Mfanyakazi wa Tanesco Arusha, Ombeni Alfayo amkata mkewe kiganja cha mkono kwa sime

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
670
1,000
Mtuhumiwa amekamatwa akiwa Jijini Dar es Salaam alikokimbilia

Mkewe ambaye ni Mwalimu wa Sekondari ya Kirenyi Arusha amelazwa Hospitali ya Selian Arusha kwa matibabu

Madaktari wanasema anaendelea vema japo Kiganja cha Mkono wake wa kulia kimetengana na viungo vingine vya mwili

Mungu amponye na ampe wepesi

hamduni%20ed.jpg

===

Mfanyakazi wa shirika la umeme Tanesco jijini Dar es salaam Ombeni Alfayo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kitendo kukata mkono mkewe na kusababisha kiganja Cha mkono wa kulia kutengana na sehemu nyingine ya mkono.

Akiongeza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni Alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya Saa 5:45 asubuhi maeneo ya siwandeti ,Iliopo kata ya Kiranyi Tarafa ya Enaboishu wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha Ambapo alimkata mke wake Veronica Kidemi (30) mmasai na mwalimu wa shule ya sekondari Kiranyi na mkazi wa siwandeti ambapo alimjeruhi kwa kumkata na kitu chenye ncha Kali katika mikono yake miwili.

Alisema kuwa uchunguzi unaendelea Ili kubaini chanzo Cha tukio hilo ingawa taarifa za awali zinasema kuwa chanzo Ni wivu wa kimapenzi ,ambapo aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikimbia Mara Baada ya kufanya tukio hilo na tayari ameshakamatwa katika jiji la Dar es salaam Mara Baada ya upelelezi kukamilika na atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria aidha pia majeruhi amelazwa katika hospital ya selian-ngaramtoni.

Akiongelea tukio hilo mwalimu huyo Veronica Kidemi Alisema kuwa mume wake huyo alikuwa anamtishia Mara kwa Mara ,na alikuwa akimpiga Mara kwa Mara na inatokana na wivu alionao mume wake.

“Aliniita kutokea kazini nikaenda nilipotoka nikamkuta amejificha jikoni ndio akaanza kunikimbiza na kunikatakata mapanga hapa unapoona mkono unaniuma huu mmoja na huu mungine nimewekewa chuma ” Veronica

Kwa upande wake daktari bigwa wa mifupa wa hospital Seliani Robert Julius amethibitisha kumpokea akiwa anavuja damu nyingi na wakaanza kumpatia matibabu na kwa sasa anaendelea vizuri.
 
quier

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
364
1,000
Mwaka huu uishe tu 😏😏 pole kwa mke na pole nyingi kwa mtuhumiwa. Ushauri binafsi: Ukiona kina ni kirefu toka kwenye maji using'ang'anie kubaki madhara huwa ni makubwa.

Kwa sasa ndoa sio kitu Cha kujivunia kabisa watu tunalala jicho moja likiwa wazi Mana hatujui wenza wetu wanatuwazia nini muda huo
 
Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
3,229
2,000
Embu waza ingekuwa mume ndo amekatwa korodani/kende...." ka utamu tukose woteee"

Utakuta changamoto zilianza ndogo/kidogo kidogo, zika lundikana na kujaza kikombe.

Hili fumbo la kuishi na mwenza ndani ya nyumba ni zaidi ya tuwazavyo/tujuavyoooo.

Bwana akatufanyie wepesi tuweze kusoma na kuelewa, kutizama na kuona, kusikiliza na kusikia, kadiri ya maandiko [vitabu vitakatifu]
 
Kilimbatz

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
301
250
Amekamatwa akiwa Dar es Salaam alikokimbilia

Mkewe ambaye ni Mwalimu amelazwa Hospitali ya Selian Arusha kwa matibabu

Madaktari wanasema anaendelea vema japo Kiganja Cha Mkono wa kulia

View attachment 1585447

===

Mfanyakazi wa shirika la umeme Tanesco jijini Dar es salaam Ombeni Alfayo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kitendo kukata mkono mkewe na kusababisha kiganja Cha mkono wa kulia kutengana na sehemu nyingine ya mkono.

Akiongeza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni Alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya Saa 5:45 asubuhi maeneo ya siwandeti ,Iliopo kata ya Kiranyi Tarafa ya Enaboishu wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha Ambapo alimkata mke wake Veronica Kidemi (30) mmasai na mwalimu wa shule ya sekondari Kiranyi na mkazi wa siwandeti ambapo alimjeruhi kwa kumkata na kitu chenye ncha Kali katika mikono yake miwili.

Alisema kuwa uchunguzi unaendelea Ili kubaini chanzo Cha tukio hilo ingawa taarifa za awali zinasema kuwa chanzo Ni wivu wa kimapenzi ,ambapo aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikimbia Mara Baada ya kufanya tukio hilo na tayari ameshakamatwa katika jiji la Dar es salaam Mara Baada ya upelelezi kukamilika na atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria aidha pia majeruhi amelazwa katika hospital ya selian-ngaramtoni.

Akiongelea tukio hilo mwalimu huyo Veronica Kidemi Alisema kuwa mume wake huyo alikuwa anamtishia Mara kwa Mara ,na alikuwa akimpiga Mara kwa Mara na inatokana na wivu alionao mume wake.

“Aliniita kutokea kazini nikaenda nilipotoka nikamkuta amejificha jikoni ndio akaanza kunikimbiza na kunikatakata mapanga hapa unapoona mkono unaniuma huu mmoja na huu mungine nimewekewa chuma ” Veronica

Kwa upande wake daktari bigwa wa mifupa wa hospital Seliani Robert Julius amethibitisha kumpokea akiwa anavuja damu nyingi na wakaanza kumpatia matibabu na kwa sasa anaendelea vizuri.
Ndoa za kikristo zina changamoto sana,kile kipengere cha mpaka umauti kinawatesa wengi sana,unamchoka mtu kumwacha haiwezekani,mambo kama huwezi kuyakuta kwenye ndoa za kiislamu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom