Mfumo na Taratibu za Kuwawajibisha Mawakili Nchini Tanzania (Mechanisms and Procedures for Disciplining Advocates)

Apr 26, 2022
64
99
Wanasheria au Mawakili hawako juu ya Sheria, bali wanaweza pia kushtakiwa kama mtu mwingine yeyote.

The legal Framework Governing the Conduct of Advocates in Tanzania (Sheria zinazosimamia maadili na mwenendo wa Mawakili Nchini Tanzania)

{i}: The Advocates Act (Sheria ya Mawakili).
{ii} The Advocates (Professional Conduct and Etiquette) Regulations.
{iii} The Advocates (Disciplinary and other Proceedings) Rules.
{iv} The Notaries Public and Commissioner for Oaths Act.
{v} Tanganyika Law Society Act na rules zake (though the rules are not enforceable yet-hazitumiki).

Disciplinary Authorities (vyombo au Mamlaka zinazoweza kuwawajibisha Mawakili)

{i} CHIEF JUSTICE (JAJI MKUU)
Ana Mamlaka ya kumuonya au kumsimamisha Wakili kwa muda fulani au kuamuru jina lake lifutwe kwenye Roll, ikiwa utovu wa nidhamu huo utafanyika mbele yake wakati wa kusikiliza kesi.
Maamuzi ya Jaji Mkuu yanaweza kukatiwa rufaa Mahakama ya Rufani ambayo uamuzi wake utakua wa mwisho. Section 22(1) (2)(a) & (c)(ii) of the Advocates Act.

NB: Ukiondoa Jaji Mkuu, Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani hawana mamlaka hayo. Sheria iko Kimya. Ila Majaji wote wa Mahakama Kuu wanayo Mamlaka hiyo kama tutakavyoona hapo mbeleni.

{ii} HIGH COURT FULL BENCH (JOPO LA MAHAKAMA KUU) - Lina Mamlaka ya kumuonya au kumsimamisha Wakili kwa muda fulani au kuamuru jina lake lifutwe kwenye Roll, ikiwa utovu wa nidhamu huo utafanyika mbele yake wakati wa kusikiliza kesi. Maamuzi ya Jopo hili hukatiwa rufaa kwenye Kamati (ya Maadili) ya Mawakili (Sio Mahakama ya Rufani). Section 22(2)(a) & (c)(i).

{iii} JUDGE OF THE HIGH COURT (JAJI WA MAHAKAMA KUU) - Ana mamlaka ya kumsimamisha Wakili kwa muda, ikiwa utovu wa nidhamu huo utafanyika mbele yake wakati wa kusikiliza kesi, na kisha kulipeleka suala husika kwenye JOPO LA MAHAKAMA Kuu ambayo itathibitisha, kubadilisha au kutengua uamuzi huo. Maamuzi ya Jopo la Mahakama Kuu hukatiwa rufaa kwenye Kamati ya Mawakili.

-Ina maana Jaji akikusimamisha Uwakili, huwezi kukata rufaa moja kwa moja kwenda kwenye Kamati ya Mawakili au popote kabla ya jopo la Mahakama Kuu kuamua. Section 22(2)(b) ya Sheria ya Mawakili.

Zingatia: Majaji wanamwajibisha Wakili kama akionesha utovu wa nidhamu Mahakamani wakati kesi inaendelea. Lakini kama ni huko nje ya Mahakama, mamlaka hayo imeachiwa Kamati ya Mawakili.

{iv} ADVOCATES COMMITTEE (KAMATI YA MAWAKILI). Wengine wanaiita Kamati ya Maadili ya Mawakili.

Zamani Kamati ilikuwa moja tu nchi nzima lakini kufuatia marekebisho ya Sheria ya mwaka 2021, (the Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 3), Act 2021, Act no. 5), Sheria imeanzisha Kamati za Maadili za Mawakili kila Mkoa ili kurahisisha upatikanaji haki na kumwezesha mwananchi anayemlalamikia Wakili kwa ukiukaji wa maadili kushughulikia tatizo lake katika ngazi ya Mkoa badala ya kusafiri kuifuata Kamati ya Maadili katika ngazi ya taifa.

Hivyo kwa sasa tuna.

(a) Kamati ya maadili ya Mawakili katika ngazi ya taifa (National Advocates Committee) na
(b) Kamati za Maadili za Mawakili kwa ngazi za Mikoa.

{a} NATIONAL ADVOCATES (KAMATI YA MAWAKILI NGAZI YA TAIFA): Hiki ndio chombo kikuu cha kuwawajibisha Mawakili nchini Tanzania.

Zamani Kamati hii ilikuwa inapokea na kusikiliza kwa mara ya kwanza malalamiko yote yanayohusu Mawakili kama vile utovu wa nidhamu, uzembe n.k. Lakini sasa mambo hayo yote yanaanzia mikoani. Hivyo, National Advocates Committee inapokea na kusikiliza rufaa zinazotoka huko mikoani lakini pia na zinazotoka Mahakama Kuu. (Haina original jurisdiction)

Maamuzi yake yanakatiwa rufaa Mahakama Kuu ambapo husikilizwa na jopo la Majaji wasiopungua watatu. Rejea section 24A(1) & (4) ya Sheria ya Mawakili.

{b} KAMATI ZA MAADILI ZA MAWAKILI KWA NGAZI YA MIKOA. Imeanzishwa chini ya kifungu cha 4A(1) cha Sheria ya Mawakili, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2021. Maamuzi yake hukatiwa rufaa National Advocates Committee (Kamati ya Mawakili ngazi ya Taifa)

Haina mamlaka kumvua mtu Uwakili. Kama adhabu husika ni kufuta jina la Wakili kwenye orodha ya Mawakili, itabidi wapeleke uamuzi na mapendekezo kwenye Kamati ya Mawakili ngazi ya Taifa (National Advocates Committee). Rejea Section 4B(3) ya Sheria ya Mawakili.

MAWAKILI WA SERIKALI

Kwa upande wa Mawakili wa Serikali, ukitaka kujua maadili yao na vyombo vinavyohusika kuwawajibisha soma sheria zifuatazo (Laws Governing Ethics of State Attorneys and Lawyers in Public Service).

{i} The Office of the Attorney General (Discharge of Duties) Act.
{ii}The Code of Ethics and Professional Conduct for Law Officers, State Attorneys and Legal Officers.
{iii} National Prosecutions Service Act.
{iv} The Attorney General (Discharge of Duties) Guidelines for Practising State Attorneys and Law Officers, 2020.
{v} Public Service Act, CAP 298, R.E 2002
{vi} Public Service Regulations, 2003
{vii} Public Service Disciplinary Code of Good Practice, G.N 53/2007
{viii} Standing Orders for the Public service, 2009 (GN 493/2009.
{ix} Public Leadership Code of Ethics [CAP 398 R.E 2002]
{x} The Code of Ethics and Conduct for the Public Service
{xi} The Advocates Act na regulations zake etc.

------Mwisho-------

Imeandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria (lawyer by profession - 0754575246 WhatsApp).

Natoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili.

Unaruhusiwa kushare lakini usibadili yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.
 
Ndg Zakaria! Naomba kuuliza, je DPP yeye akikosea kwenye kazi zake huwa anawajibishwa au kupewa onyoo na kitengo gani kwenye Mambo ya Sheria!!?
 
Back
Top Bottom