Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo: CDCF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo: CDCF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jul 29, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,603
  Trophy Points: 280
  Mkutano wa kukusanya maoni ya wadau kuhusu muswada wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo (Comunity Development Catalyst Fund-CDCF) uliofanyika jana mchana kwenye ukumbi wa Msekwa ulitawaliwa na vuta nikuvute kati ya Wabunge na wanaharakati wakiongozwa na Policy Forum.

  Mkutano huo uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mbunge wa Mpwapwa, George Malima Lubeleje, ulifunguliwa kwa hotuba ya Waziri wa Serikali za Mitaa, Bibi Celina Kombani aliyeutetea mfuko huo huku akiungwa mkono na wabunge wote waliochangia wakiwemo wa upinzani ambapo Dr.Slaa alikomelea msumari wa moto kwenye jeneza la wanaharakati kuupinga muswada huo.

  Nimefanikiwa kuupata muswada wenyewe na kuuscan sambamba na taarifa ya Policy Forum.

  Swali ni moja tuu, baada ya kuuona muswada wenyewem hawa wanaoendelea kuupinga ni kweli wanasukumwa na utashi wao na dhamira za dhati, au ni kupuliza tarumbeta kusuport msimamo wa wafadhili wanaowapo fedha na posho za kuendesha mashirika yao?.


  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
   

  Attached Files:

  Last edited by a moderator: Aug 1, 2009
 2. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Pasco,

  Mimi nitaungana na Wanaharakati wa Azaki kwa kuwa ni ukweli kuwa Serikali (Kuu, Bunge na Taasisi zake) hazina nidhamu nzuri za matumizi ya fedha na zaidi zina uzembe na uzorotaji wa hali ya juu kuhakikisha mipango ya maendeleo inafanyiwa kazi na kila hatua inafanyiwa tathmini makini kuhakikisha kuwa ni hatua chanya zinaendelezwa na kuongezewa nyenzo na hatua hasi, zinahakikiwa na kusahihishwa.
   
 3. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280
  Pasco, hayo ni maoni yako, ukiwa mtanzania anayeipenda nchi yake au wakala? Ni vigumu kuamini kuwa wapo watanzania, tena waelewa katika mtandao wa JF, ambao hawawezi kutofautisha kati ya kazi za Bunge/wabunge, kazi za Mahakama na kazi za Serikali (watendaji)!
  Elimu kwa wote:

  1. Hoja za wabunge juu ya umaskini majimboni hazisisitizi matakwa ya maendeleo majimboni bali uwezo wa kutoa michango kwa wananchi wanaoomba kusaidiwa, mf; harusi, elimu, na shughuli nyingine za kijamii.
  2. Matatizo ya maendeleo majimboni hayatokani na ukosefu wa fedha bali mfumo wa utawala wa kikoloni usioelekeza utendaji katika serikali za mitaa kufuata uwakilishi wa majimbo. Bila kurekebisha mfumo huu hata ukipeleka mabilioni mangapi, hakuna kitakachofanyika kwa manufaa ya wananchi isipokuwa kashifa za rushwa (na hili tusubuiri kidogo tuone)
  3. Kazi kuu za wabunge ni tatu; kutunga sheria, kuwakilisha wananchi katika maamuzi ya serikali, na kusimamia/kudhibiti utendaji wa serikali, siyo kufanya shughuli za serikali kama inavyobainishwa katika mswada wa CDCF.
  4. Kwa kuwa wabunge wameona serikali imeshindwa kupanga na kutekeleza shughuli za kuleata maendeleo majimboni, basi kwa mujibu wa mamlaka yake wailazimishe serikali kujiuzuru badala ya wao kutaka kuingia katika steering; siyo kazi yao.
  5. Majimbo ya uchaguzi siyo makampuni ya biashara kiasi kwamba yapewe mitaji ya kuyaendeleza.
  6. Mbali ya yote, tukumbuke maneno ya busara ya Mwl. Nyerere kuwa pesa siyo msingi wa maendeleo, bali matokeo ya maendeleo. Msingi wa maendeleo ni kazi, period!
  Wasomi tusiwahadae bali tuwasaidie watanzania kuelewa na kuchambua ujumbe uliofichika ndani ya CDCF.
   
 4. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Umenena vyema mkubwa. Hiki ni kichaka kingine tena cha ufisadi tunachokitengeneza.
  Tusipokuwa macho hii nchi italiwa hadi iishe kabisa. Kwa sababu hawa wabunge ni watu tuliotegemea kusimamaia utendaji wa serikali, na sio wao kuwa watendaji kwa niaba ya serikali.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wabunge wanaumizwa jinsi na wao wanavyokosa ulaji (kwa njia za rushwa) kama ambavyo watendaji wa serikali wanakula. Wabunge inawauma kuwa fedha zinazoliwa na watendajiw a serikali ni wao ndio wamezipitisha kwa hiyo na wao wanataka kujitengenezea mrija ili fedha zifike na kwao. Katika hili, kwa sababu watendaji wa serikali wanataka kuendelea 'kulindwa' na wabunge, lazima wataungana nao katika kushinikiza mfuko huu.
  lakini pia fedha hizi zinaweza kuwasaidia wabunge kwenye kampeni zao mwakani. Kumbuka kuwa iwapo sheria hii itapitishwa, bajeti itaanza kupangwa mwaka kesho na wakati wa kampeni ndio majimbo mengi yatakuwa ndio kwanza yamepokea mabilioni hayo. Hii itawasaidia wabunge hasa katika maeneo ambako wananchi hawana uelewa mkubwa, zitaelezwa kuwa ni fedha zilizioletwa na mbunge.
  Lakini pia wabunge wanaweza kuwa wamesukumwa na dhamira ya dhati ya kutaka kusaidia maendeleo katika maeneo yao, ingawa hilo linapaswa kuthibitishwa na jinsi mfuko wa jimbo utakavyoendeshwa. Wabunge wasihusishwe kabisa katika endeshwaji wa mfuko huu. Tunaweza kuiga mfumo wa kenya ambapo mbunge ni kama patron to wa mfuko huu na wala ahusiki na uendedhaji wa shughuli za mfuko wa Bunge. wakikubali hivyo, nitaanza kuamini kuwa wabunge wana dhamira nzuri, lakini wakitaka nao wawemo ndani, naamini itakuwa ni kwa lengo la kujinufaisha binafsi zaidi kuliko kuwasaidia wananchi
   
 6. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Sasa hawa wabunge kama wanataka kuwa watendaji wa serikali si wakaajiriwe kwenye Halmashauri zetu!? wao watasimamiwa na nani kwenye huu mfuko? wezi watupu...Wao kazi yao ni kusimamia utendaji kazi wa serikali na kama wanaona serikali haifanyi kazi yake sawa sawa basi waiwajibishe!!!
  UFISADI mtupu huu....
  nchi inaudhi sana hiiiiiii
   
 7. Joste

  Joste Senior Member

  #7
  Jul 29, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajameni, Niliangalia kwenye Luninga Juzi wakati Mwanaharakati Marcos akitoana jasho na Mzee Cheyo na Mbunge Mmoja kutoka pemba. Mitizamo ya wabunge ilionyesha wazi kuwa mfuko huo utawapa ahueni ya kuchangia maendeleo bila kutumia pesa zao. Vilevile utasaidia wabunge wanyonge na maskini kuweza kutamba na kuranda huko na huko jimboni waki pliji lile na hili. Najiuliza maswali mengi lakini kwa leo nataka kuuliza:

  1. Ni kwa namna gani mfuko huo utatumika kufuatana na sheria na kanuni za fedha zilizopo na zitakazo kuwepo?
  2. Je, Mbunge atakuwa accountable kwa nani na kwa namna gani?
  3. Kama katika hali ya sasa wabunge wengi wanakaba kupanuliwa kwa democrasia, yaani kunyima watu wengine wasigomembee, je fedha hizo hazitakuwa zinatumiwa kwa madhumuni hayo?
  Wanaharakati, naomba hoja zenu mziweke ukakasi katika maswali hayo

  Naishia
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mimi naunga mkono; wakishaanzisha mfuko huo ambao wao wabunge watausimamia wahakikishe pia mifuko ifuatayo inaundwa vile vile.

  Mfuko wa Maendeleo ya Shule za Msingi ambao utasimamiwa na walimu

  Mfuko wa Maendeleo ya Ulinzi wa Raia ambao utasimamiwa na Polisi

  Mfuko wa Maendeleo ya Benki Kuu ambao utasimamiwa na Benki Kuu

  Mfuko wa Maendeleo wa Wilaya ambao itakuwa inasimamiwa na wakuu wa wilaya

  Mfuko wa Maendeleo ya Kijiji ambao ambao utasimamiwa na wanakijiji!!

  Well.. while we are at it.. mfuko wa maendeleo ya Ufisadi utakaosimamiwa na Mafisadi wenyewe!!!!

  Anybody else got a new idea ya mfuko mpya baada ya kushindwa kusimamia fedha zetu kwenye taratibu zilizopo tayari?
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Mkuu,
  Yaani umemaliza yote yote kabisa ktk hili.
  Mimi wala sitaki kabisa kusikia hii kitu. Yaani bunge limeshindwa kuisimamia na kuidhibiti serikali yenyewe inataka ipewe fedha iende yenyewe! Independence itakuwa wapi??? Nani atauliza kama fedha za mfuko zitatumiwa vibaya??? Who is going to question that?? Upuuzi upuuzi kabisa.
   
 10. c

  cammory Member

  #10
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja yako mkuu.
   
 11. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu MMKJJ (angalizo) namba 2 huo mfuko usisimamiwe na mapolisi usimamiwe na raia wenyewe . Polisi nao wemeshapoteza mwelekeo na hata imani kutoka kwa wananchi.
   
 12. MamaParoko

  MamaParoko JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2009
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 465
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .........mfuko wa maendeleo yangu utakaosimamiwa na mimi mwenyewe.
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Huu ni ufisadi mwingine tena. Ukisoma kiundani zaidi utaona Hapa Serikali inataka iape wabunge hongo ili waweze kulitumia katika kampeni za uchaguzi mara baada ya EPA kugundulika.

  Hakika siungi mkono MFUKO HUO kumilikiwa na Mbunge.

  Kwani wabunge wengi hawaishi majimboni mwao. Kama Serikali ina nia nzuri na wananchi basi mfuko huo usimamiwe na madiwani kwani wao wanabanwa kisheria kuishi kwenye maeneo wanayoyaongoza
   
 14. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Hatuweze kuendelea kwa kuanzisha "Mifuko"!

  Uongozi bora (Responsible and Accountable) ndiyo tunachopungukiwa tu. NUKTA

  Hii "Mifuko" ni njia mojawapo ya kuhalalisha matumizi "hewa"!
   
 15. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Pasco, sijakuelewa hapa, ina maana Dr. Slaa aliungana na Wanaharakati kupinga mfuko wa jimbo, ama aliiuunga mkono ndio ukawa ni msumari wa moto kwa wanaharakati?.

  Lakini kwa vyovyote iwavyo, huwa Serikali yetu na Wabunge pia hutia pamba masikioni na kutosikiliza vilio vya Wananchi. Kwa hiyo haya maoni utakuta hadi mwisho watapeleka huo mswada Bungeni, na kwakuwa Wabunge karibu wote wako kwa ajili ya mambo yao binafsi wataupitisha. Huo ni ulaji wao Wabunge, si rahisi wenyewe wakajikwamisha. Kama walipoingia tu madarakazi wakati ule kuna ukame mkubwa TZ walitaka hapo hapo kujiongezea mshahara na marupurupu, seuze waukatae huu muswada.

  Dawa ya kurekebisha haya yote ni sisi wenyewe wananchi, haiwezekani Wabunge waishi daraja la kwanza wakati Mwananchi hata mlo mmoja inakuwa kazi. Na bado wanapata kila kitu na hawaridhiki wanataka kujiongezea. Dawa ni kuwaondoa wote ndio watakuja shika adabu, lakini vipi tutawaondoa wakati ndio watoa takrima wakubwa, wezi wa kura, wanadaidiwa na vyombo vyote vya dola wakati wa uchaguzi. Kazi tunayo lakini mwisho tutashinda, nguvu ya Wananchi hakuna wa kuizuia pale tutakaposema wote sasa BASI!.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Jul 29, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,603
  Trophy Points: 280
  Asante sana Mfumwa, wewe ni mmoja wa marealist humu JF, wengi wetu ni ma wishful thinkers ambao we just wish, na marealist ni wale wakubali ukweli hata kama hutakubaliana nao.
  Nimejaribu kuuweka hapa muswada umenigomea, mimi nimeusoma, sijaona tatizo kupeana ulaji. Ofisi ya Bunge ilipokuwa ikiendeshwa na sub-vote ya Waziri Mkuu, kulikuwa na nidhamu ya matumizi. Sasa ofisi ya Bunge inavote yake inayojitegemea, Ofisa masuhuli ni katibu wa bunge, mmeona matanuzi ya spika six, licha ya nyumba, anatumia s-class 500 model ya 2005 sasa kaagiza s-class 720 inayotoka 2010!. Mbona hamlalamiki.
  Masikini mhimili wa mahakama bado umefungwa na mbeleko ya vote ya wizara ya sheria, ni njaa kali unategemea wasile rushwa!
  Mbona madiwani ndio wanaosimamia fungu la halmashauri tena kwa kujimegea vjiposho vya misururu ya vikao visivyokwisha na wala havina tija, issue ni ulaji, sasa akila mbunge ndio inageuka nongwa?!.
  Kamanda nambari moja wa vita vya ufisadi, Dr. Slaa ndio mtetezi mstari wa mbele na kikao cha jana ndie aliyepiga nyundo msumari wa moto kukomelea jeneza la wanaharakati, waliotarajia muswada ufe uzikwe, sasa wao ndio kifo, mazishi ni keshokutwa Ijumaa utakapopitishwa kwa kishindo na bunge zima.
  Nimeuona muswada, mbunge hashiki fungu, yeye ni msimamizi tuu. Hivi mnajua wanene wanapochangia shughuli mbalimbali/harambee fedha hazitoki mifukoni mwao, sasa wabunge wanawezeshwa ili nao wajitutumue, sio mpaka Mkono/Rostam au Dewji wanaoleta jeuri ya fedha na kupita bila kupingwa. sasa ni kila mbunge aliyepo anapewe jeuri ya kutoka kifua mbele kumilikishwa jimbo kama walivyomilikishana nyumba za serikali.
  Mfuko wa majimbo hoyee! Kidumu Chama Cha Mapinduzi. Na ufisadi mzuri wa kimaendeleo nao udumu, bila ufisadi wengine hammer, vogue na ferari (gari za Tanil) tungeishia kuziona kwenye picha, sasa twazishuhudia kwenye barabara zetu, si ndio maendeleo yenyewe haya!.
   
 17. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #17
  Jul 29, 2009
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Ukishindwa kutumia rasilimali zako vizuri, na watu wakaona na kugundua, unabuni mbinu mbalimbali za kuendelea kuwaibia na kutumia hizo rasilimali.
  Huo Mfuko wa mendeleo ya Jimbo ni kiini macho cha kutafuna hela hata ile kidogo iliyo kwenye mifuko ya wananchi. Jimbo linapokuwa kama kampuni ya kabaila, sijui maafisa wa kata na tarafa watabaki wapi, na wilaya itukwa na mchango gani katika maendeleo ya Jamii.
  Nadhani elimu ya kutosha kuhusu faida za huo mfuko ingetolewa kwanza ili kuondoa mashaka na kutopoteza lengo zuri (KAMA LIPO). Mbali na hapo ni wizi mtupu kwa kundi la wateule wachahce wa kufaidi rasilimali za nchi, ambazo ni kama shamba la bibi sasa.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jul 29, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,603
  Trophy Points: 280
  Kama wenye dhamana ya matumizi mazuri ya fedha ndio wezi wakubwa huku wasimamizi wabunge wakiishia kupiga kelele tuu, kuna ubaya gani kama nao wamebuni mbinu?

  ''if you can't beat them, join them"
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna mifuko mingapi ya serikali inayolenga maendeleo?

  Hivi kuwa na mifuko hii kunataka kutatua tatizo gani hasa?
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,603
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika na idadi halisi ya mifuko ila mfuko mkubwa kabisa kwa ajili ya maendeleo ya jamii ni TASAF-Tanzania Social Action Trust Fund.
  Pia kuna Mfuko wa Rais wa Maendeleo ya Jamii. Kuna Mfuko wa Kujitegemea SELF na kuna Social Action Trust Fund-SATF mwisho ni yale mabilioni ya JK.
  Mzee Mwanakijiji, kusema ukweli huu mfuko wa maendeleo ya jimbo ni kupeana ulaji kihalali na kulindana kwa ajili ya 2010. Kama rushwa ni kila mahali, kuhalalisha ulaji ni rushwa safi kama pesa ya kamisheni.
   
Loading...