(Mfululizo wa FOCAC Dakar) Fursa Mpya za Ushirikiano kati ya China na Afrika (3): China kusaidia Afrika kufanikisha mabadiliko ya nishati ya kijani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1638240445286.png

Mradi wa kuzalisha umeme kwa jua uliowekezwa na Mfuko wa Maendeleo wa China na Afrika nchini Afrika Kusini

Katika miaka ya hivi karibuni, athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi katika bara la Afrika zinaongezeka siku hadi siku, na kuwa “mwuaji asiyeonekana” wa kundi la wanyonge. Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani WMO, mwaka 2020 Afrika ilishuhudia ongezeko la joto, kupanda kwa kina cha maji ya bahari, na maafa ya kimaumbile, na kuzidisha matatizo yaliyopo ya usalama wa chakula, umaskini na kukimbia makazi, na kuwa misukosuko ya kiuchumi na afya.



Wanasayansi wamehitimisha kuwa mabadiliko ya tabia nchi ni matokeo ya shughuli za binadamu zinazopelekea kutoa hewa zinazosababisha ongezeko la joto, kwa maneno mengine hewa ya kaboni. Zikiwa wanachama muhimu wa jamii ya kimataifa, nchi za Afrika zimejitahidi kufanya mabadiliko ya nishati ya kijani na kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni. Hata hivyo, kuna changamoto halisi katika kufanikisha mabadiliko hayo.



Ajenda ya 2063 ya Umoja wa Afrika imeweka lengo la kuhimiza mchakato wa uzalishaji viwandani barani Afrika ili kuondokana na hali ya kuwa nyuma kimaendeleo. Lakini kuinuka kwa Afrika itakuwa ni ndoto ya Alinachana kama bara hili halina maendeleo ya viwanda. Tokea mwaka 1978, watu milioni 850 wameondokana na umaskini uliokithiri nchini China kutokana na maendeleo ya uzalishaji viwandani. Lakini je, nchi za Afrika ziko tayari kuruka kiviwanda? Kwa mujibu wa Shirika la Nishati la Kimataifa IEA, asilimia 55 ya watu barani Afrika, yaani watu milioni 635 bado hawajafikiwa na huduma ya umeme. Kutokana na janga la COVID-19, idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa watu milioni 30. Katika eneo la Afrika kusini mwa Sahara kila mwaka kuna watu milioni 12 wanaoingia kwenye soko la ajira, ambao hawawezi kutafuta maisha gizani, sembuse kusaidia nchi kupata maendeleo ya uzalishaji viwandani.



Kama lilivyosema lengo nambari 7 la ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa: nishati safi kulingana na hali ya uchumi, kupata umeme ni moja ya haki za binadamu. Kuzitumbukiza nchi za Afrika kwenye umaskini zaidi si njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi duniani. Ili kuunganisha upunguzaji wa hewa ya kaboni na maendeleo, nchi za Afrika zinapaswa kukuza sekta ya nishati za kijani ili kutoa nguvu kwa maendeleo ya uzalishaji viwandani barani humo.

1638240483951.png

Mradi wa bustani ya kiviwanda ya vifaa vya kielektroniki nchini Afrika Kusini uliowekezwa na Mfuko wa Maendeleo wa China na Afrika na kampuni ya Hisense

Kwenye mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mjini Dakar, Senegal, rais Xi Jinping wa China alisema, ili kukabiliana na changamoto hii ya mabadiliko ya hali ya hewa inayoikumba dunia nzima, China na Afrika zinapaswa kutetea wazo la maendeleo ya kijani na kukuza nishati endelevu kama vile ya jua na upepo, kuhimiza utekelezaji halisi wa makubaliano ya Paris na kupata maendeleo endelevu. Katika miaka mitatu ijayo, China itasaidia Afrika kutekeleza miradi 10 ya ulinzi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kusaidia ujenzi wa “Ukuta Mkuu wa Kijani” GGW na kujenga maeneo ya vielelezo ya utoaji kidogo wa kaboni na kuzoea mabadiliko ya hali ya hewa.



Hali halisi ni kuwa China sio mgeni kwa maendeleo ya nishati ya kijani ya Afrika na uzalishaji viwandani, na kituo cha kuzalisha umeme kwa maji nchini Guinea kilichozinduliwa mwaka 1966 ni moja ya mifano hiyo. Ikiwa mwenzi wa kudumu wa ushirikiano, katika miaka ya hivi karibuni, China imewekeza sana kwenye sekta ya nishati ya kijani barani Afrika. Takwimu zimeonesha kuwa tokea mwaka 2010, miradi iliyojengwa na China imechangia theluthi moja ya ongezeko jipya la umeme barani Afrika. Sera ya China kuunga mkono maendeleo ya kijani ya Afrika imeleta matokeo mazuri na kuzaa matunda ya mradi wa umeme wa jua mjini Garissa, Kenya, bwawa la kuzalisha umeme wa maji la Karuma, Uganda, mradi wa umeme wa upepo mjini Adama, Ethiopia na miundombinu mingine mikubwa. Kwa mujibu wa IEA, China inajenga miradi ya kuzalisha umeme katika nchi 24 zilizo kusini mwa Sahara barani Afrika, na inatarajiwa kuwa miradi 49 ya kuzalisha umeme itakamilika kabla ya mwaka 2024, na kati ya hiyo mingi ni miradi ya nishati mbadala. Mbali na hayo, mradi wa bustani ya kiviwanda nchini Afrika Kusini uliowekezwa na Mfuko wa Maendeleo wa China na Afrika na kampuni ya Hisense umeleta vigezo vya mazingira na teknolojia husika katika kuzalisha vifaa vya kielektroniki barani Afrika.



Kuhakikisha kila mtu anapata nishati safi ya bei nafuu, uhakika na uendelevu ni msingi wa maendeleo ya viwanda barani Afrika. Afrika inachangia kidogo sana kutoa hewa zinazosababisha ongezeko la joto duniani ikilinganishwa na sehemu nyingine duniani, lakini athari ilizopata ni kubwa mno. Afrika inapaswa kujiunga na mabadiliko ya nishati duniani, lakini haina haja ya kupitia kila kipindi cha maendeleo ya teknolojia, kwani inaweza kupata teknolojia mpya nzuri sokoni na kutoa ufumbuzi mwingi muhimu wa kuendeleza nishati mpya. Inaaminika kuwa China na Afrika zitatumia fursa ya mkutano wa FOCAC wa Dakar, na kufanya maendeleo ya viwanda ya Afrika yanayochochewa na uchumi wa kijani kama fursa mpya ya ushirikiano kati yao.
 
Back
Top Bottom