Mfuga Kunguru

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
EDIT2:

KWA UFUPI: Pale mjini palikuwa na binti maarufu kwa ununda. Waoaji wote walikuwa wakimkwepa, wakitaka kumposa mdogo-mtu aliyesifika kwa tabia njema. Hadithi hii ni simulizi la 'baharia' mmoja aliyejitoa muhanga kumposa binti nunda.


(Iliandikwa karne kadhaa zilizopita. Imefasiriwa na Wako—Mtiifu.)

Katarina, Nunda, alikuwa ndiye binti mkubwa wa Batista, jamaa tajiri wa Padua. Alikuwa ni binti mkorofi, nunda, mwenye kupayuka maneno makali, mpaka akajulika jijini Padua siyo tena kwa jina lingine zaidi ya Nunda Katarina.

INAENDELEA SEHEMU YA PILI
 
MFUGA KUNGURU - 2

Ndivyo ilivyoonekana ni vigumu sana, kiukweli haiwezekani, kwamba mtu yoyote mwenye heshima zake angethubutu kumuoa binti huyu, na hivyo Batista alilaumiwa sana kwa kukataa kumuoza binti yake mpole Bianka, licha ya posa za ukweli toka kwa waposaji vizito, akitumia kisingizio kwamba, pale Katarina atakapokuwa ameolewa, ndipo fursa ya kumposa Bianka itatokea.


Ilitukia, hata hivyo, kwamba jamaa mmoja, akiitwa Petro, alikuja Padua, akitafuta mke wa kumuoa, ambaye, pasipo kukatishwa tamaa na manenomaneno kuhusu kisirani cha Katarina, alidhamiria kumposa binti huyu chakaramu, na kumtuliza awe mke mwema aliye mtaratibu.

Na hakukuwa na mwingine aliye vizuri kuchukua jukumu hili zito kama Petro, ambaye ukali wake ulikuwa mkubwa kama wa Katarina, na alikuwa aliyejaa vichekesho na muda mwingi alikuwa ni mwenye furaha, akifurahisha genge, na mwingi wa busara na hekima, aliyeweza kujidai amekasirika au aliyefurahi muda wowote aliotaka kufanya hivyo, ilhal ndani yu mtulivu kiasi cha kuweza kujicheka aigizapo kukasirika, na hulka yake ikiwa ni mtu wa watu asiye na kelele wala mikwaruzo; na ubandido aliouonyesha alipomuoa Katarina ulikuwa ni kama masikhara tu, au ikielezwa sawasawa, ulitokana na busara zake, kama njia pekee aliyoiona ya kumdhibiti nunda Katarina.

Kwenye posa alienda bwana Petro kumchumbia nunda Katarina; na awali ya yote alienda kwa baba Katarina, amruhusu amsemeshe bintiye mpole Katarina, kama Petro alivyomuita, akisema kama masikhara, kwamba baada ya kusikia sifa zake za upole na tabia njema, ilimbidi asafiri toka Verona kuja kumchumbia.

Japo baba yake alitamani kumuoza binti yake, alilazimika kukiri uchakaramu wa binti yake, kwani haikuchukua duru upole wake alionao kudhihirika, kwani mwalimu wake wa muziki alifika kwa haraka sebuleni, akilalamika kwamba mwanafunzi wake mpole Katarina, amempiga kichwani kwa kutumia filimbi, baada ya mwalimu kumkosoa upigaji wake; maneno ambayo Petro alipoyasikia alisema, “yu binti jasiri; nazidi kumpenda, na natamani kusema naye kidogo;” na akimharakisha baba mzazi ampe jibu zuri, alisema, “Safari yangu ina haraka, Mzee Batista, siwezi kuja hapa kila siku kufuatilia masuala ya posa. Wamfahamu baba yangu: alishafariki, na ameniachia urithi wa ardhi yake yote na mali zake zote. Niambie kama nina ruksa ya kumuoa binti yako, masuala ya mahari yakamilishwe.”

Batista aliona posa hii imekaa kiubabe fulani kwa muoaji; lakini kwa kuwa alifurahi kumuoza Katarina, walielewana papo hapo masuala ya mahari. Hivyo, ndoa ya wawili hawa ilikubaliwa na Batista alienda kumuarifu bintiye chakaramu kuhusu muoaji, na kumruhusu akaongee na Petro mposaji.

ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom