Mfanyakazi wa Vodacom aeleza alivyochunguza Simu za Sabaya

MENEJA Ulinzi na Ushirika wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Kampuni ya Vodacom (T) Makao Makuu Dar es Salaam, James Wawenje (39), ameieleza mahakama jijini hapa kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Arusha ilimuagiza achunguze namba za simu ya kiganjani za washitakiwa watatu akiwemo alyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Wawenje ni shahidi wa sita katika kesi ya uhujumu uchumi, kuongoza genge la uhalifu na kutakatisha fedha inayomkabili Sabaya (34) na wenzake sita katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha.

Washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni (41), Watson Mwahomange (27) maarufu Malingumu, John Aweyo (45), Sylvester Nyengu (26) maarufu Kicheche ambaye ni msaidizi wa Sabaya, Jackson Macha (29) na Nathan Msuya (31).

Akiongozwa na Mwendesha Mashitaka Mwandamizi wa Serikali, Ofmen Mtenga mbele ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Patricia Kisinda, Wawenje alidai namba za simu alizokabidhiwa ni za Sabaya, Mnkeni na Macha ambazo Takukuru ilitaka taarifa zake za Julai 20, mwaka huu za kupiga, kupigiwa simu na jumbe mfupi.

Wawenje alizitaja namba hizo alizokabidhiwa na Takukuru kuwa ni namba 0758 707171 iliyosajiliwa kwa jina la Lengai Ole Sabaya, 0757 978686 iliyosajiliwa kwa jina la Enock Mnkeni na namba 0746 935569 iliyosajiliwa kwa jina la Ramweli Jackson Macha.

Alisoma nyaraka za mtandao za Vodacom zikionesha watuhumiwa Sabaya, Mnkeni na Chacha walivyokuwa katika Jiji la Arusha maeneo ya Mbauda, Sombeni, FFU Kwa Mrombo na Makao Mapya kati ya saa 8.44 mchana, saa 9.52 na saa 9.55 alasiri.

Wawenje alidai alitoa taarifa zake kwa Kamanda wa Takukuru Mkoa Arusha kama alivyotakiwa ikiwa ni pamoja na taarifa za kupiga, kupokea na ujumbe mfupi wa sms kwa tarehe iliyotajwa kwa mujibu wa sheria ya nchi.

Pia alikabidhi mahakamani nyaraka ya barua kutoka Takukuru kwenda Vodacom kama ushahidi katika kesi hiyo na upande wa utetezi haukuwa na pingamizi kuhusu nyaraka hiyo.
Mungu akubariki bwana Hamduni.
Kamanda wa TAKUKURU hakika unalishughulikia hili jambazi
 
Nauliza tu, sitetei uhalifu!!

Mashirika ya simu hayana privacy kwa wateja wao, kama mitandao ya nchi nyingine i.e USA etc?
Privacy? umesoma sheria na kuzielewa? duniani kote serikali inapotaka taarifa za mtu fulani wanaemshuku huwa wanapatiwa iwe kampuni ya simu, bank n.k
 
Back
Top Bottom