Mfumo mpya wa ajira serikalini: Tutafika??

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
Salaam WanaJambo wenzangu. Habari ya wikendi?? Sasa leo nimepita pale kwenye "www.issamichuzi.blogspot.com" nikakutana na habari hapo chini kuhusu sheria ya ajira ya serikali ya mwaka 2002. Najua ni sheria na imepitishwa na Bunge lakini kwa mawazo yangu machanga naona sheria hii sio muafaka kwa nchi changa (kimaendeleo na sio kiutawala) kama Tanzania. Naomba wenzangu mnipanue mawazo lakini mimi naona yafuatayo yatakuwa ni matatizo yake:
1. Ufanisi wa idara na wizara utakuwa mdogo kutokana na watu kuwa ni walewale - damu mpya yenye fikra mpya

2. Watu ambao wapo nje ya serikali na wao qualified hawataweza kuingia katika nafasi ambazo zinawahusu na badala yake itabidi waingie chini na kupanda ngazi. Serikali sio jeshi na sheria hii itakatisha tamaa wale walio nje ya serikali/nchi kurudi na kujenga taifa lao. Hapa kuna utata ukizingatia kuwa Serikali ya JK inajitahidi ku "support" vita dhidi ya "talent/manpower poaching by the developed world".

3. Hii itasababisha kusiwe na ushindani ndani ya serikali sababu wengi watajua kuwa wao wapo ndani na cheo kikitokea ni chetu - hakuna "external competition". Na hii vilevile inaweza kupelekea baadhi ya maofisa/senior people kuwa "discourage technically" vijana/watu wapya kwenye idara/wizara na hivyo kujihakikishia kuwa "Kingdom come I will be in power and get all comming posts/promotions"

4. Last but not least, nafasi hizi ni za uteuzi. Hapa bwana tutarudisha yaleyale ya kupeana lawama. Wote tunajua kuwa hata uteuzi wa Raisi lazima apelekewe majina, sasa ni criteria gani itatumika kwenye kufanya "vetting" ya candidates? Urafiki/undugu (ambao wote tunajua utachukua nafasi ya juu), ukabila (haupo lakini nadhani tutaurudisha kwa mtaji huu), malipo "in kind" (hii wote tunajua inategemea nani anaweza kutufichia madhambi yetu)??

Kwa maoni yangu hii sheria ni kwa ajili ya kuwalinda/kujilinda wale tulio ndani bila kufukiria wale walio kwenye sekta binafsi na zaidi wale walio nje ya nchi!!! Yeyote aliyefikiria kitu kama hiki na kukataa kuweka "free competition" nadhani hajui kuwa tuendako ni mambo ya ushindani na "uchetu" na sio "umimi" na "usisi"!!!!!

Naomba kuwakilisha...


Mfumo mpya wa ajira serikalini

Na Pascal Mayalla

Serikali haitaajiri watumishi wa umma wa kuanzia ngazi za maofisa waandamizi, bali sasa nafasi za kazi katika ngazi hizo, zitakuwa ni za uteuzi na zitagawiwa kwa watu wenye sifa walio ndani ya utumishi wa umma kinyume na ule utaratibu wa kuzitangaza kwa ushindani wa uwazi kwa kila mtanzania mwenye sifa kuwa na haki ya kuomba.
Uamuzi huo, umetangawa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bibi Hawa Ghasia, katika hafla ya kumuaga Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji msataafu, Lameck Mfalila, makamishina wa tume hiyo na wafanyakazi waliostaafu, iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waziri Ghasia emesema, uamuzi huo wa serikali, unafuatia mabadiliko ya Sheria ya Utumishi Namba 7 ya Mwaka 2002, yaliyofanywa na Bunge hivi katika kipengele cha ajira katika utumishi wa umma kwa ngazi za maofisa waandamizi sasa sio za ushindani wa wazi.
Waziri Ghasia amesema, lengo la mabadiliko hayo ni kuipunguzia serikali mzigo wa kuendesha mafunzo ya mara kwa mara kwa maofisa wanaoajiriwa toka nje ya serikali, na kusisitiza kuwapandisha vyeo maofisa wa serikali wenye sifa na utendaji wao unajulikana kutaleta tija zaidi kuliko kuajiri watanzania wenye sifa ambao utendaji wao haujulikani.
Hata hivyo Waziri Ghasia amesema uamuzi huo hauna maana kuwa watanzania wenye sifa walio nje ya serikali sasa hawana nafasi tena katika uongozi wa utumishi wa umma, ila bado watanzania wenye sifa wataendelea kuajira katika utumishi wa umma pale ambapo hakutakuwa na watumishi wa umma wenye sifa zinazotakiwa.
Naye Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bibi Thecla Shangali, amewasisitizia watumishi wa umma kuzingatia taratibu sheria na kanuni katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili utendaji wa serikali upate mafanikio yaliyokusudiwa na kuleta tija kwa maendeleo ya taifa.
Mwenyekiti mstaafu wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, Lameck Mfalila, amesema anajivunia sifa ya kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa tume hiyo iliyoundwa mwaka 2002 na mafanikio makubwa ya tume hiyo iliyoyapata katika kipindi kifupi ambapo ni pamoja na kubadilisha sura na mitazamo ya watumishi wa umma toka utumishi wa zamani ambao ni utumishii tuu mpaka sasa kwenye utumishi wa umma unazingatia matokeo huku ukifanya kazi kibiashara kwa kufuata kanuni za mikataba ya huduma kwa wateja.
Jumla ya makamishna watano wa tume hiyo ewamestaafu na mwenyekiti wao sambamba na wafanyakazi 3 wa tume hiyo akiwemo, Naibu Katibu wa tume hiyo, Bibi Prisilla Ole Kambainei.

Mwisho wa kunukuu
 
Morani,

Umeuliza Tutafika?..........jibu ni kuwa HATUTAFIKA............period!

1. Aliyepeleka hilo wazo atakuwa ana mamtatizo ya akili na ni wale ambao tunawaita average or belo average person ktk perfomance iwe kazini hata shuleni/vyuoni...trust me

2.Walioandaa muswada niwatu wa kuogopwa kama UKOMA kwani ndio mafisadi/walaji rushwa wenyewe katika milango ya ajira

3. Waliopitisha mswada..............sina hata la kusema maana hao wanajulikana ni rubber stamp

Please please Waziri...............kama tumefikia kiwango cha kuwa wavivu ktk ku-review CV za watu......................then mnatupa picha kuwa hao hao mnaotaka wachukue vyeo in future hawataweza ku-review miktaba mbali mbali ya serikali............kwa sababu wamepanda cheo kwa kuwa yeye ni senior na sio utendaji!!!!

Yaani sijapata ku-feel kwamba kuna watu wana mawazo duni kiasi hichi

JK............sina hakika kwamba umeshaweka sahihi yako ktk hili au bado.................kama bado nakushauri usiidhinishe upuuzi huo. kama tume ya utumishi imeshindwa ku-review CV na ku-interview watu competetively.............................then pangua hiyo tume weka watu wenye uwezo wa kufanya kazi...........

Waziri anasema eti ni kwa jili yakupunguza gharama za mafunzo!!!!!!!!!!!!.............what a crap!!.............yaani career development ya mtu ni gharama kuliko hizo hasara wanazotuingiza ktk mikataba feki!!!

Mh Ghasia..............Hivi unajua kuwa ukimpa nafasi mtu/watu ambao ni dumb........huyo/hao ma-dumb ndio watakuwepo kwenye kamati mbali mbali za maamuzi makuu ya serikali................what do you expect then..................bunch of IPTLs ofcourse

nimesoma na kufundisha watu very senior serikalini....................yaani kuna wakti mpaka nikawa najiuliza hivi hawa walifikaje fikaje ktk zile kozi..........and i was wondering ni kitu gani watapeleka huko makazini................

anyway just ushauri kwa JK.......................DO NOT ENDORSE hiyo kitu
 
Inanibidi kwanza nifanyie utafiti. Give me few days Then I will comment. Ingawa ninavyojua sasa Upendeleo ndiyo njenje, Rushwa na uzembe uatongezeka sana. ujipendekeze upande cheo. Ila uchambuzi yakinifu nipeni siku tatu niingie msituni kwanza. Maana hizo ndizo anga zangu!!
 
Kwa mtaji huu, suala la manpower kuhama litaongezeka badala ya kupungua. Haingii akilini, watu wa serikalini kufikiria namna hii. Ukombozi wa Mtanzania kufikia maisha bora itaendelea kuwa simulizi za Alinacha.
 
Mugo

hilo jambo linasikitisha sana.....................na hasa ukizingatia hivi sasa vigogo wanafanya kila namna kuwaingiza watoto wao both in Siasa na ktk System pia............ sisemi kuwa vijana wao hawafai no............isipokuwa the move behind ndio inatisha.........na hasa ukiangalia nafasi ya mwananchi wa kawaida
 
Waziri Ghasia amesema, lengo la mabadiliko hayo ni kuipunguzia serikali mzigo wa kuendesha mafunzo ya mara kwa mara kwa maofisa wanaoajiriwa toka nje ya serikali, na kusisitiza kuwapandisha vyeo maofisa wa serikali wenye sifa na utendaji wao unajulikana kutaleta tija zaidi kuliko kuajiri watanzania wenye sifa ambao utendaji wao haujulikani.
Hata hivyo Waziri Ghasia amesema uamuzi huo hauna maana kuwa watanzania wenye sifa walio nje ya serikali sasa hawana nafasi tena katika uongozi wa utumishi wa umma, ila bado watanzania wenye sifa wataendelea kuajira katika utumishi wa umma pale ambapo hakutakuwa na watumishi wa umma wenye sifa zinazotakiwa.

Yaani pamoja na kutaabika kwangu kote kujisomea ili niitumikie sirikali naona sasa nachinjiwa baharini. Sijauelewa vyema huu uamuzi wa Hawa Ghasia na wenzake wa utumishi wa umma, sijajua mantiki hasa ya kufanya maamuzi haya ambayo kwa maoni yangu naona ni maamuzi ya ajabu kupita maelezo.

HOJA
1. Napinga suala la serikali kujitetea kwamba wanaepuka gharama za "On job training", hizi haziepukiki kabisa. Teknolojia mpya za utendaji kazi huwa zinabadilika kila leo, kwa hiyo mafunzo kazini hayakwepeki. Madhara ya kutowapa elimu mpya hao watumishi wa zamani ni makubwa sana kuliko hizo gharama wanazojifanya wanaziepuka, na hapo ndipo tunapoangamiza kabisa na zile juhudi kidogo tulizozionyesha katika utumishi wa umma. Wanataka turudi kwenye kuhifadhi mafaili "Manually", badala ya kutumia nyenzo? Mfano, mwishoni mwa miaka ya tisini, wengi tulitumia programu za kompyuta za "Windows 9x, yaani 95 na 98. Kuanzia mwaka 2000 kumekuja Windows mpya zikiwa na mambo mengi mapya. Windows hizi ni Millennium Edition (ME), 2000, XP, Media Cente Edition, Server na sasa vista. Sasa kama uliajiri watu wa kutumia windows 95 miaka hiyo, lazima watu hawa wapate elimu ya kutumia programu hizi mpya, ama uamue kubaki na teknolojia ya zamani na kupunguza ufanisi. Mpaka hapa lazima utafute mtu wa kuwapa elimu mpya hawa watumishi. Huu uhafidhina naona umefikia mahali pabaya sana. Huo ni mfano mmoja tu. Najua kwa watawala, mbinu za kiutawala hubadilika kuendana na mazingira na wakati, kwa hiyo kutokubali kubadilika ina manaa tunarudisha maendeleo nyuma.

2.Kasema kuwa wataajiri watendaji pale tu ambapo kutakuwa hakuna kabisa watumishi wa nafasi husika waliopo kazini kwa wakati huo. Sawa! Je hawa hawatapatiwa mafunzo ya utendaji? Sasa hapa unaepuka nini na unakwepa nini?

3. Kuna hizi tuhuma hapa Jf kwamba watoto wa vigogo wamejazana kule kunako pesa za sie walipa kodi. Ina maana kama hakuna mtu wa kuingia kutoka nje ya hao waliopo basi sisi wenye hizo pesa tunakosa imani na waliopo, hili nalo litafanya hata kile kidogo tulichohifadhi kitokomee kabisa. Nina wasiwasi na hili, labda nipatiwe ufafanuzi. Nina hofu na hizi ajira za vimemo.

4. Hoja nyingine ya Mheshimiwa Ghasia ni kwamba wanakwepa kuajiri watu ambao utendaji wao haujulikani. hili nalo mimi nalipinga kabisa. Sirikali haina uwezo wa kumjua kila mtu na utendaji wake, sawa, lakini kuna watu ambao wako nje ya utumishi wa umma na wanafahamika kuwa ni watendaji kazi bora sana. Mfano, kuna Dr Kimei wa CRDB ambaye utendaji wake unaonekana, kwamba benki anayoiongoza inazalisha faida na wanahisa wanapa gawio, tofauti na TOL. Sasa huyu naye watasema utendaji wake haufahamiki? Kuna wahandisi, mameneja, watawala na watafiti kibao sana wanaotumika nje ya utumushi wa umma na wanafahamika kwa utendaji wao, sasa kwa nini watiliwe shaka? Hali kadhalika kuna kipindi cha maangalizi (probation), mtu anapoanza kazi, kama utenaji wake hauridhishi basi anabadilishwa. Napinga kabisa kitendo cha sirikali kuogopa kuajiri watu eti kwa sababu utendaji wao haufahamiki. Huku ni kutokubali changamoto. Ingekuwa ni mtihani kwa Ghasia na wenzake ningewapa alama "G" kabisa, kwa sababu wamepitiliza kiwango cha mwisho cha kufelia ambacho ni daraja "F".
Huo ndio mtazamo wangu
Naomba kuwasilisha!
 
MI nadhani kuna haja kabisa ya kuzuia move hii ambayo mi naiona imelenga katika ubaguzi kinyume na katiba ya nchi inayokataza ubaguzi wa aina yeyote.

Kama suala la mafisadi lilivovaliwa njuga, ningependa kuona na hili wanaharakati wanaliona na wanalivalia njuga vile vile kwa sababu kama tukiliruhusu basi tujue ndo ivo mfumo wa ajira umeshatekwa na wachache!
 
Wanaforum kweli hili ni jambo la kutisha! Siamnini wenye kuleta hilo wanazo za kuwatosha! Hivi wale walio nje ya public service wanachukiliwaje? Sio watz? Hawana haki ya kulitumikia taifa lao katika ofisi za uma? Ati mimi nikiwa "energy expert" na nina miongo kadhaa kazini katika private sector, nikitaka kufanya kazi wizara ya nishati, nitatakiwa kuanza kama trainee? Sielewi kabisa! Waziri Ghasia mbona unazungumzia ghasia bila kufikiri mama?! Kazi za umma ni haki ya kila mtz, zitangazwe na mwenye sifa aombe.
 
Hii ni ubaguzi na ni kinyume cha katiba na haki za binadamu. Hatuna wanasheria JF watupe mwanga? Sera kama hizi inabidi ziwe challenged mahakamani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom