wazungu wana ishu za race damuni
Hata Waafrika/Watanzania - undugu, ukabila, udini.
wazungu wana ishu za race damuni
Hivi askari wa JWTZ waliompiga traffic kwa kuchelewesha kuruhusu gari lao lipite pale Ubungo (Traffic Lights) miezi michahce iliyopita nao walishikiliwa na polisi au walikuwa kazini?
Hapa Tanzania kuna udhalilishaji mwingi ila ukifanywa na watu fulani ndio unaonekana kuwa mbaya. Mfano, 'former inmate' mmoja alikuwa anasimulia jinsi wanavyodhalilishwa jela eti kwa vile ni wafungwa. Alisema kwa muda ambao amekaa huko walikuwa wakirushwa kichura wakiwa uchi 'at least' mara tatu kwa wiki.
Alichokifanya huyo njemba (Mkanada) ni kibaya na vilevile udhalilishaji mwingine unaofanywa na Watanzania wenzetu ni mbaya pia ila unakuwa kama unafumbiwa macho.
Magobe umenena, hivi tunapiga kelele sana shauri huyu mama ni mzungu au shauri ya tendo lake???? Mmachinga anapopigwa na askari mpaka kuachwa uchi wakati anafanya biashara ya kujikimu yeye na familia yake hatusemi.
Dawa zinapoibiwa hospitali kimchoro na wagonjwa kukosa dawa, je huo sio udhalilishaji, tena huo ni uuaji, tunaangalia tu na kucheka.
Mtu akifanya mchoro na kuleta mitambo ya umeme isiyofaa na kulipwa mahela kibao na kuacha mamia hawana umeme na yeye kuendelea kufaidi, huo sio udhalilishaji. Wala hatupigi kelele.
Kampuni ikipewa ardhi kuchimba madini na nchi kupata 3% twaona ni sawa tu sio udhalilishaji, tunafurahi wala hatusemi.
Wagapi miongoni mwetu tunatukana mahouseboy, mahousegirl, walinzi madereva na mashambaboy, je huo sio udhalilishaji. Tunawachapa viboko, tunawamwagia maji ya moto, tunawachoma na vijinga vya moto, je hivyo vyote sio udhalilishaji shauri vitendo hivyo tunafanyiana watanzania kwa watanzia ndio maana hatulalamiki.
Wangapi miongoni mwetu wana chakula cha ziada na wanansahau kuwa wengine hawana hata chakula, na hicho chakula cha ziada kimetokana na rasilimali za yule ambaye hana, hatusemi, tunakaa kimya tu au shauri ni ngozi nyeusi imefanya hivyo basi huo sio udhalilishaji?????
Wangapi wapo kwenye baridi kali na hawana nguo za kuvaa ( hata mitumba) na sisi tunashindana kuvaa nguo za gharama, kutokana na jasho lao wenyewe.
Ndugu zangu tuamke kama tuko serious udhalilishaji Tanzania uko kila sehemu kuanzia miongoni mwetu, tusiwe na jazba kwa ajili ya rangi au utaifa.
Tutoe vibanzi kwenye macho yetu kwanza.

Ushahidi wa mate kwenye fulana na Jerry utakuwepo kweli baada ya masaa machache!?
hivi kafukuzwa kweli au? manake you never know bwana labda yupoKiutaratibu, hakupaswa hata kupelekwa polisi, badala yake alipaswa kupewa 24 hours notice ya kuondoka nchini kama ambavyo wao wanatufanyia tukiwa nchini kwao. Nitaishangaa serikali kama itamchekea, au itaanza kumfungulia mashitaka mahakamani yasiyokuwa na mwelekeo. Afukuzwe!
Klinton Raisi mstaafu wa Marekani yalikutwa manii yake kwenye nguo ya Monica Lewinsk miezi kibao baada ya manii yale kuangukia kwenye nguo ambao Monika aliitunza nguo hiyo, walipochunguza wakathibitisha kwamba ni kweli ni manii yake Clinton. Hata mate hayo yataangaliwa DNA yake na kulinganishwa na mtuhumiwa na wakemia. Afterall, fulana iliyotemewa mate ndiyo iliyohifadhiwa na wala sio mate. Wakitaka wangeweza kuyatunza mate hayo pia kwa uchunguzi zaidi. Tanzania nao wamo bwana.
Leka
Hii kitu imenikumbusha mwaka jana Wachina pame Shekilango kituoni walimpiga kijana mmoja wa vodacom kama waniga nyoka watanzania wamesimama . Maana wachina walileta shida kubwa sana lakini kosa lilikuwa lao . Mie nikaoga game lote nikaenda polisi nikawabeba na gari langu . Kufika pale kumbe aliye anzisha fujo ndiye mkuu wao mwenye garage pale wakaanza zao . Basi ikabidi tuingie kazini . Mkuu yule alilala ndani na akawekwa karibu na choo na pekee yake maana jamaa wa ndani walitaka kumgombania . Usiku wachina wakabena 500,000 na kumpeleka kibarua mchina kwamba aingie ndani on behalf of his boss . Tukawa makini ili kutoa heshima .Kituoni paliwaka moto jamaa akalala hadi kesho yake saa 7 mchana kwa kosa lile akalipa dola 1000 kesi ikiahsa lakini kalala .Maana alimshambulia kijana wa watu ile mbaya .Na huyu ma Canada anafanya haya anajua Barrick yao nk sl haoni shida .
It is a shame hakika kudharauliwa namna hii .
Huyu mama msimlaumu sana, inawezekana alikuwa ana mimba changa!
http://www.cbc.ca/canada/ottawa/story/2009/12/11/cdn-diplomat-spitting.html?ref=rss#socialcomments
tazameni wakanada wanavyotufikiria..,a bit relieved there are fair minded,BUT some are almost approving their country-mate's behavior