Mfumo gani huu mfumo wa shetani kuchukua mali za masikini kugawa kwa matajiri

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,681
1,109
Nchi yetu ya Tanzania ina hitaji mabadiliko makubwa ya kiuongozi ili kuweza kuleta maendeleo na maisha bora kwa kila Mtanzania.Nchi hii imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu mbalimbali ambazo zimeshindwa kuleta tija katika kusukuma gurumu la maendeleo lisonge mbele.

Mabadiliko ya kiuongozi ndiyo pekee yatakayo weza kubadilisha mfumo uliopo ambao umekuwa unanyang'anya mali za masikini wa Tanzania na kuzigawa kwa matajiri(wawekezaji).

Mfumo huu uliopo Mwalimu JK Nyerere aliukemea na kuuita mfumo wa shetani,badala ya kutumia resources zetu to the maximum sisi tunazigawa kwa matajiri kwa kigezo cha kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji.

Hali hii imekuwa ikiwa nogesha wageni hawa na kuwa kimbilio lao kwa kuwa tu nchi imegeuzwa shamba la bibi,matokeo yake wamekuwa wakikwepa kodi kwa kubadilisha majina ya kampuni zao na kujifanya wawekezaji wapya ili waweze kupata msamaha wa kodi kwa kigezo cha uwekezaji mpya ndani ya nchi.

Kama nchi ikiwa na mfumo wa kishetani basi hata viongozi wake watakuwa wanaongoza kwa utashi wa kishetani bila kujali,umoja wa kweli ni nguvu ya Mungu.Mwalimu alikemea sana hali hii lakini leo ana bezwa kwa viongozi kushindwa kuyasimamia yale yote aliyoyaamini yanaweza kujenga taifa lililo bora na lenye maadili mema kwa viongozi wa umma na wananchi wake,huku wakijinasibu wana muenzi Mwalimu ilihali wanampinga kivitendo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom