila siku zinazoizunguka jamii nzima ya kitanzania.Kwa hiyo hii ni sekta nyeti mno ambayo bila uwepo wake mambo yote haya yatadorora na hivo wasibezwe.

Licha ya kutafuta mitaji yao kwa mbinu na akili ya ziada pamoja na kuilinda lakin pia wamejitahidi kuwa wazalendo wa kwanza kwa kutoa michango ya kodi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa taifa linajiendesha kwa kuwahudumia watu wote kwa kupitia hizo kodi zao pamoja na kwamba natambua kuwa wapo pia wafanyabiashara ambao c wazalendo,wanakwepa kulipa kodi hizo.

USHAURI.Biashara kama ajira nyingine nchin,ningeiomba serikali kubuni mbinu za kuwawekea akiba watu hawa ili mwisho wa cku anapofilisika au kuacha biashara kwa hiari basi apate motisha yake kama wanavolipwa mafao watumishi wa kada tofautitofauti.Nayasema haya c kwa sababu ya kwakwamisha zoezi la kodi...hapana ni kwa nia njema ya kumlinda mtu huyu awezekuwa endelevu kwa muda mrefu katika shughuli yake lakin pia pale inapotokea mtu kafilisika kwa ghafla pia apate msingi wa kuaanzia kwa kupitia mafao haya.

Si hivyo tu lakin pia hali hii ingeweza kuipunguzia serikali mzigo mkubwa wa kukwepana na walipa kodi maana kila mmoja angeliona ni wajibu halali kabisa na kumfanya atambue kuwa bila kuyatimiza haya atayakosa mafao yake baadaye.

Fursa hii pia ingewawezesha watu wengi kujikita kwenye sekta ya bishara na kulifanya taifa kuwa na mapato makubwa bila kutumia nguvu yoyote ya ukusanyaji,lakin pia ingewezesha watu kuwa wabunifu zaidi kwa kufanya shughuli zenye tija zaidi ili kukutana na fursa hii.

Mkulima angelima kwa tija na kwa juhudi zaidi,mfugaji hivohivo,wimbi la wahuni na wasiotaka kutumika lingepungua na pia nchi ingeenda kupata familia nyingi zenye uchumi imara na mwisho wa cku kuwa na taifa imara lenye watu imara zaidi hata ya sasa.Kazi ya serikali hapa ingekuwa tu ni kumtafutia mwananchi masoko pamoja na wataalam wa kada mbalimbali wa kuwezesha dira kubwa ya mafanikio.

Nimeamua kuleta hoja hii kama chachu baada ya kufanya tafiti kwa kina na kubaini kuwa watu wengi hawalipi kodi mpaka washinikizwe,na kwa kutoa motisha hii kwao basi taifa litaepukana na changamoto hii.

Naomba kuwasilisha na kupokea michango yenu.
 
Back
Top Bottom