Mfumko wa bei umo ndani ya mafuta ya vyombo vya moto (petroli na dizeli), kwenye umeme, na kwenye gesi ya kupikia

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,315
8,214
Mfumko wa bei umo ndani ya mafuta ya vyombo vya moto (petroli na dizeli), kwenye umeme, na kwenye gesi ya kupikia.

Ukitaka kucontrol mfumko wa bei inatakiwa ucheze na bei za mafuta, gesi ya kupikia na umeme ndani ya nchi.

Pia kutokana teknolojia kukua, mfumko wa bei umo hadi kwenye huduma za mitandao ya simu (huduma za kutuma na kupokea pesa, pamoja huduma za vifurushi vya internet, na kupiga na kupokea simu)

Siku hizi ili bidhaa imfikie mtumiaji wa mwisho, inategemea huduma za mawasiliano pia. Huduma za mawasiliano zinahitaji gharama zitumike. Hizo gharama zilizotumika zikingizwa kwenye bei ya mwisho ya bidhaa lazima bei ipande.

Hapa, bidhaa ili ingie sokoni inategemea usafiri, usafiri unategemea mafuta, mafuta nakipanda bei, na gharama za kusafirisha bidhaa zinaongezeka. Gharama za kusafirisha zikiongezeka bei ya kuuzia lazima iongezwe, ili muuzaji aweze kupata faida.

Bei ya gesi ya kupikia inacontrol bei za vyakula migahawani, mahotelini na bidhaa zote za kupikwa zinazouzwa madukani. Lakini pia kuna viwanda, vinatumia gesi kuzalishia bidhaa, kama vinanunua gesi kwa bei kubwa lazima navyo viuze bidhaa kwa bei kubwa.

Vivyo hivyo na kwenye umeme.

Bei ya mafuta inachangiwa na vitu vifuatavyo.
1. Kuongezeka kwa bei katika soko la dunia kuliko tokana na vita.
2.kuingizwa kwa ushuru, tozo, na kodi mbalimbali.

Ili kupunguza bei ya mafuta serikali ifanye yafuatayo:

Serikali haina uwezo wa kucontrol namba moja. Ila inauwezo wa kucontrol namba 2.

Katika kipindi hichi cha dharura, ipunguze kodi, ushuru na tozo ilizoweka kwenye mafuta ili yaweze kupungua bei. Kama haina uwezo huo basi itoe ruzuku kwenye makampuni ya mafuta ili yauze mafuta kwa bei ndogo.

Hapo ndipo itaweza kupunguza gharama za maisha na kupunguza mfumko wa bei nchini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom