Mfuko wa bima ya afya ni kero kwa wafanyakazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfuko wa bima ya afya ni kero kwa wafanyakazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 19, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mfuko wa Bima ya afya uliingizwa kinyemela.Wala wafanyakazi hatukuhojiwa kama tunapenda au laa.Kwa hiyo mishahara yetu ilikatwa bila ridhaa yetu.Kitendo hiki kisheria si halali,na nadiriki kusema kwamba serikali ilikiuka haki za msingi za wafanyakazi wake.Kana kwamba hilo halitoshi,bado mfuko huo umeendelea kuwa kero kubwa kwa wafanyakazi.Mpaka leo wafanyakazi wengi hawana vitambulisho na vituo viko mbali mno na wafanyakazi,kiasi kwamba wengi hatupati huduma hiyo muhimu.Jambo la kushangaza ni kwamba uongozi wa mfuko huo hauonyeshi jitihada zozote za dhati za kupeleka huduma hiyo karibu na wanachama wake.Hata pale unapojikongoja na kufika kwenye kituo chote chote kinachotoa huduma hizo, huduma kwa ujumla ni mbovo sana.Hata zile huduma ambazo mfuko unasema unatoa kama vile miwani ya macho,matibabu ya Typhoid nk.vituo vingi hata kama vina uwezo wa kutoa huduma hiyo vinasema havitoi.Mimi binafsi nimeanza kukatwa huduma ya afya zaidi ya miaka mitano iliyopita,kwa kiwango cha Sh.20,000 kwa mwezi,lakini nimeshawahi kupata huduma hiyo mara tatu tu.Jamani kama sio uonevu huo na wizi wa hela zetu ni nini.Malengo ya huduma hiyo sio mabaya,lakini utekelezaji wake ni mbaya mno.Naomba serikali ichukue hatua za dhati za kusimamia uboreshwaji wa huduma zinazotolewa na mfuko huo.
   
 2. N

  Nansawa Senior Member

  #2
  Sep 23, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa kweli mfuko unaboa! na kweli ni MFUKO!! maana tunatunisha tu mifuko na matumbo ya wakurugenzi wake. Wanachojua ni kukopeshana marangerover tu! Kwanza kuna ufisadi uliwahi ripotiwa hapa kutoka NHIF. mNAJUA ULIISHIA WAPI? ULIZIMWA KWA GHARAMA KUBWA BADALA YA KUTULETEA HUDUMA WANAFUNGA SAFARI NJE YA JIJI ETI KUMSAFISHA HUYO MKURUGENZI MKUUJamani msicheze na pesa za sie wagonjwa tusiopata dawa nyie mnatanua . Jirekebisheni kabla hatujaaamua sie wanachama hatununuliwi! HUMBA WATCH OUT
   
 3. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  naomba mwenye ile taarifa ya kusitishwa mkataba kati ya marie stopes na NHIF nimesikia somewhere kwenye radio sijajua ni gazeti gani.
  hawa marie stopes wamelalamikia sana ufisadi wa hawa NHIF mpaka wameshindana nao
   
 4. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2013
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,553
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  mtoa mada japo mambo au shida hizo zipo kwa muda mrefu lakini taasisi hiyo bado haijaweza kukidhi mahitaji ya wanachama wake ipasavyo hadi leo....
   
 5. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2013
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 3,320
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada umenena. Huduma kiukweli ni mbovu mno na kuna ubaguzi wa huduma jambo ambalo sikubaliani nalo. Mfano wengine wana kadi za kijani na sie wa chini kadi za brown. Kwanini wote tusipate huduma sawa as long kuwa wote tupo mfuko mmoja? Pia sheria iliyoanzisha mfuko huu inasemaje kuhusu uanachama? Je, ni wa hiari au lazima kwa wafanyakazi? Wenye kujua tujuzeni.
   
 6. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2013
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 3,320
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Kuna mambo yalofichama ndani ya mifuko hii inayoletwa na serikali bila kuwashirikisha wananchi. Mara nyingi mifuko hii ipo kisiasa zaidi na ubadhirifu unaotokea ni kwa ajili ya viongozi wa kisiasa kujichotea fedha za wanachama kwa shughuli zao za kisiasa au binafsi. Hii ni kwasababu ya uswahiba uliopo baina yao na watendaji wateule wa mifuko yao waliowaweka kwa maslahi yao binafsi. Tushtuke wanajamii kwani mifuko hii ni kwa maslahi ya wachache. Tumeliwa vya kutosha sasa, tuikatae!?
   
 7. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2013
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 3,320
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada umenena. Huduma kiukweli ni mbovu mno na kuna ubaguzi wa huduma jambo ambalo sikubaliani nalo. Mfano wengine wana kadi za kijani na sie wa chini kadi za brown. Kwanini wote tusipate huduma sawa as long kuwa wote tupo mfuko mmoja? Pia sheria iliyoanzisha mfuko huu inasemaje kuhusu uanachama? Je, ni wa hiari au lazima kwa wafanyakazi? Wenye kujua tujuzeni.
   
 8. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #8

 9. SaaMbovu

  SaaMbovu JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2013
  Joined: Oct 8, 2013
  Messages: 3,491
  Likes Received: 815
  Trophy Points: 280
  Ni zaidi ya kero
   
 10. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2013
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,553
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  nashauri shirika hili livunjwe kuwe na sehemu tatu na wale wa Serikali KUU, TAMISEMI na Jingine kwa wananchi binafsi wa kawaida wanaotaka kuchangia kwa hiari yao.
   
 11. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2013
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 3,320
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada umenena. Huduma kiukweli ni mbovu mno na kuna ubaguzi wa huduma jambo ambalo sikubaliani nalo. Mfano wengine wana kadi za kijani na sie wa chini kadi za brown. Kwanini wote tusipate huduma sawa as long kuwa wote tupo mfuko mmoja? Pia sheria iliyoanzisha mfuko huu inasemaje kuhusu uanachama? Je, ni wa hiari au lazima kwa wafanyakazi? Wenye kujua tujuzeni.
   
 12. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #12

Loading...