Mfumo na Ubora wa Elimu yetu ndio chanzo cha umasikini

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
892
1,226
MFUMO WETU WA ELIMU NDIO CHANZO CHA UMASIKINI,UCHUMI MBOVU WA RAIA NA NCHI KIUJUMLA.

Swali hili nawajibu wale waliojiuliza kwanini tunatoa elimu za biashara na kijamii mitandaoni??

Tafiti zilizofanywa mwaka 2020 zinaonyesha uchumi wa nchi hautegemei tu jumla ya bidhaa na huduma zinazotolewa kwenye nchi kwa mwaka huo yaani 'Gross Domestic product' bali mfumo wa elimu pia unachangia.Uthibitisho huu unapatikana kwenye nchi zenye mfumo bora zaidi wa elimu duniani kama Finland,Denmark na Korea ya kusini.

Kwahiyo tusipopambana na chanzo cha matatizo yote yaliyotajwa kwenye kichwa cha habari tutakuwa tunaziba matobo tu sio kutibu tatizo.

Wamewezaje kujenga mfumo bora wa elimu??

-Mfumo bora wa masomo kwa Korea wao ni 6-3-3(yaani miaka 6 primary-3 Sekondari-3 Chuo cha taaluma au chuo cha ufundi)
Sisi mfumo wetu wa 7-4-2 ni wakizamani na mbovu kabisa.Na mni mfumo mgumu kuhudumia kwa budget yetu
Mfano kwa Nchi kama Korea Kusini wanfunzi wana term nzima amabapo hawafanyi mtihani wanachagua kitu cha kufanya nje ya elimu ili kutambua vipaji vyao na hii inaongez ubunifu kwa wanafunzi.

-Kwa madarasa ya chini kabisa watoto husomeshwa kwa mfumo wa michezo njia ambayo ni rahisi kushika

-Chakula cha bure mashuleni.

-Vyuo vikuu bure(Kwa Denmark mtu yeyote raua wa bara la ulaya ni bure.

-Walimu bora,Kwa Finland na Denmark wanafunzi bora husomea ualimu na kila mwalimu lazima awe na degree 2.Kwetu ni hadithi aliyepata division 4 ya 30 ndio mwalimu wa kindergarten anayetengeneza mwanafunzi bora wa kesho.Malipo madogo pia yamechangia muitikio usiwe mkubwa na walioitikia hawana ajira.

-Uwekezaji mkubwa katika elimu.Kwenye nchi kama Denmark 8% ya budget yao hupelekwa kwenye sekta ya elimu.

Viashiria vya elimu bora ni vipi?

(1)Uandikishwaji wa shule katika umri mdogo
Katika kitu tunachofeli kwenye shule za umma ni kulazimisha watoto waanze darasa la kwanza wakiwa na miaka 7 bila kuangalia uelewa wa watoto husika.Ni wazi kuna watoto wengi walio na umri chini ya miaka 6 wanauwezo kuliko baadhi ya walio na miaka 7 na kuendelea

Moja kati ya faida za uandikishwaji wa mtoto shule katika umri mdogo ni mtoto anakuwa na tabia njema,Mtoto anakuwa na uelewa mzuri mapema,mapenzi ya kusoma yataanza mapema hivyo kupunguza uwezekano wa kukatisha masomo katikati,Mtoto hujifunza namna ya kujisafisha mwenyewe,Kujengeka kwa utashi wa kuchanganyika na watu na mtoto anajengeka kihisia mapema.Kwa ambao hamjui tabia nyingi za ukubwani ni matokeo ya malezi kabla ya miaka 10.

(2)Uelewa wa mahesabu,kusoma na kuandika na ufaulu wa masomo ya sayansi
Hivi vyote vinahitaji wingi wa walimu na wenye ujuzi mfano kwa nchi kama Finland walimu wote wana Masters Degree,Vifaa vya kusomea kama maabara nzuri na motisha kwa wanaosoma.Vyote hapo juu ni hadithi kwenye nchi zetu

(3)Uwezo wa wahitimu wa Sekondari na Vyuo.
Ukitaka kujua ubora wa elimu angalia aliyeibeba elimu hio.Ni wazi wahitimu wetu wengi wa Sekondari mfano kidato cha 6 hawana ujuzi wa kufanya chochote na elimu zao zaidi ya kufundisha tuition. Kwa wale wa vyuo vikuu wengi wao hawana uwezo wa walivyovisoma kwa vitendo,kiufupi zimejaa theory na nadharia za michoro kichwani tu.

(4)Idadi ya watu wenye elimu.
Idadi ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika kwa Tanzania ni zaidi ya asilimia 4%,waliomaliza shuke ya msingi ni 70%,waliofika sekondari na kumaliza 50% ya wale 70%..Na wenye elimu ya juu 20% tu.Idadi hii ni ndogo ndio maana uchumi wa watu wetu na nchi bado ni wa chini.Kwa maana hii ndio maana tunaanzisha madasa ya mitandaoni kuinua asilimi 30% yenye uwezo wa kufikia mitandao.

ANGALIZO
Tusipobadilisha huu mfumo wa elimu hatutakaa tuondoe umasikini,tatizo la kazi,biashara mbovu na uchumi mbaya.
 
Mkuu you're 100% right.

Natamani wahusika wasome hapa.

Serikali tafadhali badilisheni huu mfumo wa elimu.

Serikali ipo kwa ajili ya wananchi na sio wananchi wapo kwa ajili ya serikali hivyo ni wajibu wenu serikali kusikiliza wananchi.
 
CCM INATENGENEZA WAJINGA NA WAPUMBAVU KWA MASLAHI YAO NA WATOTO WA VIONGOZI WAO KUENDELEA KUTUTAWALA.

Tunamawaziri Mizigo kuntu.

elimu.
elimu.
elimu.
 
Mkuu you're 100% right.

Natamani wahusika wasome hapa.

Serikali tafadhali badilisheni huu mfumo wa elimu.

Serikali ipo kwa ajili ya wananchi na sio wananchi wapo kwa ajili ya serikali hivyo ni wajibu wenu serikali kusikiliza wananchi.
kikwete alipunguza miaka PS iwe sita.Hawa wamerudisha iwe saba.Wanaamini uwingi wa miaka ndio ubora wa elimu.Wing wa masomo ndio ndio ubora wa masomo.Tehama imafundishwa bila vifaa, S/kazi lipo kama maonyesho shuleni.Hakuna walimu wa hizo stadium Ila wanafundisha.Afrika kuna vituko sana huwezi amini mambo yanavyofanyika.
 
Yaani ukiangalia bado tunachangamoto kubwa, kwa sababu hata kwenye hiyo asilimia 20 ya hao waliofika elimu ya juu, bado nao hawakupata elimu bora, yaani wangine wanamaliza chuo kikuu halafu hawaoni cha kufanyia hizo elimu zao.
 
Back
Top Bottom