Mfuko Maalum wa Kuchangia gharama za Kesi kwa ajili ya Majimbo tulioporwa Ushindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfuko Maalum wa Kuchangia gharama za Kesi kwa ajili ya Majimbo tulioporwa Ushindi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mhafidhina, Nov 5, 2010.

 1. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wanajamii,

  Kwa kweli nimesikitishwa sana kwa hali ninayoina ikiendelea kwa CHADEMA kuporwa wazi wazi tena bila huruma ushindi wa baadhi ya majimbo.

  Sasa ni ushauri wangu tuanzishe mfuko maalum wa kuchangia gharama za kufungua na kuendesha kesi dhidi ya wale mafisadi waliotupora ushindi waziwazi ili haki ya wananchi isipotee bure.

  Kwa taarifa nilizonazo, kufungua kesi moja ya uchaguzi inabidi ulipe kiwango cha Sh. 5,000,000/= kama deposit mahakamani of caurse huwa kuna gharama za mawakili za kuendesha kesi hizi pamoja na mashahidi ambao huwa inagharimu fedha za kuwaleta mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi. So walau kesi moja inaweza kugharimu hadi sh. 10,000,000/=.

  Ni wito wangu basi tushirikiane kwa pamoja kujumuisha nguvu zetu ili tuweze kushangisha fedha walau za kukomboa majimbo manne (Segerea, Kilombero, Sumbawanga Mjini na Karagwe....!) ambayo ushindi wake ni dhahiri uligubikwa na wizi wa kimachomacho.

  Pamoja tutaweza...! :israel:
   
 2. Mfikiri

  Mfikiri JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2010
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 592
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Usisahau jimbo la SHINYANGA MJINI.........hali ni tete pale....
   
 3. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kesi mtafungua mwezi wa kumi na mbili mwaka huu halafu itaahirishwa kwa muda wa miaka mitano. Ikiwa imebaki miezi miwili bunge kuvunjwa ndo wataisoma hiyo kesi. Hao ndiyo CCM ndugu yangu. Nafikiri tukubaliane namna ya kuisusia serikali ya Kikwete. Au kuwaimpower hawa wabunge wachache waliopata nafasi kwenda huko kuhakikisha wanazibeba hasira zetu na kuishughulikia ipasavyo serikali ya huyu jambazi.
   
 4. c

  chanai JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi binafsi sina uhakika sana na suala la kwenda mahakamani. Mahakama zenyewe ni kama NEC. Mmeshasahau kesi ya Mnyika 2005 na ile ya Mch Mtikila? Watachelewesha na kuzungusha hadi 2015 itafika.
   
 5. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ili kudumisha amani ni bora tutumie utaratibu huu wa kutumia vyombo vyetu vya kutafutia haki. Sioni kama ni busara kusisitiza au kuchochea vurugu manake mwisho wa siku tutakao umia na kupata matatizo ni sisi wenyewe au ni ndugu na marafiki zetu pamoja na mali. Indeed gharama ya kufanya vurugu au kuchukua hatua mkononi ni kubwa kuliko hii ya kwenda mahakamani.

  Tukitumia mob psychology na kuwa convince wananchi waende barabarani au wafanye CHADEMA itapoteza credibility na ndio itakua ndio mwanzo wa kujichimbia kaburi. Ni bora tukapambane huko huko mahakamani ili tuhakikishe haki inapatikana na hatimaye tupate wabunge watakaoweza kuichachafya CCM na hatimaye kuing'oa 2015.
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Siungi kabisa mkono wazo la kuanzisha fujo. Napinga kabisa jambo hili. Lakini pia nafikiri hili la kufungua kesi na kuamini kwamba mahakama ni chombo cha sheria kitakachotenda haki kwa watanzania, hiyo kwakweli sidhani. Maana mahakama za Tanzania ni mojawapo ya taasisi za CCM kama ilivyo NEC. Hawana jipya. Tunaweza tukapoteza resources zetu na muda wetu na bado tusipate chochote. Mgombea mwenyewe akiona busara kufungua kesi, na afanye hivyo sisi tutamuunga mkono. Lakini kusema tuchangishe kwa ajili ya hilo, nafikiri ni kupoteza muda tu.
   
 7. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Msisahau kahama pia na Bukoba mjini na busanda wakuu.
   
 8. A

  Anaruditena Member

  #8
  Nov 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jimbo la Kibaha mjini pia
   
 9. a

  anney Senior Member

  #9
  Nov 5, 2010
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Babati vijini NCCR waliporwa kwa nguvu
   
Loading...