Mfanyakazi wa ndani amuua tajiri yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyakazi wa ndani amuua tajiri yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndibalema, Jun 19, 2010.

 1. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mtu mmoja aliyejulika kwa jina la Ritha Mrema (48) mkazi wa njiro amefariki dunia mara baada ya kupigwa risasi na mfanyakazi wake wa ndani katika paji la uso.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi wa mkoani hapa Basilio Matei wakati akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa tukio hilo lilitokea June 17 majira ya usiku katika eneo la Njiro Block F ambapo ambapo mtuhumiwa Omary Ally (18) alimpiga risasi tajiri yake ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Njiro.

  Kamanda amesema kuwa wakati walipokuwa wakimuhoji mtuhumiwa alisema kuwa ilikuwa ni majira ya usiku katika nyumbani kwao walisikia kishindo cha wezi wakivunja ili kuaingia ndani, ndipo marehemu akaignia ndani na kuchukua bastola na kumpa mfanyakazi wake huyo wa ndani aitumie.

  Alisema kuwa mara baada ya kukabithiwa kijana huyo wakati alipokuwa ana jiandaa kwa ajili ya kukabiliana na wezi hao ndipo alipo jikuta amempiga tajiri yake .

  "kijana huyu alikuwa hajui kutumia silaha. Sasa mara baada ya kukabidhiwa na tajiri bastola hiyo wakati akiikoki badala ya kuwageuzia wale wezi alikosea na kumgeuzia tajiri yake na kumpiga katika paji la uso"alisema Kamanda Matei.

  Basilio alisema kuwa wakati tukio hilo likitokea mume wa marehemu alikuwa hayupo na ilisemekana kuwa alikuwa amesafiri kibiashara kwenda nje ya nchi na alimuachia mkewe silaha hiyo kwa ajili kujilinda. Alisema kumuachia mtu silaha unayomiliki kihalali ni kinyume cha sheria ya umiliki wa silaha kutokana na mwanamke huyo kutokuwa na ujuzi pamoja na leseni ya kutumia silaha hiyo.

  Aidha kamanda alisema mtuhumiwa mpaka sasa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi hapo uchunguzi utakapo kamilika na kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu shitaka, bila shaka la kuua bila kukusudia


  SOURCE: MICHUZI BLOGSPOT.
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ndibalema Heshima Mbele.

  Naomba kuliweka suala hili sawa.Mume wa Marehemu Mzee Komba hakumwachia mke wake silaha bali aliacha nyumba [chumbani] mahali ambako mke wake alikuwa akipajua.Mzee Komba ni mfanyabiashara anaesafiri nje ya nchi mar kwa mara si rahisi kusafiri na silaha kunakuwa na taratibu nyingi za kirasimu zinazomzuia mtu kusafiri na silaha.

  Mzee Komba ni jirani yangu kabisa bado hajarudi sasa sijui maelezo ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha kayatoa wapi ?.
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  duniA IMEHARIBIKA..................tuendako siko tulikokusudia.........unyama unyama............undava undava............no huruma to each other.........tuombe God atusaidie kwani dudumtu kesha ingia mioyoni mwa watu
   
 4. valex

  valex Member

  #4
  Jun 19, 2010
  Joined: Jun 18, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh maskin mama wa watu lakin ni somo hili kwa wamiliki wa mabomba hasa mikoa ya kaskazini maana hata ukienda arusha umekaa bar utaona watu wanafunuliana mashati yaani wakioneshana mabomba viunoni mwao
  valex
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hii kweli? Sijatembelea sehemu hizo miaka. nashukuru kwa kutujulisha.
   
 6. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Kijana ameua kwa bahati mbaya... Nategemea, watamuhurumia... maskini

  Roho ya Marehemu ilale Mahali Pema Peponi
   
Loading...