Mfanyakazi wa Bodi ya Mikopo akamatwa kwa kuingiza Majina hewa na kujipatia ulaji mil 91

Duh kweli za mwizi arobaini. Huyu dada ni mtu wa mishemishe sana mwaka juzi nilikutana nae alikua anajenga nyumba mbezi beach, huu mchezo hajaanza leo.
 
KWAHALI HII WATOTO WAMASKINI WATAPATA MIKOPO KWELI?

Mfanyakazi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Esther Budili, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka 10 ikiwemo kughushi majina ya wanafunzi na wizi wa Sh. Milioni 90.7 mali bodi hiyo.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Bingi Mashabala.
Wakili wa Serikali Frida Mwela alidai kuwa kati ya Agosti 5 mwaka 2010 na Aprili 24, mwaka 2011, katika ofisi za Bodi hiyo zilizopo Msasani Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alighushi majina ya John Suzane, Peter Bahati, Mombo Kazim Yusuph, Bitaliho Lidya Gordian, Kwangaya Ibrahim, Majaliwa Nandu, Mtitu Catheline, Happy Alfred, Simon Isack P., Juliana J.W. Nyangige, ili waingizwe kwenye orodha ya kulipwa mkopo kupitia Chuo Kikuu cha Tiba Bugando Mwanza.
Shitala la pili, tarehe za tukio la kwanza, mshtakiwa huyo anadaiwa kughushi majina ya Catheline O. John Nkya, John S. Nkyaa, Andrew John, Goliama Hamza Ally, Simon Pamela, Gaash Ester Damian, Suzane John na kuingiza kwenye orodha ya kupewa mkopo kupitia Chuo Kikuu Cha Uhandisi akionyesha ni wanafunzi wa chuo hicho huku akijua sio kweli.
Mwela alidai kuwa shitaka la tatu, tarehe hizo mshtakiwa huyo alighushi majina ya Suzane John, Mella Boniface Christopher, Zake Ezra, Goliana Hamza Ally, Simon P. Michael, Peter Bahati Massawe, Naruo Peter, Pamela Simon, Catheline Nkyaa na kuingizwa kwenye orodha ya kupewa mkopo kupitia Taasisi ya Mafunzo ya Maendeleo akionyesha kuwa ni wanafunzi wa chuo hicho huku akijua sio kweli.
Katika shitaka la nne, ilidaiwa kuwa tarehe hizo, katika ofisi za bodi hiyo, mshtakiwa huyo alighushi majina ya Pamela Simon N., Munisi Grace na Hamza Ally Goliama, na kuingizwa kwenye orodha ya kupewa mkopo kupitia Chuo Kikuu cha Ualimu (DUCE) akionyesha kuwa wanafunzi wa chuo hicho huku akijua sio kweli.
Shitaka la tano, tarehe hizo , mshtakiwa alighushi majina ya Pamela Simon, John Suzan, Alfred Happyness, Wambura N. Juliana, John Andrew, Andrew J. Nkyaa, Hamza Y. Golima na Suzane John na kuingizwa kwenye orodha ya kupewa mikopo kupitia Taasisi ya Ustawi wa Jamii akionyesha kuwa ni wanafunzi wa chuo hicho huku akijua ni uongo.
Wakili huyo wa serikali aliendelea kudai kuwa, katika shitaka la sita mshtakiwa huyo alighushi majina ya Peter D. Naruo, Simon P. Nkyaa na Pamela Simon na kuingizwa kwenye orodha ya kulipwa mkopo kupitia Chuo cha Tiba Kilimanjaro (KCMC) akionyesha kuwa ni wanafunzi wa chuo hicho.
Katika shitaka la saba, ilidaiwa kuwa tarehe hizo na katika ofisi hizo mshtakiwa huyo alighushi majina ya Pamela Nkyaa, John Andrew Nkyaa, Simon Pamela Andrew, Pamela Simon Michael, Ester A. Goashi, Ester G. Damian, Daudi Ester, Adiambula Ester, Peter Bahati N., Naruo Peter na Suzane N. John na kuingizwa kwenye orodha ya kulipwa mkopo kupitia Chuo Kikuu Mzumbe akionyesha kuwa ni wanafunzi wa chuo hicho.
Shitaka la nane, ilidaiwa kuwa mshitakiwa alighushi majina ya Hamza Ally Goliama, Ester Lissu, Kalinga Ester, Alfred O. Happy, Andrew John, Pamely Simwel Michael, John Nkywimba, Pamela Simon N., Suzane Nkya, John Nkumba, Catheline O. John, Simon P. Nkyaa, Adia Elisha, Suzane John, Naruo Peter D., Ester Lucus na Adiambo Delinja na kuingizwa kwenye orodha ya kulipwa mkopo kupitia Chuo Kikuu Tumaini Makumira akionyesha kuwa ni wanafunzi wa chuo hicho huku akijua ni uongo.
Upande wa utetezi katika shitaka la tisa, ulidai tarehe hizo na katika ofisi hizo, mshitakiwa alighushi majina ya Wambura Juliana N., John Suzane Michael, Pamela Simon, Makinda Harison Jordan, Bumba Helfrid, Mombo Kazimi, Ally Hamza, Alfred Happy, Nkyaa Suzane M., Paul Peter Naruo, Michael Pamela S., Bahati Peter, Dismas A. Ester, Lilian Victor, John Sukamule, Diambo Mbudala, Pamela John, Suzane John, Anorld Ester Bulili, John Suzane, Simon N. Pamela, Catheline O. Nkyaa, Damas Ester na Simon Suzane Ngonyani waliingizwa kwenye orodha ya kulipwa mkopo kupitia Chuo Kikuu Ruaha akionyesha kuwa ni wanafunzi wa chuo hicho huku akijua sio kweli.
Katika shitaka la 10, mshitakiwa anadaiwa kuwa katika tarehe hizo na ofisi za bodi hiyo, akiwa mtumishi na mwajiriwa wa bodi aliiba Sh 90,775,800 mali ya bodi hiyo.
Mshitakiwa huyo alikana mashtaka hayo na kuachiwa baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaowasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh. milioni 45 au kutoa fedha taslimu.
Kesi hiyo itatajwa tena Februari 7, mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE
 
jiulizeni sasa huyu ni mmoja tu
wangapi wameiga kwenye vyeo vya juu na majina ya wangapi yameingizwa pengine na mwanao ameingizwa na ameshalipiwa vyuoni miaka mitatu we unachakachalika aende chuoni ...hizi ndio laana za watanzania lakini nawaambia ayuko pekee na hata ukiuliza vizuri kilichomsibu huyu binti aunguzwe alichomoa kugawa million 45 kwenye uongozi wa juu hii ni mekudokeza tu fwatilia mwenyewe na pengine atatufungua kwa ni navyojua wale njaa mahakimu wala akuna kesi hapo
 
hivi mkulo atakuwa anapiga mabilioni mangapi kama huyu dagaa anajichotea hivi,na naamini sio mara yake ya kwanza,ndio maana zahanati hazijengwi,walimu hawalipwi,form six wenye vigezo kibao wako mitaani kwa kukosa mikopo..m..kw...e.re anakenua meno.
 
Wanafunzi wakiandamana na kudai walipwe wanapigwa virungu na kuwekwa rumande bila dhamana.Aliyekwapua kapewa dhamana, watanzania tupigane kwanza ndo turudi kujenga nchi kwa kuheshimiana, inakuwaje mtoto mdogo anakwapua 90million, where is the internal controls over there????
 
Duh kweli za mwizi arobaini. Huyu dada ni mtu wa mishemishe sana mwaka juzi nilikutana nae alikua anajenga nyumba mbezi beach, huu mchezo hajaanza leo.

inawezekana,ameuanza last year,coz amekamatwa kwa kosa alolifanya mwk jana mwez wa 8
 
hivi mkulo atakuwa anapiga mabilioni mangapi kama huyu dagaa anajichotea hivi,na naamini sio mara yake ya kwanza,ndio maana zahanati hazijengwi,walimu hawalipwi,form six wenye vigezo kibao wako mitaani kwa kukosa mikopo..m..kw...e.re anakenua meno.

wakiyafumua ya Mkuro tutajua
 
jiulizeni sasa huyu ni mmoja tu
wangapi wameiga kwenye vyeo vya juu na majina ya wangapi yameingizwa pengine na mwanao ameingizwa na ameshalipiwa vyuoni miaka mitatu we unachakachalika aende chuoni ...hizi ndio laana za watanzania lakini nawaambia ayuko pekee na hata ukiuliza vizuri kilichomsibu huyu binti aunguzwe alichomoa kugawa million 45 kwenye uongozi wa juu hii ni mekudokeza tu fwatilia mwenyewe na pengine atatufungua kwa ni navyojua wale njaa mahakimu wala akuna kesi hapo

ki'uhalisia hawez kula alone
 
Database na system nzima ya bodi ya yetu ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ni mbovu na inatoa mwanya wa kuibiwa na kuwaibia watanzania maskini waliotukopesha. Wiki iliyopita kwenye website yao wametoa majina ya wadaiwa na vitisho kibao, miongoni mwao kuna majina ya watu ambao wameshamaliza kulipa mikopo yao, kuna ambao bado tunaendelea kuwalipa lakini wao taarifa zao zinaonesha hata kuripoti na kupeleka taarifa zetu huko bado. Wizi mtupu.
 
Watu wengi wanahusika hapa, hawezi kuwa peke yake, isitoshe kuanzia mwaka huu pesa zote zinapitia vyuoni sasa imekuwaje?
 
hivi mkulo atakuwa anapiga mabilioni mangapi kama huyu dagaa anajichotea hivi,na naamini sio mara yake ya kwanza,ndio maana zahanati hazijengwi,walimu hawalipwi,form six wenye vigezo kibao wako mitaani kwa kukosa mikopo..m..kw...e.re anakenua meno.

hilo nalo neno
 
Back
Top Bottom