Mfuko wa Pensheni wa LAPF: Mkutano wa Sita wa Wadau-AICC-Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfuko wa Pensheni wa LAPF: Mkutano wa Sita wa Wadau-AICC-Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Oct 10, 2013.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,771
  Likes Received: 15,689
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Salaam.

  Niko hapa ndani ya Ukumbi wa Kimaifa wa Mikurtano wa AICC Arusha kuwaletea live ya Mkutano wa Sita wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF.

  Hivi Sasa, mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Hawa Abrahman Ghasia, ameisha wasili, pia waziri wa Kazi, Mhe. Gaudensia Kabaka, Manaibu mawaziri wawili, Kasim Majaliwa na Aggrey Mwanri.

  Ukumbi umeshiba kisawa sawa, Waheshimiwa wabunge lukuki akiwemo Mhe. Kigwangala, Mhe. Machali, Mhe. Wenje, Mhe. Nasari, Mhe. Lusinde etc.

  Wakuu wa mifuko ya hifadhi za jamii, wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Bi Irene Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, GEPF NA NHIF, wamewakilishwa.

  Karibuni muendelee nami nikiwajuza kinachojiri

  Asanteni


  Paskali.

  ---------------------------------

  Background.

  Wana Bodi,

  Mfuko wa pesnsheni wa LAPF Umedhamiria kuongeza ushirikishwaji kwa wanachama wake kuhusu uendeshaji wa mfuko na mafao yatolewayo, ili kuufanya mfuko wa LAPF kuendelea kuwa ni mfuko bora wa Pensheni.

  Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Bwna. Eliud Sanga, wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari, ulifanyika katika hoteli ya Naura Springs, mjini Arusha.

  Bwana Sanga, Amesema, ushirikishwaji huo, utafanyika kupitia Mkutano wake Mkuu wa Sita wa Wadau wenye Kauli Mbiu ya " KUKIDHI KWA MAFAO YA KUSTAAFU; CHANGAMOTO NA NJIA ZA KUBORESHA." utakaofanyika katika Ukumbi wa AICC mjini Arusha, ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Hawa Ghasia.

  Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Valerian Mablangeti, amezungumzia washiriki wa Mkutano huu kuwa ni pamoja na Mamlaka ya Usimamizi Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Waajiri wachangiaji, wanachama, vyama vya wafanyakazi, taasisi mbalimbai za umma na binafsi pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya ndani na nje ya nchi.

  Menaja Matekelezo wa LAPF, Bwana Victor Kikoti, amezungumzia Mada mbalimbali zitakazowasilishwa kutoka ndani na nje ya Tanzania zikijadili kauli mbiu hyo ambazo ni pamoja na Mada anzilishi juu ya kauli mbiu ya mkutano., Mada juu ya dhana ya kukidhi kwa mafao ya kustaafu, Mada ya ulinganifu wa mafao kwa nchi mbalimbali za Afrika mashariki na kati, Mada ya ujasiriamali, Mada juu ya taarifa za utendaji wa Mfuko kwa mwaka wa fedha ulioshia Juni 2013 pia zitajadiliwa.

  Meneja LEPF Kanda ya Mashariki, Amina Salum, amezungumzia Waajiri wachangiaji wa LAPF kwa sasa wanatoka katika makundi ya Halmashauri zote za majiji, Manispaa, miji na wilaya nchini, Wizara zote za serikali, Taasisi zote za serikali, Mashirika ya umma, Sekta binafsi, Mashirika yasiyokuwa ya serikali (NGO's) na Wajasiriamali.


  Hebu Fuatilia.

  --------------------------------------

  [​IMG]


  ------------------------------------

   

  Attached Files:

  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,771
  Likes Received: 15,689
  Trophy Points: 280

  MFUKO WA PENSHENI WA LAPF


  STAAFU KWA UFAHARI

  MKUTANO WA SITA WA WADAU WA LAPF utafanyika Tarehe 11 na 12 Oktoba 2013 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC, JIJINI ARUSHA.

  Kaulimbiu ya mkutano huo ni;

  "UBORA WA MAFAO YA KUSTAAFU: CHANGAMOTO NA UFUMBUZI WAKE".

  Mkutano huo utawashirikisha Wadau mbalimbali katika Sekta Ya Hifadhi Ya Jamii kutoka ndani na nje ya nchi. Mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwa ni pamoja na Taarifa ya Utendaji wa Mfuko kwa mwaka 2012/13.

  Thibitisha ushiriki wako kwa kujisajili kupitia tovuti ya mfuko LAPF Tanzania: Home Page au wasiliana nasi kwa namba 0783 655 655.

  Staafu kwa ufahari na LAPF


  Tangazo limetolewa na Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Pensheni wa LAPF


  ----------------------------------


  [​IMG] P.O Box 1501 Dodoma. Simu: +255 262321952 , Fax: +255 262321701
   

  Attached Files:

 3. T

  Tata JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2013
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,654
  Likes Received: 579
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa nini kusiwe na mfuko mmoja tu wa pensheni kwa watumishi wa umma kuondoa huu utitiri wa mifuko usio na tija kwa wastaafu? Kila siku kuna mfuko uko Arusha kufanya mikutano ya wadau ambao ni watu walewale!
   
 4. Queen Esther

  Queen Esther JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,687
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hongera sana Mfuko wa LAPF.

  kwanza kauli mbiu ya mkutano wenu inadhihirisha mmejiandaa kuzungumza masuala nyeti kwa uwazi zikiwamo changamoto za Mfuko na wanachama kwa ujumla hasa huduma na mafao. Hili ni jambo la kuigwa na mifuko mingine maana unakuta mifuko mingine kauli mbiu tu yenyewe ni changamoto.

  Pili kitendo cha kutangaza mkutano wenu hadi humu JF ni kuwa mnajiamini - hongereni kwa uongozi uliojaa TRANSPARENCY na ukomavu.

  Tatu tuna kuomba Bwana Pascal Mayalla utumie kila kinachoendelea huko na uchangiaji mwingine ufanyike kupitia mtandao huu maana sio wote wanaweza kuja huko.

  All the best.
  Queen Esther
   
 5. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2013
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,321
  Likes Received: 2,749
  Trophy Points: 280
  Mi nipo PSPF
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,771
  Likes Received: 15,689
  Trophy Points: 280
  Mapicha ya matukio mbalimbali

  [​IMG]

  M:Kiti Bodi ya LAPF Prof. Hasa Mlawa akikabidhi zawadi Kwa Mgeni Rasmi

  [​IMG]

  Mgeni rasmi, Waziri Ghasia Akifurahia Zawadi

  [​IMG]

  Zawadi mbalimbali zilitolewa kuthamini baadhi ya michango.

  [​IMG]

  Waziri Ghasia na Waziri Kabaka Wakibadilishana Mawazo..
   
 7. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2013
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,517
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  So? mambo yameisha
   
 8. b

  big_in JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2013
  Joined: Sep 26, 2013
  Messages: 3,434
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  Well noted
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 23,771
  Likes Received: 15,689
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Salaam.

  Niko hapa ndani ya Ukumbi wa Kimaifa wa Mikurtano wa AICC Arusha
  kuwaletea live ya Mkutano wa Sita wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa
  LAPF.

  Hivi Sasa, mgeni rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala
  za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Hawa Abrahman Ghasia, ameisha
  wasili, pia waziri wa Kazi, Mhe. Gaudensia Kabaka, Manaibu mawaziri
  wawili, Kasim Majaliwa na Aggrey Mwanri.

  Ukumbi umeshiba kisawa sawa, Waheshimiwa wabunge lukuki akiwemo Mhe.
  Kigwangala, Mhe. Machali, Mhe. Wenje, Mhe. Nasari, Mhe. Lusinde etc.

  Wakuu wa mifuko ya hifadhi za jamii, wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa
  Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Bi Irene Isaka, Mkurugenzi Mkuu wa LAPF,
  Eliud Sanga, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, Mkurugenzi Mkuu wa
  PSPF, Adam Mayingu. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, GEPF NA NHIF,
  wamewakilishwa.

  Karibuni muendelee nami nikiwajuza kinachojiri

  Asanteni

  Picha: Wajumbe Mbali mbali
   

  Attached Files:

 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Oct 11, 2013
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,971
  Likes Received: 412
  Trophy Points: 180
  Katika mkutano wa LAPF unaoendelea hapa Arusha, Mama mmoja anayeitwa mama sufian ametoa ushuhuda jinsi mfuko ulivyomsaida katika maisha yake, more interesting akadai kuwa Ikulu zamani ilikuwa na heshima sana, ilikuwa ukienda Ikulu unaona kabisa ni Ofisi ya Mkuu wa nchi. Lakini hivi sasa ikulu imekosa heshima, utawala unaonekana umeparaganyika, Ikulu imekuwa kama genge la watu fulani kwa maslahi ya watu fulani, na si kwa ajili ya kuwatumikia watanzania.

  Hayo ni maneno ya Mama Sufiani ambaye amewahi kuwa karibu na Uongozi wa Juu wa nchi.


  Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
   
 11. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2013
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Alikuwa a nazungumzia Ikulu ipi mkuu ,
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Oct 11, 2013
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,971
  Likes Received: 412
  Trophy Points: 180
  Magogoni kamanda. Au sikuizi Tanzania hakuna ikulu?

  Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
   
 13. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2013
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sijui maana ipo ile ambayo Wassira anafunguo zake na milango imefungwa , na ipo ile ya JK ambayo milango imefunguliwa , sasa lazima tujiulize maana nchi hii imechanganyikiwa sana ....
   
 14. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2013
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,949
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mkuu pasco hv ile tv yenu mtairudisha lin iwe mikonon mwa wa nyonge,ili isiwe inapat masharti ya kurusha habar kama ilivyo sasa?
   
 15. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2013
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,187
  Likes Received: 2,173
  Trophy Points: 280
  HOTUBA YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI MHE. HAWA ABDULRAHAMAN GHASIA WAKATI WA KUFUNGUA MKUTANO MKUU WA SITA WA WADAU WA LAPF TAREHE 11/10/2013 KATIKA UKUMBI WA KIMATAIFA WA MIKUTANO (AICC) – JIJINI ARUSHA


  Mheshimiwa Gaudencia Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha;
  Manaibu Mawaziri mlioko hapa;
  Waheshimiwa Wabunge;
  Makatibu Tawala wa Mikoa na Makatibu Wakuu mlioko hapa;
  Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya LAPF;
  Mkurugenzi Mkuu wa LAPF;
  Viongozi wa Wizara, Wakurugenzi wa Halmashauri, Makampuni, Mashirika na Taasisi mbalimbali mnaochangia LAPF;
  Wageni toka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ndani na nje ya nchi,
  Wanahabari, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana.


  Nianze kwa kukushukuru Mwenyekiti wa Bodi, Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini pamoja na Menejimenti ya LAPF kwa kunikaribisha kwenye mkutano wenu huu lakini pia niwapongeze sana kwa maandalizi mazuri ambayo sote tumeyaona.


  Ndugu Washiriki, tumesikia maelezo toka kwa Mwenyekiti wa Bodi kuhusu masuala ya kisera na mwelekeo wa Mfuko lakini pia tumesikia toka kwa Mkurugenzi Mkuu Bwana Sanga kuhusu maendeleo ya LAPF kwa mwaka 2012/2013. Nawapongeza sana kwa mafanikio makubwa mliyopata na nasema jitihada hizo ziongezeke ili wanachama wenu na wananchi wengine waweze kunufaika zaidi.


  Ndugu Washiriki, mkutano huu ni muhimu sana kwani ndio mkutano pekee katika mwaka unaowakutanisha ninyi na hivyo kuwapa fursa ya kujadili hoja mbalimbali toka LAPF. Ni fursa pia kwenu kuweza kuueleza uongozi mambo ambayo mngependa Mfuko ufanye kwa manufaa yenu na wananchi kwa ujumla. Hivyo tutumie vizuri sana siku hizi mbili za mkutano kuibua maazimio ambayo ninyi pamoja na Mfumo mtaenda kuyafanyia kazi.


  Tumeambiwa kuwa kauli mbiu yetu ni Kutosheleza kwa mafao ya Kustaafu: Changamoto na Njia za Kuboresha. Kauli mbiu hii ni muhimu sana ikajadiliwa kwa kina kwa matokeo ya mjadala wake itatupa mwelekeo wa nini kifanyike kuboresha zaidi mafao ya wanachama wa Mfuko. Ni kweli kabisa wapo wastaafu wetu wamepata fedha nyingi sana lakini ndani ya mwaka mmoja au miwili fedha hizo zinakuwa zimekwisha na hakuna jambo la msingi walilofanya.


  Inaonyesha dhahiri kuwa nidhamu ya utunzaji fedha kwa watumishi na wastaafu wengi ni tatizo. Ni vizuri eneo hili likajadiliwa kwa kina na mkaondoka hapa na maazimio ya kurekebisha dosari hii. Najua kuwa uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii uko hapa. Naomba mtumie nafasi hii kuona namna ambavyo mnaweza kuboresha sekta hii ili iwanufaishe walengwa zaidi.


  Nimeambiwa pia kuwa ipo mada kwa ajili ya mbinu za ujasiriamali. Tupende tusipende ujasiriamali haukwepeki kama tunataka kumaliza sehemu yetu ya maisha kwa furaha na amani. Kila shughuli utakayoifanya baada ya kumaliza utumishi wako ni ujasiriamali na shughuli hiyo itakuwa na manufaa kwako endapo utakuwa umeifanyia maandalizi ukiwa bado kazini. Wale wanaokimbilia kujifunza biashara kwa mfano ya daladala baada ya kustaafu kimsingi wanajitafutia matatizo. Sio biashara nyepesi kama wanavyofikiri ila ni rahisi endapo imefanyiwa utafiti wa kutosha juu ya namna ya kuisimamia. Hivyo naona Mfuko umefanya jambo la msingi sana kuleta mada hii hapa. Aidha, nashauri isiishie hapa ila nanyi mhakikishie kuwa watumshi wengine walio kule maofisi wanapata taaluma hiyo japo kwa uchache.


  Ndugu Washiriki, katika sekta hii ya hifadhi ya jamii huduma bora ni jambo muhimu mno. Wastaafu wengi wanasumbuka kupata mafao yao wanakuwa wamestaafu. Leo nafurahi kusikia na kuona kuwa LAPF sasa inaweza kulipa wanachama wake kabla au katika siku ya kustaafu. Hili ni jambo zuri nami nashauri waajiri mlichukue kwa umuhimu wake kwa kuhakikisha wale wanaokaribia kustaafu maombi yao yanawasilishwa LAPF angalau miezi mitatu minne kabla ya tarehe ya kustaafu ili Mfuko uweze kufanya malipo kama tulivyoona leo hapa. Huduma bora ni kivutio kikubwa cha wanachama hivyo mkiendelea na kasi hiyo hakika mtapata wanachama wengi zaidi.


  Ndugu Washiriki, nitoe rai kwa Mfuko wa LAPF kufanya kazi moja. Angalieni uwezekano wa kutoa "Guarantee" kwa wanachama wenu ili wapewe mikopo na mabenki. Hii itasaidia kukuza mitaji yao na kuzalisha zaidi, hivyo kua na uwezo wa kuchangia zaidi katika mfuko. Ni matumaini yangi likifanyiwa kazi jambo hili linaweza likawa ni fursa kwa Mfuko na wanachama pia.


  Mwaka jana tulizungumza kuhusu uwezekano wa kutoa mikopo ya elimu kwa wanachama wa Mfuko. Leo mmesema kuwa jambo hili sasa liko kwa mtathmini wa Mfuko. Naomba liharakishwe kwani nina uhakika wanachama wenu wanalisubiri kwa hamu kubwa sana.


  Ndugu Washiriki, nikirudi sasa kwenu, nawaomba sana mtimize wajibu wenu kwa kuwasilisha michango kwa wakati. Michango hii inahitaji kuwekezwa kwa wakati ili kuujengea Mfuko uwezo wa kuboresha zaidi mafao ya wanachama wenu. Sasa inapocheleweshwa ni hatari mfuko kupoteza mapato na hivyo uwezo wa kuboresha zaidi mafao.


  Ndugu Washiriki, Sheria ya Mamlaka imetoa uhuru wa watumishi wapya kuamua Mfuko wanaoupenda, hii ni njia nzuri ya kujenga mazingira ya ushindani na kuhakikisha kila mfuko unaboresha huduma zake na mafao yanayotolewa ili kuweza kupata wanachama zaidi. Waajiri mnapaswa kutoa fursa kwa mifuko kujieleza mbele ya watumishi wapya kila mnapowaajiri ili wafanye maamuzi sahihi kuhusu mfuko wanaotaka. Naomba kusiwe na upendeleo au mizengwe ya aina yoyote katika eneo hili.


  Aidha, wanachama mnaofaidi na mikopo ya LAPF kupita SACCOS zenu muendelee kurejesha fedha husika kwa wakati na pia muwe na mipango madhubuti ya kuitumia mikopo hiyo ili ionekane kuwa na manufaa kwenu na kuwaletea maendeleo. Nashauri LAPF na Mifuko mingine muwaelimishe wanachama wenu jinsi ya kusimamia mikopo hiyo ili iwe na tija kwao.


  Mwisho napenda kuwashukuru tena kwa kunipa heshima hii na kuipongeza kwa dhati Bodi ya Wadhamini na Uongozi wa LAPF kwa kazi yenu nzuri. Nasema endeleeni na kazi hiyo kwa manufaa ya wanachama na Taifa kwa ujumla. Baada ya kusema hayo machache sasa natamka kuwa mkutano wa sita wa Wadau wa LAPF mwaka 2013 umefunguliwa rasmi.


  ASANTENI SANA
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2013
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 145
  Honestly bado sijaridhika na namna LAPF pamoja na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii inavyowatendea wanachama wao.

  Kwa vitegauchumi vinavyojengwa na mifuko hii lingekuwa jambo la busara sana kama wanachama wangekuwa wanafaidika moja kwa moja na uwekezaji huo unaofanyika.

  Wanachama wa mifuko ya jamii wanahangaika kujenga nyumba za kuishi ama kusomesha watoto wao kwa ugumu na hata kukopa katika mabenki ya kibiashara kwa riba kubwa wakati mifuko hii ingeweza kabisa kuwasaidia wanachama wake kujikwamua na matatizo ama mahitaji kama hayo.
   
 17. Mtingaji

  Mtingaji JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2013
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 1,218
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Nilimsikia Mkurugenzi Mkuu wa LAPF kwenye Luninga kuwa mwanachama aliye kamilisha vigezo vya kustaafu, hulipwa Lump sum mara 2 mpaka 3 ya michango yake kisha anaendelea kupata pension kama kawaida. Nilifurahishwa sana lakini NALIA na mfuko wangu wa NSSF ambao umetekwa na MAFISADI ambao mwanachama aliyekidhi vigezo vya kustaafu, hasa aliyekuwa anachangia zaidi ya milioni kila mwezi, atalipwa Lump sum kama robo ya michango yake, kisha robo tatu atakuwa anapewa kiduchu kiduchu mpaka afe...!

  Nawaombeni LAPF muache maneno mengi, njooni kwa watingaji migodini mchukue wanachama tuondokane na minyororo ya NSSF-Mafisadi!
   
 18. b

  bandu bandu JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2013
  Joined: Sep 7, 2013
  Messages: 2,560
  Likes Received: 386
  Trophy Points: 180
  wezi tu hao hizo fedha za wanachama baada ya kufanyia mambo ya maana mnakopeshana na kujidai kuziwekeza kwenye vimajengo uchwara tupeni interest ya maana wanachama acheni wizi mifuko kibaaaao mara PSPF,NSSF.PPF,GEPF wich is wich kuweni na mfuko mmoja na wa kueleweka eboo.
   
 19. Mwanyasi

  Mwanyasi JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2013
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 5,717
  Likes Received: 1,845
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimeipenda hii!
   
 20. Queen Esther

  Queen Esther JF-Expert Member

  #20
  Oct 13, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,687
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mkuu Asante kwa taarifa, nimeendelea kufatilia nikitegemea kuona na papers ilituzichangie sijazipata.
  is it possible ukaziweka tuchangie?
  Queen Esther
   
Loading...