Hapa sio issue ya wananchi wanataka nini, hapa ni ulaji na kuhodhi majimbo kwa kisingizio cha mimi nimeleta maendeleo haya a haya hivyo nichagueni mpaka kufa kwangu. Tunatengeneza wabunge wa maisha.Wale Wabunge waliotarajiwa kupinga huu mfuko, hasa wapinzani nao wameziba masikio na pamba. Hapa ndio kwa kiasi fulani tunapata Wabunge wetuwengi wako Bungeni kwa maslahi yao binafsi kuliko kuangalia Wananchi wanataka nini.
Mkutano wa kukusanya maoni ya wadau kuhusu muswada wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (Comunity Development Catalyst Fund-CDCF) uliofanyika jana mchana kwenye ukumbi wa Msekwa ulitawaliwa na vuta nikuvute kati ya Wabunge na wanaharakati wakiongozwa na Policy Forum.
Mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mbunge wa Mpwapwa, George Malima Lubeleje, ulifunguliwa kwa hotuba ya Waziri wa Serikali za Mitaa, Bibi Celina Kombani aliyeutetea mfuko huo huku akiungwa mkono na wabunge wote waliochangia wakiwemo wa upinzani ambapo Dr.Slaa alikomelea msumari wa moto kwenye jeneza la wanaharakati kuupinga muswada huo.
Nimefanikiwa kuupata muswada wenyewe na kuuscan sambamba na taarifa ya Policy Forum.
Swali ni moja tuu, baada ya kuuona muswada wenyewem hawa wanaoendelea kuupinga ni kweli wanasukumwa na utashi wao na dhamira za dhati, au ni kupuliza tarumbeta kusuport msimamo wa wafadhili wanaowapo fedha na posho za kuendesha mashirika yao?.
NB. Nimejaribu kuatach muswada na msimamo wa serikali zimenigomea
Hapa sio issue ya wananchi wanataka nini, hapa ni ulaji na kuhodhi majimbo kwa kisingizio cha mimi nimeleta maendeleo haya a haya hivyo nichagueni mpaka kufa kwangu. Tunatengeneza wabunge wa maisha.
Mkuu,
Yaani umemaliza yote yote kabisa ktk hili.
Mimi wala sitaki kabisa kusikia hii kitu. Yaani bunge limeshindwa kuisimamia na kuidhibiti serikali yenyewe inataka ipewe fedha iende yenyewe! Independence itakuwa wapi??? Nani atauliza kama fedha za mfuko zitatumiwa vibaya??? Who is going to question that?? Upuuzi upuuzi kabisa.
Mkuu Pasco hapa sijakuelewa vizuri, unaunga mkono kuanzishwa kwa mfuko huu na unawashangaa wanaharakati kuupinga japo unaamini kuwa lengo lake ni kutengeneza ulaji na kuhodhi majimbo.
Msimamo wa Dr. Slaa katika hili ni vyema ukatazamwa kwa kuangalia role yake katika kuanzishwa kwa muswada huu. Picha yenyewe ilianzia kwake, yeye na kamati anayoiongoza walianza kufanya utafiti juu ya mifuko kama hii huko Kenya, Malawi na India.Kwa bahati mbaya Slaa na wenzake hawakwenda kujifunza bali walitaka ku confirm wanachokitaka hivyo walifumbia macho uozo wote waliouona na kurudi kuishauri serikali kuanzisha mfumo huo. Japo si suala jema kulizungumzia kwa sasa ila Slaa na kamati yake walitumia pesa za walipa kodi 'hovyo hovyo' na kushindwa kuishauri serikali vizuri. Na kwa kuwa serikali inalengo la kulidhoofisha bunge hasa baada ya mhimili huu kuanza kuonesha cheche zake ililikubali wazo hili harakaharaka. Pasi kufanya tafiti au kusikiliza ushauri kutoka pande nyingine serikali imedhamiria kulipeleka suala hili mbele kwa kujua iwapo wabunge watalipitisha litakuwa ni aibu kubwa kwao kwa sababu mosi kutokusikiliza wananchi ambao wao ni wawakilishi wao na pili ni kushirikiana nao(serikali) kuvunja katiba hivyo mara zote wataendelea kuoneana aibu.
Asante Mwita Maranya kwa kunielewa, mimi ni realist, hata kama siupendi huu mfuko, ni ulaji kwa wabunge, hata upingwe vipi leo unapitishwa. Kama realist ni lazima kukubali matokeo ya ambayo lazima yatatokea.Pasco anatambua kwamba huumfuko ni ulaji kwa namna nilivyomuelewa, lakini anaonekana kukubaliana na hali hiyo kwa vile wanaoupinga wanapata vijisenti vya wafadhili na kwamba anaona bora wabunge nao wapate vijisenti vya kuwapa wananchi takrima wakati wa uchaguzi wa mwakani.
Ninao na nimeuscan ila unagoma kujiatach sijui tatizo nini, kesho nitamtupia invi aubindike ila fainali ndio leo, jamaa wanaupitisha.Tatizo letu watanzania ni kupenda kupinga kila kitu. I for one support this. Wekeni huu muswada hapa halafu tuujadili.