MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewekeza kwa kutoa zaidi ya Sh bilioni 111.7 kwenye ujenzi wa hospitali na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa kat

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1089227


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umewekeza kwa kutoa zaidi ya Sh bilioni 111.7 kwenye ujenzi wa hospitali na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa katika hospitali mbili kubwa mkoani Dodoma. Hivyo, uwekezaji huo umeokoa maisha ya wananchi wengi masikini wasioweza kugharamia uchunguzi na tiba ya maradhi sugu ya go na moyo, kutokana na kulipia kwa kutumia kadi za bima zilizoanzishwa na serikali.

Akizungumzia uwekezaji huo, Osa Habari na Mawasiliano wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Karim Meshark amesema NHIF imewekeza kwa kutoa mkopo wa kujenga hospitali hiyo na kuweka vifaa vya kisasa kwa gharama ya Sh bilioni 104. Aidha, mfuko huo umewekeza katika ujenzi wa jengo la huduma ya bima katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma wa Sh bilioni 7.7.

Meshark alisema uwekezaji huo umewasaidia wananchi wenye magonjwa ya go na moyo, kutibiwa katika hospitali hiyo, badala ya kwenda India kwa kutumia kadi za bima kwa gharama nafuu. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wagonjwa hao walipongeza serikali kwa kuanzisha bima ya afya, wakasema kama si kuwa na kadi ya za bima ya afya, wasingemudu kugharamia uchunguzi na vipimo mbalimbali katika hospitali hizo.

Akizungumza mgonjwa anayesashwa go, Sophia Minja alisema kama si kuwa na kadi ya bima, asingemudu kulipa Sh 200,000 hadi 250,000 kwa siku sawa na Sh 750,000 kwa siku tatu, ambazo zinatakiwa kusashwa. Mstaafu ambaye alikuwa mtumishi wa serikali, Sebastian Lolee kutoka Bahi alisema, amempeleka mke wake ambaye ana matatizo ya go, gharama alizokumbana nazo kama asingekuwa na bima, asingeweza kumudu matibabu hayo ya mkewe.

Mgonjwa anayetibiwa bila kadi ya bima kutoka Mpwapwa, David Habeli alisema ameshindwa kulipia dawa baada ya kutumia Sh 120,000 kwa ajili ya vipimo tu, hivyo anataka kwenda nyumbani kutafuta fedha za dawa, lakini aliwaomba watanzania wajiunge na bima inasaidia sana.

Akizungumza Daktari wa Magonjwa ya Figo, Dk Kessy Shija alisema Mfuko wa Bima ya Taifa wa Afya ni mdau mkubwa kutokana na kutoa fedha za kujenga hospitali hiyo pamoja na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa mbalimbali wakiwemo wenye kadi za bima.

Alisema uwekezaji wa NHIF katika Hospitali hiyo wa Sh bilioni 104 wa majengo na vifaa, umesaidia kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa kati ya 300 au 400 kwa siku. Lakini, pia imepunguza mzigo wa gharama za wananchi wenye kadi, kwani matibabu katika hospitali hiyo ni ya bei kubwa.

Dk Shija alisema kwa wananchi wasio na bima ya afya, wanatakiwa kuwa na fedha nyingi hata kama hospitali inachangia, lakini wananchi wanaofaidi huduma hizo ni wale wenye bima, kwani inasaidia wamudu gharama hizo.

Akizungumza Msimamizi wa Wodi la Wagonjwa Private, Dk Simon Deus alisema wagonjwa wanaolipa fedha kutoka mifukoni mwao kwa siku moja wanalipia Sh 50,000, huku wanaolipa kwa bima wanatoa jumla Sh 70,000, ambapo Sh 40,000 inachangia bima na Sh 30,000 wanachangia wao. Akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Bima katika Hospitali ya Dodoma, Dk Athanas Maselle alisema jengo lilianza mwaka 2016 na linatumika kama Kituo cha Pamoja ambapo wagonjwa wanaotumia kadi za bima wanapata vipimo vyote na kulaza wagonjwa badala ya kwenda hospitali ya rufaa.

Meneja Uhusiano wa NHIF, Angela Mziray alisema Watanzania wanatakiwa kutumia kadi za bima ya afya kwani zinasaidia kupunguza gharama za kupata uchunguzi tiba na matibabu ya kibingwa kwa gharama nafuu. Kwa kujiunga na mfuko wa bima watapata huduma za kibingwa kwa gharama nafuu, ambazo wasingeweza kuzipata bila kuwa na kadi za bima.
 
Back
Top Bottom