Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,150
1,713
Naomba ufafanuzi wa hii skendo kwa wale waijuao. Je hii ni dalili ya nguvu mpya dhidi ya ujambazi au over confidence ya ma afande imezua soo!??

-------------------------------------------------------

Afande Zombe aunganishwa kwenye tela

Hatimaye aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Dar, Abdallah Zombe ameunganishwa katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini waliokamatwa maeneo ya Sinza jijini.

Afande Zombe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu akituhumiwa kwa mauaji ya watu wannne; Ephraim Sabinus Chigumbi, Sabinus Chigumbi Jongo, Juma Ngugu na Mathias Lunkombe.

Zombe hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo na alirejeshwa kule alikozoea kuwasweka wahalifu mbalimbali katika gereza la Ukonga kuunganishwa na watuhumiwa wengine wa mauaji hayo.

Wengine walioko sero na wanaoshtakiwa kwa kosa hilo hilo ni maaskari Polisi; Christopher Bageni, Ahmad Makelle, Noel, Jane Andrew, Nyangelera, Emmanuel Mabula, Felix Sandys Cedrick, Michale, Abeneth, Rashid Mahmoud Lema na Rajabu Hamisi Bakari.

Wengine wanaoendelea kusakwa na jeshi hilo ni CPL Saada Allawi, PC Frank, SSGT James na CPL Festus.

Tukio hilo liliibuka Januari 14 mwaka huu baada ya kutokea tukio la ujambazi maeneo ya Kariakoo na jeshi la polisi likiongozwa na Afande Zombe lilikurupuka na kuwakamata wafanyabiashara hao katika maeneo ya Sinza na kupotea nao.

Taarifa za polisi zilizotolewa jioni ya siku hiyo hiyo zilitonya kuwa watu hao walikuwa majambazi na wameuawa katika mpambano mkali wa kurushiana risasi.

Awali Afande Zombe alishikilia msimamo wake kuwa watu hao walikuwa majambazi pamoja na kuwepo na ushahidi wa watu kibao waliokuwa wanawafahamu marehemu na alikuwa amefungua kesi mahakamani kuvishtaki baadhi ya vyombo vya habari kwa kumpakazia na kumkashifu.


Kesi hiyo itasikilizwa tena June 16 mwaka huu.
 
  • Thanks
Reactions: jme
Masikini ya Mungu, balaa lote la majambazi wamesukumiziwa hawa wanyonge, na wakati tunasikia kuwa majambazi walikuwa wakipewa silaha na info zote na wakubwa zaidi wa polisi na serikali!
 
Ni kweli Mzee Es, to me kina Zombe ni tip ya iceberg, uozo bado upo mwingi. Ila kwa huu mwendo wa kuwapa muda watendaji wajirekebishe wengi watapona, though it will send a wrong signal to the mass
 
Habari hii inatoka gazeti la Mwananchi la leo lakini iko shallow kidogo, kama kuna wana JF wanaofahamu tunaomba mtufunulie zaidi, isije kuwa bado tuna kina Zombe wengine.

*Mwapachu asema kazi amemaliza
*Jalada lapelekwa Ikulu


Na Ramadhan Semtawa


SAKATA la mauaji yenye utata ya vijana wawili wa Dar es Salaam, Hija Shaha Salehe na Mine Chomba, limeingia katika hatua mpya baada ya ripoti ya uchunguzi ya vifo hivyo, kupelekwa Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete...
 
Gari la Hija analo kamishna wa Kanda Maalumu, ya Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana, ambaye ndiye kigogo wa polisi anayetajwa kuwamo kazini wa zamani ni yule yule Abdalah Zombe, ambaye anaelezwa alihusika moja kwa moja na mauaji ya Hija Shaha Salehe na Mine Chomba.
 
Thanks Halisi
Lord have mercy. Sasa ni kwanini watanzania hawa waliuawa? au ndio yanafanana na yale ya watu wa Moro wauza madini?
 
  • Thanks
Reactions: cmp
Gari la Hija analo KAmishna wa Kanda Maalumu, ya Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana, ambaye ndiye kigogo wa polisi anayetajwa kuwamo kazini.. Wa zamani ni yule yule Abdalah Zombe, ambaye anaelezwa alihusika moja kwa moja na mauaji ya Hija Shaha Salehe na Mine Chomba.

halisi kwanini Alfred ana gari hilo? je halikupelekwa polisi pale central kama mengine yanavyopelekwa na kukaa pale ? yeye alfred ametumia sheria gani mpaka kuchukua gari hili vijana hawa wamefanya jitada gani za kuweza kuwasilina na vyombo vya sheria ili kuweza kungamuliwa suala lao ?
 
Yanafanana kabisa na watu wa Moro, japo wote waliouwawa wanaelezwa pia kuwa si watu waaminifu, na kwamba kuuwawa kwa kulitokana na kutoelewana na hao Vigogo wa ;polisi.. lakini wanasema Hija aliacha kabisa wizi na kuanza kuwa mfanyabiashara mwaminifu na alikua anaishi nje ya nchi.

Gari la HIJA analo Tibaigana na anadai kwamba alilinunua kihalali baada ya Hija kuuwawa, lakini amesahau kesi ilikua haijaisga un anuaje gari?...SHAME
 
Kwa hiyo it is very possible that we have another known criminal in our police force. Inasikitisha sana kama yeye mwenyewe alikiri kununua gari hilo. Lakini iwe ni baada au hata kabla ya kuuawa still inatia shaka, aibu na kuibua maswali mengi!
 
Maelezo ya polisi yaliyotolewa wakati huo yalionekana kupingana na picha, kwani yanaeleza Hija aliuawa na wananchi wenye hasira kali, lakini picha za awali kabla ya kifo ambazo gazeti hili inazo, zinaonyesha alikuwa mzima asiye na jereha huku akiwa chini ya ulinzi katika gari aina ya Landrover.

Awali ipi tena? Hapa na mimi wananichanganya sasa. Maana mimi nimeona picha zilizochapishwa kwenye gazeti (I Believe it was Mfanyakazi), na mpiga picha aliweza kuonyesha jamaa alivyokuwa ameshikwa na wananchi, then picha ingine, ameanza kupigwa na damu kumtoka, na nyingine alipokuwa amekata roho! Sasa hili gazeti lina picha gani za awali?

Utata huo upo pia katika kifo cha Mine, ambaye baada ya kudaiwa kuawa na majambazi katika baa hiyo ya Meeda, baadhi ya maafisa wa polisi, wanadaiwa walikwenda nyumbani kwa marehemu Mwenge na kuchukua baadhi ya magari wakimtaja kwamba alikuwa ni mwizi wa magari.

Hii ya Mine hata mimi nimeisikia sana , maana kuna habari nyingi sana zinazongumzwa kuhusiana na kifo chake.

Kumbukumbu tu, wakati huu ndio ile sheria, sijui amri ya "Shoot to Kill" ilikuwa imepitishwa, wengine waliuawa kwa mgongo wa amri hii, ingawa majina ya hawa nasikia yalikuwa miongoni mwa ile list ya majambazi?!? Interesting!
 
Kwa police kununua gari la victim in a standing homicide case is more than a coincedence......scary!!!
 
Tetesi nyingi hata kabla ya mauti zililenga kwamba Hija alikuwa ni jambazi kweli kweli, mtumia mguu wa kuku.
Alishawahi kutiwa nguvuni na Polisi mara kadhaa kuhusiana na wizi wa magari na mara moja kwa tuhuma za kuuwa na kuiba gari la mzungu.

Mara zote alitolewa nje katika mazingira ya Kibongo si wote mnajua. Who is your Daddy?

Sasa kwa vile baba yake Hija yuko karibu na system amesukuma mambo mpaka yamefikia hapo yalipo fikia.

Kwamba Hija alikuwa Jambazi hizo ni tetesi za muda mrefu hata kabla mauti ya kuangukiwa na ukuta hayajamfikia.
 
SAKATA la mauaji yenye utata ya vijana wawili wa Dar es Salaam, Hija Shaha Salehe na Mine Chomba, limeingia katika hatua mpya baada ya ripoti ya uchunguzi ya vifo hivyo, kupelekwa Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete...

Kama maafisa wa juu wa jeshi wanahusika ni mpaka rais atoe amri ili wapelekwe mahakamani? Kwanini wasipelekwe mahakamani kama mtuhumiwa mwingine yeyote bila idhini ya rais? what if these people are his (president) people?

Rais anataka kutoa maamuzi kwenye kila kitu na mambo ya kienda mrama tukilaumu tunaambiwa "oh he can't do it by himself."

Rais inabidi apunguziwe madaraka kidogo, he is too powerful.
 
Taratibu..............

Ni kuwa Mine aliuwawa na Hija, hiyo inasemekana Hija alitumwa na Zombe, sasa ktk kupoteza ushahidi ilibidi Hija naye auwawe. Mine alikuwa na connection na IGP wa wakati huo.

Alikuwa anazo hela. Hija na Mine walikuwa majambazi sugu. Hilo halikuwa siri. Hija alikuwa na backup ya baba yake, mzee alijitahidi sana na alikuwa anasikitishwa na vitendo vya mtoto wake.

Kwa kifupi kama waliuwawa kwa vyovyote ilikuwa sahihi jamaa walikuw hatari sana.

Hija aliposhikwa na polisi Kimara aliwekwa kwenye Landrover. wananchi wakapiga kelele, polisi wakasema kwani hamuwezi kumchukua/ huyo hapo, ndipo wakaanza kumpa kisago ilipangwa ndio maana kuna pich za hatua kwa hatua toka anapigwa mpaka ana kufa, na kabla ya kifo alikiri kumuua Mine.

FD
 
Kama maafisa wa juu wa jeshi wanahusika ni mpaka rais atoe amri ili wapelekwe mahakamani? Kwanini wasipelekwe mahakamani kama mtuhumiwa mwingine yeyote bila idhini ya rais? what if these people are his (president) people? ....

Siyo apunguziwe kidogo sana tu! Angalia hata mambo ya ANBEM, PCCB wanadai raisi kaisha sema no, ndo imetoka.. hivi kweli hiyo ni haki??
 
hii habari inautata mwingi sana,lakini sijui ukweli uko wapi.ila nachoweza kusema mine alikuwa na uhusiano na viongozi wengi wa juu wa jeshi la polisi,kwa IGP hilo sina uwakika ila DCI hilo ninauwakika nalo.pia msisahau alikuwa pia na urafiki wa karibu na muungwana,

kama vijana wengine wa mjini walivyokuwa.vile vile rafiki zake wakubwa ni wale SABA wanaoshughulika na spear parts. Mine ndie alikuwa anashughulikia kutoa mizigo yao bandarini,sijui kwa undani walikuwa vipi. Sasa sijui huwenda hapa kunashinikizo la hawa wakubwa kutaka kujua kiini cha vifo vyao.

Hija nilimjua kama dalali wa magari tu yeye ni kundi la kina moshi majungu na wengineo w dizaini hiyo.kama kuna nyeti basi asisite kuzi mwaga hapa
 
Hivi hii nchi hakuna utaratibu wa kudeal na mambo kama haya mpaka raisi apelekewe?

polisi,mahakama,prosecutors,lawyers nafikiri ndio wa kudeal na issue kama hizi...ukiona mambo kama hayo kupelekewa raisi ni ubababishaji tuu na dalili za mfumo uliooza au udikteta,mfumo wa sheria ufanye kazi sio huu upuuzi wa kumpelekea raisi issue kama hii na hao vijana waliouwawa nasikia waliua watu wengi sana na kuiba mali za watu.

sometimes thats what you get ukiwa criminal na polisi nao wanachoka kudeal na wewe kisheria maana wanajua wewe ni muuaji na jambazi ila wanashindwa kukuconvict in the court of law sababu may be of corruption or insuffienct evidence basi wanakutafutia shortcut tuu ili usiendelee kusumbua ingawaje its illegal ni risk ya polisi maana nao wanaweza kuhukumiwa wakijulikana na sio kitu kigeni sometimes LAPD na NYPD ndivyo wanavyodeal na drug dealers & murderers na polisi wengi sana wako jela kwa deal kama hizi....waswahili wanasema ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga!
 
Koba Inasikitisha Sana Kuona Wauwaji Wanajulikan A Kisa Kuna Wakubwa Wa Police Kimya,,haji Sio Siri Alikuwa Ni Mwiba Na Kama Uko Ahera Kuna Vyeo Basi Atakuwa Mwema Wa Ahera Sasa,,

Jamni Ni Kweli Muungwana Kadai Kanunua Gari La Wizi,,ila Si Yeye Napenda Niweke Wazi Wako Wengi ,yale Magari Pale Nje Ikifka 3months Wanuziana Lakin Nane Mpaka Milionn 1.

Gari Za Wizi Kisa Uchafu Umezidi,,,jakaya Analijua Hili,,kuna Jamaa Mchaga Alikuwa Na Cheo Pale Police Mungu Amlaze Hali Pema Ana Gari Kama 20.

kapaka Rangi Nyekundu Na Nyeupe,,nyumbani Kwake Wacha Magari Yanawaka Waka Kila Kona Mpo???? Mwapachu Unajua Hili.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom