Mfuko wa Pensheni wa PSPF, inakuwaje mnawalipa watumishi wengine pensheni ya vyeo vya chini na si walivyo navyo?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Sheria inasema, ukipata cheo kipya unatakiwa ukae na hicho cheo Mwaka mmoja ili uweze ku qualify kulipwa pensheni ya cheo kipya endapo utastaafu.

Kuna malalamiko ya Askari Polisi ambao mmoja alikuwa OCS mkuu wa kituo na wengine 5 walikuwa ma major na sajenti ambao walilipwa pensheni kama ifuatavyo: OCS alilipwa pensheni ya meja, sajenti alilipwa pensheni ya kiwango cha koplo.

PSPF mtusaidie kujua kuhusu hili je mlijisahau au kuna sheria nyingine imetumika kwa wachache na wengine wanalipwa sawasawa, je kuna wakati mnajikuta hamna pesa za kutosha ndio mnaamua kufanya hivyo au fafanueni kwanini hili linatokea.

Hawa wanao lipwa pensheni ya chini ya vyeo vyao wote wanasema hawana mikopo na taasisi yoyote ambayo tunaweza tukasema huenda wanadaiwa wakakatwa hapana.
 
Cheo my foot! Pambana na maisha achana na kuvizia vyeo. Watu tunakesha kwenye mashamba kutafuta riziki miaka na miaka bila cheo unaleta zako za kuleta.
 
Ss mashamba yako yanahusikaje kwenye tatizo la hawa mabwana?
 
Kwanini wahusika wasiende na barua rasmi na vielelezo/ushahidi wao na kujadiliana na taasisi husika ili kupata suluhu ya kudumu?

Mitandaoni ni suluhisho?
 
Unapojaza fomu ya pensheni kati ya nyaraka unazo ambatanisha ni pamoja na BARUA YA MARA YA MWISHO KUPANDISHWA CHEO na SALARY SLIP si kwamba hawaoni na huna vielelezo ulivyo ambatanisha hapana.
 
Kwanini wahusika wasiende na barua rasmi na vielelezo/ushahidi wao na kujadiliana na taasisi husika ili kupata suluhu ya kudumu?

Mitandaoni ni suluhisho?
Hwana majibu ya kuwaridhisha wanaeleweka kuna ujanja unao fanywa nikawauliza kwanini msiseme kama hamna hela ya kutosha kuwalipa watu badala ya kutoa kiwango ambacho hakipo kisheria, wanaingiza siasa.
 
Hwana majibu ya kuwaridhisha wanaeleweka kuna ujanja unao fanywa nikawauliza kwanini msiseme kama hamna hela ya kutosha kuwalipa watu badala ya kutoa kiwango ambacho hakipo kisheria, wanaingiza siasa
Nina mashaka kama mliadress hii issue in writing afu mjibiwe kienyeji kiasi unasema wanaleta siasa.

Hukuridhika na majibu ya reception panda kwa meneja wa eneo hilo kwa majibu zaidi.

Mifuko ya pensheni wanakusanya hela kila mwezi nchi nzima uhaba wa pesa sidhani kama ni sababu kwa uelewa wangu mdogo
Itakua kuna sababu heri kufatilia 'officially' kupata huduma kuliko lawama.
 
Je, ulipopata cheo na mshahara umerekebishwa maana kikotoo kinafuata mshahara.
 
Pesheni kikotoo kinafuata mshahara wa mwisho. Cheo kama umepata na mshahara umerekebishwa hakuna atakaekunyima haki yako. Kuna utata kwenye taarifa.
 
Muhimu usijaribu kupiga simu huduma kwa wateja PSSSF au kuwasiliana nao kupitia mitandao ya kijamii.

Nenda ofisi iliyokaribu nawe directly.

Hicho kitengo cha huduma kwa wateja wanatumia taarifa za ofisi kupotosha wastaafu na kuwatapeli.
 
Nina mashaka kama mliadress hii issue in writing afu mjibiwe kienyeji kiasi unasema wanaleta siasa.

Hukuridhika na majibu ya reception panda kwa meneja wa eneo hilo kwa majibu zaidi.

Mifuko ya pensheni wanakusanya hela kila mwezi nchi nzima uhaba wa pesa sidhani kama ni sababu kwa uelewa wangu mdogo
Itakua kuna sababu heri kufatilia 'officially' kupata huduma kuliko lawama.

Hudhani kama Pesa ni tatizo?

Kwa taarifa yako tu kuna wafanyakazi wa serikali wamestaafu 2017,wakaja kulipwa mafao yao kiasi flani mwaka 2019 then mpk leo hawajamaliziwa pesa zao tena ambazo ni nyingi kuliko walizolipwa Mwanzo, wanapigwa danadana tu. Wanalipwa kwa makundi makundi.

Hakuna pesa.
 
Muhimu usijaribu kupiga simu huduma kwa wateja PSSSF au kuwasiliana nao kupitia mitandao ya kijamii.

Nenda ofisi iliyokaribu nawe directly.

Hicho kitengo cha huduma kwa wateja wanatumia taarifa za ofisi kupotosha wastaafu na kuwatapeli.

Mkuu hio mifuko ina mambo mengi sana ya ajabu.

Siku hizi wastaafu wanalipwa pesa zao kwa mafungu,mtu anastaafu 2017 analipwa pesa yake kidogo 2019 then inayobaki mpk leo hakuna kitu.

Wakiulizwa hapo ofisini wanasema eti wanasubiri rais aweke sahihi.

Wastaafu awamu hii wanaishi maisha magumu sana,omba usistaafu awamu hii nakwambia utauchukia utumishi wako wote.
 
Sioni ajabu swala hili kufanyika maana mifuko haina mamlaka tena wanafanya wanachoelekezwa wakifanye kiwe kibaya kwa wananchi au wastaafu wao hawajali.
 
Ukiona huna cha kuandika ni bora ukapita kushoto, kuliko kujivua nguo kiasi hiki, kumbuka pension sio hisani, ni haki ya mtumishi aliyechangia kwenye pension yake

Back
Top Bottom