Elections 2010 Mfuko Maalum wa Kuchangia gharama za Kesi kwa ajili ya Majimbo tulioporwa Ushindi

Mhafidhina

JF-Expert Member
Feb 6, 2008
549
22
Wanajamii,

Kwa kweli nimesikitishwa sana kwa hali ninayoina ikiendelea kwa CHADEMA kuporwa wazi wazi tena bila huruma ushindi wa baadhi ya majimbo.

Sasa ni ushauri wangu tuanzishe mfuko maalum wa kuchangia gharama za kufungua na kuendesha kesi dhidi ya wale mafisadi waliotupora ushindi waziwazi ili haki ya wananchi isipotee bure.

Kwa taarifa nilizonazo, kufungua kesi moja ya uchaguzi inabidi ulipe kiwango cha Sh. 5,000,000/= kama deposit mahakamani of caurse huwa kuna gharama za mawakili za kuendesha kesi hizi pamoja na mashahidi ambao huwa inagharimu fedha za kuwaleta mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi. So walau kesi moja inaweza kugharimu hadi sh. 10,000,000/=.

Ni wito wangu basi tushirikiane kwa pamoja kujumuisha nguvu zetu ili tuweze kushangisha fedha walau za kukomboa majimbo manne (Segerea, Kilombero, Sumbawanga Mjini na Karagwe....!) ambayo ushindi wake ni dhahiri uligubikwa na wizi wa kimachomacho.

Pamoja tutaweza...! :israel:
 
Kesi mtafungua mwezi wa kumi na mbili mwaka huu halafu itaahirishwa kwa muda wa miaka mitano. Ikiwa imebaki miezi miwili bunge kuvunjwa ndo wataisoma hiyo kesi. Hao ndiyo CCM ndugu yangu. Nafikiri tukubaliane namna ya kuisusia serikali ya Kikwete. Au kuwaimpower hawa wabunge wachache waliopata nafasi kwenda huko kuhakikisha wanazibeba hasira zetu na kuishughulikia ipasavyo serikali ya huyu jambazi.
 
Hata mimi binafsi sina uhakika sana na suala la kwenda mahakamani. Mahakama zenyewe ni kama NEC. Mmeshasahau kesi ya Mnyika 2005 na ile ya Mch Mtikila? Watachelewesha na kuzungusha hadi 2015 itafika.
 
Nafikiri ili kudumisha amani ni bora tutumie utaratibu huu wa kutumia vyombo vyetu vya kutafutia haki. Sioni kama ni busara kusisitiza au kuchochea vurugu manake mwisho wa siku tutakao umia na kupata matatizo ni sisi wenyewe au ni ndugu na marafiki zetu pamoja na mali. Indeed gharama ya kufanya vurugu au kuchukua hatua mkononi ni kubwa kuliko hii ya kwenda mahakamani.

Tukitumia mob psychology na kuwa convince wananchi waende barabarani au wafanye CHADEMA itapoteza credibility na ndio itakua ndio mwanzo wa kujichimbia kaburi. Ni bora tukapambane huko huko mahakamani ili tuhakikishe haki inapatikana na hatimaye tupate wabunge watakaoweza kuichachafya CCM na hatimaye kuing'oa 2015.
 
Siungi kabisa mkono wazo la kuanzisha fujo. Napinga kabisa jambo hili. Lakini pia nafikiri hili la kufungua kesi na kuamini kwamba mahakama ni chombo cha sheria kitakachotenda haki kwa watanzania, hiyo kwakweli sidhani. Maana mahakama za Tanzania ni mojawapo ya taasisi za CCM kama ilivyo NEC. Hawana jipya. Tunaweza tukapoteza resources zetu na muda wetu na bado tusipate chochote. Mgombea mwenyewe akiona busara kufungua kesi, na afanye hivyo sisi tutamuunga mkono. Lakini kusema tuchangishe kwa ajili ya hilo, nafikiri ni kupoteza muda tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom