Mfanyakazi wa tiGo afariki dunia baada ya kunywa mizinga mitano ya konyagi wakati akishindana kunywa

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,059
2,000
Shinyanga, Tanzania — Katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyakazi mmoja wa kampuni ya simu za mkononi ya TIGO mkoani Shinyanga amekufa papo hapo baada ya kudaiwa kunywa pombe nyingi aina ya Konyagi kupita kiasi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamemtaja mfanyakazi huyo kuwa ni Godi Mangala (34) aliyekuwa akiishi mtaa wa Majengo mapya kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga ambapo tukio hilo limetokea juzi saa moja usiku wakati wa sikukuu ya Krismas.

Mashuhuda hao wamewaeleza waandishi wa habari mjini kwamba siku hiyo ya tukio, Godi akiwa na marafiki zake katika moja ya grocery za mjini humo waliamua kupata vinywaji ambapo waliamua kunywa pombe hiyo kwa kushindana ili kuweza kumpata bingwa wa utumiaji wa kilevi hicho.


Walisema muda mfupi baada ya marehemu kuonesha ubingwa wake katika unywaji wa pombe hiyo alionesha dalili za kuzidiwa na kuishiwa nguvu hali ambayo ilisababisha rafiki zake wamtafutie usafiri na kumrudisha nyumbani kwake ili apumzike: “Hata hivyo tulipoona hali yake inaendelea kuwa mbaya tulichukua uamuzi wa kumkimbiza katika hospitali ya serikali mkoani Shinyanga ili aweze kupatiwa matibabu haraka lakini hata hivyo alifariki dunia kabla ya kufikishwa hospitali,” alieleza mmoja wa marafiki wa marehemu ambaye hata hivyo hakupenda kutajwa jina gazetini.

Kwa upande wake John Maganya ambaye pia ni mmoja wa marafiki wa marehemu alielezea kushitushwa kwake na tukio hilo ambalo limesababisha kifo cha rafiki yake ambaye hata hivyo alisema enzi za uhai alikuwa ni mzoefu katika unywaji wa pombe japokuwa kuna wakati alikuwa akizimia na kuzinduka: “Nimeshitushwa na kifo cha rafiki yangu, kwani kama ni pombe mbona alikuwa mzoefu, nafikiri hii Konyagi aliyokuwa anakunywa na wenzake imesababisha kifo chake, maana tumeelezwa kwamba alikunywa mizinga mitano kwa mkupuo, ni hatari,” alieleza Maganya.

Kwa upande wake mganga mfawidhi katika hospitali ya serikali mkoani Shinyanga, Dkt. Fredrick Mlekwa alikiri kupokea mwili wa marehemu huyo juzi mnamo saa moja usiku na kwamba baada ya kuchunguzwa na kubainika tayari ameishafariki alielekeza mwili huo ukahifadhiwe katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alisema hakuwa na taarifa juu ya tukio hilo na kwamba huenda ndugu wa marehemu hawakuona umuhimu wa kutoa taarifa polisi ya kifo cha ndugu yao.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana mjini hapa, tayari ndugu wa marehemu waliuchukua mwili wake na kupelekwa jijini Mwanza eneo la Mabatini ambako ulitarajiwa kuzikwa leo mchana (Jumamosi). ---
 

Pukudu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
3,133
2,000
Huyu mshikaji namfahamu sana kilichomcost ni kupenda sifa... Alitaka aonekane mkali ona Sasa anaenda zikwa hata mwaka hajauona
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,809
2,000
Apumzishwe anakostahili. Sipati picha maongezi ya kwenye familia wakati wa maziko. Kweli mwana -------- ni mzigo wa *****
 

Sunshow

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
1,139
1,500
Inasikitisha mtu mwenye elimu kufanya mambo ya ovyo ovyo. Hivi hakujua kuwa kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako?
 

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
7,371
2,000
Konyagi mizinga mtano loh, nakumbuka nilishakunywa mmoja nilihisi natapika maini yangu loh.

Ni kinywaji nachokiheshinu sana
 

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,281
2,000
Pole mkali wa nyagi zinga 5 aaah lazima uvute man pumzika kwa amani
 

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,707
1,225
Mashindani ya kijinga sku zote hutoa athari za kijinga!
Wenzetu wanashindana kuvumbua, eti sisi tunashindana kunywa mipombe!!!!!
 

Jajani

Senior Member
Oct 13, 2012
137
0
Ukweli, elimu ya marehemu Na kupenda sifa zilizopinda ni hatari.
Akalazwe huko anakoenda
 

feswane

New Member
Dec 30, 2013
4
20
Polen sana wafiwa. Na ni onyo kwa wengine tusipende kuiga mambo ya kijinga tunamrahisishia kazi Israel
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
17,253
2,000
SLAVE - LUCKY DUBE
Ministers of religion

have visited me many times
to talk about it
They say to me
I gotta leave it I gotta leave it
It's a bad habit
for a man
But when I try to leave it
my friends keep telling me
I'm a fool amongst fools

Chorus:
Now I'm a slave, a slave
I'm a slave
I'm a liquor slave
I'm a slave, a slave, slave
I'm a slave
Just a liquor slave


I have lost my dignity
I had before trying
to please everybody
Some say to me
yo yo
I look better when I'm drunk
Some say no no no
I look bad you know
Sometimes I cry
I cry but my crying
never helps me none


Chorus:
'Cos now I am a slave, a slave
I'm a slave
I'm just a liquor slave
I am a slave, a prisoner
I'm a slave
Just a liquor slave


Every night when I'm
coming back home
My wife gets worried
'cos she knows
Shes got double trouble
coming home
Sometimes I cry
I cry lord I cry
But my crying
never helps me


Chorus: (till fade)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom