Mfanyakazi wa Serikali mmoja huku Idukilo kasema kwa masikitiko bado anatumia mshahara wa enzi za Kikwete

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
219
500
Ameongea kwa masikitiko sana sana kuwa ameshindwa kutoa rejesho la mkopo niliomkopesha wa shilingi laki 3 kwa sababu mshahara anaoutumia mpaka sasa ni wa wakati wa JK haujapanda na wakati maisha yamekuwa magumu mno.

Nikamwambia lkn vipi mbona watoto wenu wanasoma bure, huoni kama mmesaidiwa? Akanijibu "bora basi hata wkt ule tulikuwaga tukitoaga fedha kidogo za ada kwa watoto lakini fedha tulikuwaga tukizipataga mtaani kiurahisi. Kila ulichokuwa unakifanyaga kinakupatia fedha, kila mwaka angalau kamshahara kanapanda sasa kipindi hiki hakunaga kupanda kwa mshahara na nasikia fedha zote siku hizi zinatunzwa Benki Kubwa na hamna mzunguko kabisa".

Mhhh nikashangaa halafu nikamchomekea tena anilipe tu kwa sababu mume wake amestaafu Septemba mwaka jana na aliniambia mume wake akipata pensheni yake atanilipa mara moja na tangu amekopa ni miezi mitatu sasa na riba inapanda.

Alivyonijibu sasa:
"Iiiiiiii we ngosha wewe nivumiliage tu baba hajapataga pensheni mpaka sasa, hata ile ya mwezi hapati na anategemea toka kwangu akitaka kwenda kukaa na wenzake jioni pale kijiweni, mimi nitakulipaga tu hata riba ikifikia laki 3 nitatoaga tu Ngosha"

Ameniacha natafakari na kama mwezi huu atakuwa hajanilipa nitaenda kujifariji bar kwa kulewa tila lila kwani marejesho ya mikopo yameshuka sana toka kwa watendaji wa Government
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,077
2,000
Sawa kabisa hata angefanyia wa Nyerere, aongezwe Mshahara kwa ufanisi gani?
 

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
4,879
2,000
Haijawahi kutokea uongozi wa dhulma kama huu. Madai mengi ya wafanyakazi,madaraja, nyongeza za mishahara ni kama vile uamuzi wa mtu na sio sheria. Akupe asikupe ni hiyari yake
 
Top Bottom