Mfumo/sera ya elimu ya sasa ndio chanzo cha tatizo la madarasa na matatizo mengine

Alwatan kamba

Member
Nov 16, 2020
70
236
Sera ya sasa ya elimu na mafunzo inayolenga kutoa elimu ya msingi kwa wote "Universal Primary Education For All" ni sera mbovu inayozalisha matatizo nchini.

Awali, sera ya elimu ililenga kutoa elimu ya msingi kwa kila mtoto kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la saba. Baadae mfumo na sera ya elimu vilibadilishwa ambapo elimu ya msingi kwa sasa ni kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Hivyo ni lazima angalau kila mtoto apate elimu ya kidato cha nne(elimu ya msingi).

Sasa tangu tumeingia kwenye huu mfumo mpya wa kisera ni matatizo matupu yamekuwa yakizalishwa nchini,

1. Kumekuwepo na ongezeko kubwa la kustaajabisha la ufaulu wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza. Ni jambo la kushangaza sababu ni rahisi kumkuta hata mwanafunzi asiyejua kusoma wala kuandika akiwa amejiunga na elimu ya sekondari ya kidato cha kwanza. Swali linakuja, huyu mwanafunzi alifaulu vipi?

2. Mitihani ya upimaji ya darasa la nne, darasa la saba na kidato cha pili haina nguvu tena sababu sera inataka angalau kila mtoto afike kidato cha nne hata kama ni kilaza.

3. Kwa kuwa sera yenyewe ni "twanga pepeta" inadahili kila mwanafunzi kujiunga kidato cha kwanza, imepelekea kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa na majengo kutokana na wingi wa wanafunzi.

4. 'Mori' ya usomaji kwa wanafunzi hasa kwa shule za msingi imepungua sababu hawahofii chochote kwakuwa mitihani ya upimaji na mchujo ipo kama 'geresha' na haina nguvu.

5. Mitihani ya sasa haipimi uelewa wa wanafunzi wala uwezo wao wa kufikiri kwani maswali yote yapo katika mfumo wa machaguzi "MCQ'S" hivyo kazi kubwa ya wanafunzi ni kubashiri na kusiliba majibu kwenye viboma.

6. Udhibiti wa wizi wa mitihani ya darasa la saba umekuwa mdogo kwakuwa ni rahisi mwalimu au mtu yeyote kuiba na kukokotoa maswali ya mtihani kisha kuwapa wanafunzi wakakariri hayo majibu. Mfano, kwenye hesabu ni vigumu mwanafunzi kukariri jibu la kwanza ni 18, la pili ni 3.4, la tatu ni 2¼. Lakini ni rahisi mwanafunzi kukariri majibu hayo in terms of 'herufi' kwakuwa herufi ni rahisi kukaririka kuliko namba.

7. Morali ya ufundishaji kwa walimu imepungua kwa sababu badala ya kuendelea mbele kwa mujibu wa mtaala wa elimu-sekondari na kucover 'syllabus' inamlazimu kurudi nyuma kumfundisha mwanafunzi kujua kusoma na kuandika kitu ambacho alipaswa kujua kabla ya kufika sekondari.

Kutokana na madhaifu ya mfumo huu wa "twanga pepeta" tutarajie nini hapo baadae?

1. Tutarajie kuwa na taifa lenye wasomi vilaza wasio na elimu hapo baadae. Hawa ni jamii ya wasomi ambao watakuwa na vyeti vizuri vya kitaaluma lakini watakuwa na uwezo butu na umahiri hafifu katika fani zao au maeneo yao ya ubobezi.

2. Tutarajie mkwamo wa kiuchumi sababu mfumo utakuwa unazalisha wasomi vilaza wasioweza kulisaidia taifa kwa chochote.

3. Tutarajie kuona tender zote za miradi zikiendelea kushikiliwa na wageni sababu wasomi watakuwa hawana uwezo wa 'practice' umahiri wa taaluma zao kwakuwa ni zao linalotokana na kukariri badala ya kuelewa maarifa.

4. Tutarajie kuona rasrimali za taifa zikiendelea kuvunwa na wageni kwakuwa wasomi wetu watakuwa hawana uwezo wa kuzivuna. Mfano kwenye sekta ya madini, tutakuwa na wataalam wasio kuwa na uwezo wa kufanya utafiti, kuchimba na kuchakata madini, hivyo yataendelea kuvunwa na makampuni ya kigeni.

5. Tutarajie ongezeko kubwa la wasomi wasiokuwa na ubunifu wowote hivyo suala la utegemezi wa ajira serikalini litaendelea kuwa kubwa zaidi ya ilivyo sasa.

6. Tutarajie kujenga vyumba vya madarasa kila mwaka sababu mfumo uliopo unatoa fursa hadi kwa vilaza kuendelea na elimu ya sekondari. Kufuatia misingi hiyo ndio maana kumekuwa na ongezeko kubwa la ufaulu kwa wanafunzi na hivyo uhitaji wa vyumba vya madarasa utaendelea na reaources zingine vitaendelea kuhitajika mwaka hadi mwaka.

Nini kifanyike?

1. Wizara ya elimu irudishe sera/mfumo wa elimu wa zamani ambapo elimu ya msingi inaishia darasa la saba na sio kidato cha nne.

2. Wizara ya elimu irudishe na iweke msisitizo kwenye mitihani ya mwisho ya upimaji. Sambamba na hilo, utaratibu wa awali wa kukariri(kurudia) darasa urejeshwe. Na mwanafunzi atakayeshindwa kukariri darasa zaidi ya mara mbili atolewe kwenye mfumo rasmi wa elimu(formal education) badala yake aendelee na elimu ya kujifunza ujuzi na ustadi katika vyuo vya ufundi(VETA)

3. Wizara ya elimu irudishe sera ya elimu ya kujitegemea ' self reliance education' mashuleni. Elimu hii inasaidia kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujitegemea katika nyanja mbali mbali za uzalishaji mali na ujasiriamali na hivyo kuwafanya wamalizapo masomo wasiwe tegemezi wa ajira serikalini hapo baadae.

4. Mambo yote ya elimu yasiingiliwe na wanasiasa bali yaachwe yafanywe na wataalam. Kitendo chochote cha wanasiasa kujigeuza kuwa ndio wataalam kitaendelea kuharibu ubora wa elimu nchini.
 
Malizia na morali ya kufundisha (kwa walimu hasa wa sekondari inashuka) kwasababu ya aina ya wanafunzi tunaoletewa .. watoto hawajui kusoma wala kuandika physics anaelewaje hapo
 
Sera ya sasa ya elimu na mafunzo inayolenga kutoa elimu ya msingi kwa wote "Universal Primary Education For All" ni sera mbovu inayozalisha matatizo nchini.

Awali, sera ya elimu ililenga kutoa elimu ya msingi kwa kila mtoto kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la saba. Baadae mfumo na sera ya elimu vilibadilishwa ambapo elimu ya msingi kwa sasa ni kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne. Hivyo ni lazima angalau kila mtoto apate elimu ya kidato cha nne(elimu ya msingi).

Sasa tangu tumeingia kwenye huu mfumo mpya wa kisera ni matatizo matupu yamekuwa yakizalishwa nchini,

1. Kumekuwepo na ongezeko kubwa la kustaajabisha la ufaulu wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza. Ni jambo la kushangaza sababu ni rahisi kumkuta hata mwanafunzi asiyejua kusoma wala kuandika akiwa amejiunga na elimu ya sekondari ya kidato cha kwanza. Swali linakuja, huyu mwanafunzi alifaulu vipi?

2. Mitihani ya upimaji ya darasa la nne, darasa la saba na kidato cha pili haina nguvu tena sababu sera inataka angalau kila mtoto afike kidato cha nne hata kama ni kilaza.

3. Kwa kuwa sera yenyewe ni "twanga pepeta" inadahili kila mwanafunzi kujiunga kidato cha kwanza, imepelekea kuwepo kwa uhaba wa vyumba vya madarasa na majengo kutokana na wingi wa wanafunzi.

4. 'Mori' ya usomaji kwa wanafunzi hasa kwa shule za msingi imepungua sababu hawahofii chochote kwakuwa mitihani ya upimaji na mchujo ipo kama 'geresha' na haina nguvu.

5. Mitihani ya sasa haipimi uelewa wa wanafunzi wala uwezo wao wa kufikiri kwani maswali yote yapo katika mfumo wa machaguzi "MCQ'S" hivyo kazi kubwa ya wanafunzi ni kubashiri na kusiliba majibu kwenye viboma.

6. Udhibiti wa wizi wa mitihani ya darasa la saba umekuwa mdogo kwakuwa ni rahisi mwalimu au mtu yeyote kuiba na kukokotoa maswali ya mtihani kisha kuwapa wanafunzi wakakariri hayo majibu. Mfano, kwenye hesabu ni vigumu mwanafunzi kukariri jibu la kwanza ni 18, la pili ni 3.4, la tatu ni 2¼. Lakini ni rahisi mwanafunzi kukariri majibu hayo in terms of 'herufi' kwakuwa herufi ni rahisi kukaririka kuliko namba.

7. Morali ya ufundishaji kwa walimu imepungua kwa sababu badala ya kuendelea mbele kwa mujibu wa mtaala wa elimu-sekondari na kucover 'syllabus' inamlazimu kurudi nyuma kumfundisha mwanafunzi kujua kusoma na kuandika kitu ambacho alipaswa kujua kabla ya kufika sekondari.

Kutokana na madhaifu ya mfumo huu wa "twanga pepeta" tutarajie nini hapo baadae?

1. Tutarajie kuwa na taifa lenye wasomi vilaza wasio na elimu hapo baadae. Hawa ni jamii ya wasomi ambao watakuwa na vyeti vizuri vya kitaaluma lakini watakuwa na uwezo butu na umahiri hafifu katika fani zao au maeneo yao ya ubobezi.

2. Tutarajie mkwamo wa kiuchumi sababu mfumo utakuwa unazalisha wasomi vilaza wasioweza kulisaidia taifa kwa chochote.

3. Tutarajie kuona tender zote za miradi zikiendelea kushikiliwa na wageni sababu wasomi watakuwa hawana uwezo wa 'practice' umahiri wa taaluma zao kwakuwa ni zao linalotokana na kukariri badala ya kuelewa maarifa.

4. Tutarajie kuona rasrimali za taifa zikiendelea kuvunwa na wageni kwakuwa wasomi wetu watakuwa hawana uwezo wa kuzivuna. Mfano kwenye sekta ya madini, tutakuwa na wataalam wasio kuwa na uwezo wa kufanya utafiti, kuchimba na kuchakata madini, hivyo yataendelea kuvunwa na makampuni ya kigeni.

5. Tutarajie ongezeko kubwa la wasomi wasiokuwa na ubunifu wowote hivyo suala la utegemezi wa ajira serikalini litaendelea kuwa kubwa zaidi ya ilivyo sasa.

6. Tutarajie kujenga vyumba vya madarasa kila mwaka sababu mfumo uliopo unatoa fursa hadi kwa vilaza kuendelea na elimu ya sekondari. Kufuatia misingi hiyo ndio maana kumekuwa na ongezeko kubwa la ufaulu kwa wanafunzi na hivyo uhitaji wa vyumba vya madarasa utaendelea na reaources zingine vitaendelea kuhitajika mwaka hadi mwaka.

Nini kifanyike?

1. Wizara ya elimu irudishe sera/mfumo wa elimu wa zamani ambapo elimu ya msingi inaishia darasa la saba na sio kidato cha nne.

2. Wizara ya elimu irudishe na iweke msisitizo kwenye mitihani ya mwisho wa upimaji. Sambamba na hilo, utaratibu wa awali wa kukariri(kurudia) darasa urejeshwe. Na mwanafunzi atakayeshindwa kukariri darasa zaidi ya mara mbili atolewe kwenye mfumo rasmi wa elimu(formal education) badala yake aendelee na elimu ya kujifunza ujuzi na ustadi katika vyuo vya ufundi(VETA)

3. Wizara ya elimu irudishe sera ya elimu ya kujitegemea ' self reliance education' mashuleni. Elimu hii inasaidia kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujitegemea katika nyanja mbali mbali za uzalishaji mali na ujasiriamali na hivyo kuwafanya wamalizapo masomo wasiwe tegemezi wa ajira serikalini hapo baadae.

4. Mambo yote ya elimu yasiingiliwe na wanasiasa bali yaachwe yafanywe na wataalam. Kitendo chochote cha wanasiasa kujigeuza kuwa ndio wataalam kitaendelea kuharibu ubora wa elimu nchini.
Serikali inahitaji mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi, kulipa kodi na kutii watawala tu.

Hayo mengine yanakupa wasiwasi wewe tu.

Kama ni masuala ya utawala, wao wanapita wanawaacha watoto wao.

Angalia Surnames kubwa kubwa kama tatizo la Ajira: Mwinyi, Kikwete, Magufuli, Nnauye, Pinda et al. kama wana tatizo la elimu au ajira ?

Wewe unaambiwa serikali haiwezi kuajiri kila mtu, chukua kitambulisho cha machinga ujiajiri.

Ukizeeka hilo Genge au birika la Gahawa mrithishe mwanao!!!

Kwanza hiyo elimu wao hata watoto wao hawaipitii, so hawahangaiki nayo.
 
Back
Top Bottom