BASHADA
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 513
- 148
Wana JF, naomba ushauri wenu huyu binti niliye naye story yake inasikitisha sana, mpaka wakati mwingine inaniliza.
Kama mjuavyo maisha yetu haya ya Mr & Mrs kuwahi maofisini lazima utafute msichana wa kazi. Kwa kuanzia, mke wangu alitafuta msichana ambaye ni ndugu kwa upande wa kwao lakini tumeona ni pasua kichwa. Baadaye tukaamua kutafuta binti mwingine kupitia kwa ndugu wengine. Kuna dada akatuambia yeye ana wasichana wawili, kwa hiyo kama tuko tayari atatupatia mmoja, na kwa kweli tulishukuru, huyo binti akaletwa.
Ili kujua undani wake nikapeleleza maisha yake ili nisije nikauziwa mbuzi kwenye gunia. Katika kupiga naye story, nikagundua kuna maswali nikimuuliza, especially kuhusu familia yake binti akawa hanipi majibu, na kwa baadhi ya maswali aliishia kulia tuu. Nikaona ngoja nimuache nifanye upelelezi kwa namna nyingine. Nikampigia huyo dada aliyekuwa naye, na baadaye nikatafuta namba ya simu ya mtu aliyemuunganisha na huyo dada. Kwa sababu huyo mtu (pia ni relative wetu) anakaa jirani na familia ya binti, nikajua nitapata data kamili. Na niligundua mambo yafuatayo;
Majuma machache tangu binti afike kwangu, huyo mama akapata namba zake, akamwambia arudi nyumbani kwa sababu shuleni wanamsumbua anatakiwa arudi shule (kwa kuanzia alaikuwa anatumia lugha nzuri). Nikachukua jukumu la kufanya tena research kujua undani wa hilo jambo, na kama ni kweli nilikuwa tayari kumrudisha. Ikumbukwe kuwa binti wakati anawasiliana na mama alidanganya alipo. alitaja mkoa mwingine wa mbali kabisa kumbe yeye yuko kwingine.
Utafiti wangu ukabaini kuwa hakuna cha shule wala nini, kwa sababu hata wadogo zake na binti pia walishaachishwa shule na ni mwendo wa kazi za nyumbani kwa kwenda mbele. Binti alipoona vile akamwambia ataenda lakini siyo haraka hivyo. Mama akakasirika na kuanza kuporomosha matusi ya ajabu ambayo siwezi kuyaandika hapa. Mwisho wa story, akaaga kwa maneno haya "Nahesabu kuwa umekufa, Bwana alitoa na Bwana ametoa, Jina la Bwana na libarikiwe. Nisikuone ukija kwangu kwa mema au kwa mabaya, ikiwa ni kwa uzima au ni kwa kifo, huyo uliye naye atajua kila kitu"
Huyo mama ametuma sms nyingi za vitisho na laana, lakini binti anasema mbona hayo siyo matusi, ni cha mtoto ukilinganisha na matusi aliyokuwa anapewa na mateso siku za nyuma. Binti ameapa hatorudi tena. Yuko much more comfortable kukaa kwangu, anapenda sana watoto, ni mchapa kazi mpaka utafurahi. Changamoto mbele yangu naomba ushauri wa mambo yafuatayo;

- Binti aliacha shule akiwa form two na sasa alitakiwa kuwa form three (off course hili hata binti mwenyewe aliniambia.
- Binti hana wazazi wote wawili, japo yeye hajui hilo. Wazazi wake walifariki yeye akiwa mdogo sana, hivyo alikabidhiwa kwa ndugu mwingine wa kike (bila shaka ni mama mdogo). Binti amekua akijua yule ndiye mama yake mpaka leo anajua hivyo.
- Binti kila akimwuliza huyo mama kuhusu alipo baba yake, huishia kupigwa, matusi na vitisho vingine.
- Binti aliachishwa shule na mama yake na kuishia kufanyishwa kila aina ya kazi (ilikuwa ni mateso). Kwa sababu ya hayo mateso, binti alishawahi kunywa sumu ili afe, lakini aliwahiwa matibabu na akapona.
- Mama huyo yuko na mwanaume mwingine (baba wa kambo wa binti) ambaye alikuwa hajali maisha ya binti.
- Binti alipoona mateso yanazidi pale nyumbani aliamua kutoroka, ndipo alipofika kwa huyo dada ambaye ameamua kumforward kwangu.
Majuma machache tangu binti afike kwangu, huyo mama akapata namba zake, akamwambia arudi nyumbani kwa sababu shuleni wanamsumbua anatakiwa arudi shule (kwa kuanzia alaikuwa anatumia lugha nzuri). Nikachukua jukumu la kufanya tena research kujua undani wa hilo jambo, na kama ni kweli nilikuwa tayari kumrudisha. Ikumbukwe kuwa binti wakati anawasiliana na mama alidanganya alipo. alitaja mkoa mwingine wa mbali kabisa kumbe yeye yuko kwingine.
Utafiti wangu ukabaini kuwa hakuna cha shule wala nini, kwa sababu hata wadogo zake na binti pia walishaachishwa shule na ni mwendo wa kazi za nyumbani kwa kwenda mbele. Binti alipoona vile akamwambia ataenda lakini siyo haraka hivyo. Mama akakasirika na kuanza kuporomosha matusi ya ajabu ambayo siwezi kuyaandika hapa. Mwisho wa story, akaaga kwa maneno haya "Nahesabu kuwa umekufa, Bwana alitoa na Bwana ametoa, Jina la Bwana na libarikiwe. Nisikuone ukija kwangu kwa mema au kwa mabaya, ikiwa ni kwa uzima au ni kwa kifo, huyo uliye naye atajua kila kitu"
Huyo mama ametuma sms nyingi za vitisho na laana, lakini binti anasema mbona hayo siyo matusi, ni cha mtoto ukilinganisha na matusi aliyokuwa anapewa na mateso siku za nyuma. Binti ameapa hatorudi tena. Yuko much more comfortable kukaa kwangu, anapenda sana watoto, ni mchapa kazi mpaka utafurahi. Changamoto mbele yangu naomba ushauri wa mambo yafuatayo;
- Analilia kwenda shule ndiyo njozi yake kuu. Na mimi natamani aende shule lakini uwezo si mkubwa kivile. Ningependa aende shule ambayo iko serious kidogo, sitaki st. Kayumba, ila hizo shule ambazo walau atatoka vizuri ziko expensive and i may not afford now. Naweza kumhakikishia uniform za shule, pocket money, chakula na matibabu. Lakini ada kwa sasa sitaweza, naomba ushauri wenu nifanyeje? maana asiposoma hana amani.
- Pili, ishu ya wazazi wake kuwa walifariki tena kwa ugonjwa huu wa sasa (ngoma), lakini yeye alifanyiwa check up na dada aliyemchukua hana tatizo (yuko salama). Sometimes binti ana wasiwasi kama yule ni mama yake kwa jinsi anavyomtreat.
- Please, changamoto ni nyingi naomba ushauri wenu nimsaidiaje huyu binti? Especially shule, angepatikana mtu au taasisi itakayoweza kumlipia ada, hizo gharama zingine ningempatia, maana ananichukulia kama mzazi/mlezi wake na amesema hatathubutu kuondoka kwangu.