Mfumo bora wa utawala kwetu barani Afrika ni upi?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,305
45,607
Mfumo gani wa utawala ungefaa zaidi kuondoa umaskini, kuleta maendeleo makubwa,utangamani,haki na furaha kwa bara la Afrika ? Je ni.

1. Demokrasia

2.Ufalme kamili

3.Udikteta mwema/benevolent
 
Haya Mambo ya Mfumo hayatabiriki kwa nchi zet za kiafrica.
Mfano Mfumo wa demokrasia ndio tumeushindwa kabisa. Naamini huu ndio unaweza kuwa mfumo ambao ni source ya Machafuko ya nchi zetu za kiafrika.

Kikubwa ni kupata Viongozi bora katika mfumo wowote kati hapo.
 
Misingi ya utawala bora huletwa na Ushirikishwaji, Maridhiano, mwitikio, matokeo bora na ufanisi, uwajibikaji, uwazi, utawala wa sheria, maono ya kimkakati pamoja na uadilifu.

Na viongozi ni lazima wazingatie:

Matumizi sahihi ya dola.

Matumizi mazuri ya madaraka yao.

Kujua na kutambua madaraka waliyonayo na matumizi yake.

Madaraka yatumike kulingana na mipango iliyowekwa na katiba na sheria.
 
Decentralization Wananchi wapate nguvu ya kujiamulia mambo yao Raisi awe wa ceremonial tu nguvu apunguziwe
 
Wazungu wanaamini Afrika ni bara special kwa ajili ya kuishi machizi yeah i mean mimi na wewe tumo.Unawapelekea visu vya kumenyea vitunguu na nyanya wao wanavitumia kuuana so hakuna formula sahihi ya kuitawala Afrika TRUST ME
 
Mfumo gani wa utawala ungefaa zaidi kuondoa umaskini, kuleta maendeleo makubwa,utangamani,haki na furaha kwa bara la Afrika ? Je ni.

1. Demokrasia

2.Ufalme kamili

3.Udikteta mwema/benevolent
Namba 3 nafikiri inafaa...tungekuwa na madictator wenye mapenz na nchi kam Gaddafi alivyokuwa libya, alikuwa dictator ila inchi ilipata karibu kila kitu
 
Demokrasia na mfumo wa katiba sio asili yetu tumerithishwa tu kwa waafrika almost kila tunachopractice kwa sasa tumerithishwa na wazungu.

Kabla ya kuja wakoloni tulikuwa na aina za utawala na pia namna ya kuabudu.

Wazungu wao wamebakia na aina zao za kujitawala ndio maana hawapati tabu kuiendesha.

Uk Wana Malkia/Mfalme lakini Wana waziri mkuu na nchi haina katiba ya kuandikwa( written constitution).

Ujerumani Chancellor.

Sijui nini kilitupata ila tumeacha kila kitu chetu na kukumbatia vya wageni.

Kuna haja ya kuhakikisha kuwa tamaduni zetu zinakuwa properly documented.

Ama la tamaduni za Mwafrika zitapotea kabisa.
 
Back
Top Bottom