Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi(WCF) unafanyaje kazi?

uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
1,424
1,966
Habari za majukumu wakuu.
Kama kichwa kinavyojieleza,serikali iliunda
mfuko huu ambao ni sheria kuchangiwa na kila mwajiri.
Kabla ya mfuko huu kuanzishwa waajiri walikuwa
wanahusika kuwalipa wafanyakazi wao fidia pale wanapopata
matatizo/maafa kutokana na kazi wanazozifanya,lakini pia
mashirika kama NSSF yamekuwa yakisema yanatoa fidia
kwa mfanyakazi ambaye ni mwanachama na akapatwa na matatizo.
maswali yangu ni:
1.Je,endapo mfanyakazi ni mwanachama wa nssf akipatwa na ajali analipwa mara mbili
au ni moja kati ya hii mifuko miwili?
2. Kuna makampuni yana bima za maisha kwa wafanyakazi wao
je,kunapotokea tatizo mwajiri atamlipa mfanyakazi kwa bima ya maisha
inayolipwa na kampuni au ni WCF au vyote viwili?

Kwa wataalama wa maswala haya naomba mnijuze
Natanguliza shukrani.
 
Maswali mazuri sema watu wamejaa kwenye udaku. Natamani kupata majibu toka kwa wenye kujua
 
Uzi mzuri sana ,uliokosa mchango?,inasikitisha sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu inawezekana wafanyakazi /waajiriwa wa mifuko husika hawomo humu jf
maana nilitegemea wao kwa uzoefu wa kazi zao watanisaidia kutoa majibu.
Ua huenda ni kinyume na maadili yao ya kazi,maana mambo mengi ya bima
yana maswali mengi kuliko majibu.
 
Back
Top Bottom