Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wakanusha kuondoa malipo ya Oksijeni na dawa kwa wagonjwa wenye shida ya upumuaji

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,075
4,111
NHIF.jpg
 
Heparin injection tulikuwa tunauza tsh 5000-6000 Kwa ampoules lkn ndani ya mwezi huu hii sindano haipo TANZANIA na bei yake imefika tsh 18000 Kwa ampoule moja.....
Kwa Sisi ambao tupo Kwenye ishu hizi za madawa tunajua namna changamoto za Corona ni hatari balaa hata ascorbic acid nayo imeanza kuhadimika kutokana na wagonjwa wengi wa Corona kupewa hiyo dawa
 
Tunashukuru kwa ufafanuzi na kwa kazi hiyo nzuri inayofanywa na mfuko huu,
ushauri wangu kwa watumishi wa mfuko huu ni wafanye ufuatiliaji kwa mahospitali
yanayotoa huduma kwa kuingia mkataba na mfuko huu.
Sababu ya kusema hivyo ni kwamba kuna mahospitali ambayo sio waaminifu katika utoaji wa huduma
ktk kutimiza azma zao ovu wanasingizia mfuko wa bima ya afya kwa lengo la kujipatia faida.
Wanaposema dawa fulani hazipo kwenye bima ili ununue kwa fedha taslimu au wanatoa dawa za hali ya chini kwa kudai ndo zinazopatikana kwenye kifurushi cha bima hiyo.
Niliwahi kwenda hospitali mojawapo nikapewa panado za kupima na kijiko,
nilipouliza ni kwa nini nisipewe za blista nikaambiwa hizo ndo zipo kwenye kifurushi cha NHIF,
Nilishangaa na kwa kuwa nilikuwa naumwa niliamua kuondoka na kuangalia ustarabu mwingine mbele ya safari
nilipopata mtu wa kunipa ufafanuzi aliniambia habari hiyo si kweli.

Ushauri wangu kwa watumishi wa mfuko huu,pamoja na taarifa kutoka kwetu walaji
ni vyema kufanya upelelezi wa kushtukiza kwa mawakala wao,hata kwa kwenda kama wagonjwa ili kukagua ubora wa huduma zitolewazo
ili kuepuka kupakwa matope yasiyo ya lazima.
 
Back
Top Bottom