Mfanyakazi wa Bilionea Saniniu Laizer auawa kinyama Mererani..Ndugu waja juu

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Baada ya Mgodi wa mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite ,Mererani, Saniniu Laizer kutoa mawe makubwa ya Tanzanite kiasi cha serikali kumtangaza Bilionea Mpya , mgodi huo umeingia dosari baada ya watu wasiofahamika kumuua mlinzi wa mgodi huo ,Manase William (47)Mkazi wa Ilkiding'a wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha na kisha mwili wake kuegeshwa pembezoni mwa
mgodi.

Familia ya Marehemu imeshtushwa na tukio hilo,na kulitaka jeshi la polisi Mkoani Manyara kufanya uchunguzi wa kina na kutoa majibu sahihi juu ya kifo hicho chenye utata , baada ya kukerwa na taarifa za awali zinadai kuwa ndugu yao aliuawa na majambazi jambo ambalo si kweli.

Akiongea kwa masikitiko mara baada ya mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi Katika hosptali ya Mkoa Mount Meru Leo,kaka mkubwa wa marehemu,Peter William alidai kuwa Manase aliuawa septemba 27 mwaka huu katika mgodi, block D unaomilikiwa na mchimbaji mdogo, Saniniu Laizer kisha mwili Marehemu kuegeshwa kwenye eneo lake la kazi huku taarifa zikieleza kuwa ameuawa na majambazi.

"Tulipata taarifa kuwa ndugu yetu ameuawa na majambazi lakini tulipoenda eneo la tukio tulitilia shaka tukio hilo kwani hakuna mahala ambapo majambazi wamevunja au kupora ,pia marehemu hakuuawa eneo la tukio ila mwili wake ulipelekwa pale ndio maana tumegoma kuzika ili ufanyiwe uchunguzi" alisema

Alisema baada ya mwili wa marehemu kufanyiw uchunguzi (Postmortem) taarifa zikionyesha kwamba marehemu alikutwa na majeraha kadhaa kichwani yaliyoonyesha kupigwa na kitu kizito chenye ncha kali na kuvuja damu nyingi zilizopelekea kifo chake.

"Tunalitaka jeshi la polisi lifanye uchunguzi wa kina ili sheria ichukue mkondo wake kwani ndugu yetu hakuuawa na majambazi Bali ameuliwa kikatili " Alisema Peter

Aidha William alikanusha taarifa zilizotolewa awali na kamanda wa polisi mkoani Manyara kuwa mwili huo ulikuwa umefanyiwa uchunguzi na ndugu kukabidhiwa kwa ajili ya maziko jambo ambalo walidai sio kweli kwani mwili ulifanyiwa uchunguzi Jana baada ya ndugu kususia na kwamba hadi Leo Jumapili walikuwa bado hawajakabidhiwa .

Naye kaka mwingine wa marehemu Efatha Mollel Alisema baada ya kushuhudia mwili wa mdogo wake na taarifa za daktari wameridhika kwamba ndugu yao aliuawa kwa kupigwa na kitu Kizito kichwani ,ambapo amelitaka jeshi la polisi kuchukua hatua Kali kwa wahusika ili iwe fundisho kwa mauaji ya kutatanisha yanayojiyokeza Mererani.

Alisema marehemu mdogo wake alikuwa ameajiriwa kitengo cha ulinzi katika mgodi wa Saniniu Laizer na amefanyakazi kwa muda mfupi wa miezi miwili na kwamba taarifa za awali kwamba aliuawa na majambazi hazina ukweli wowote kwani hakuna mahala palipovunjwa ama kuporwa katika tukio hilo.

"Baada ya mwili wa ndugu yetu kufanyiwa uchunguzi tumeridhika na taarifa ya daktari tunajipanga kufanya mazishi nyumbani kwake Ilikiding'a na baada ya hapo ndugu watakaa na kutoa tamko" alisema Mollel.

Naye Meneja wa mgodi huo,Kiria Laizer alisema kuwa tukio hilo limewasikitisha sana na wameliomba jeshi la.polisi kuchukua hatua ili kubaini ukweli wa tukio hilo na kuahidi kushirikiana na ndugu wa marehemu katika mazishi ya marehemu.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara, Paul Kasabago alisema kuwa jeshi la polisi linawashikilia watu saba wakiwemo wafanyakazi wa mgodi wa Saniniu Laizer wakihusishwa na tukio hilo la mauaji .

Alisema uchunguzi bado unaendelea na pindi upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Picha ya Marehemu Manase pamoja na Nyumba yake aliyokuwa akiishi eneo la Ilikiding'a wilayani Arumeru
IMG-20201004-WA0031.jpg
IMG_20201003_173328_6.jpg
 
Wanasema alijaribu kutorosha Tanzanite mdomoni! Hatuungi mkono mauaji bora angekamatwa na kupewa kesi ya kuhujumu uchumi, ila akuna ajuaye labda marehemu alijaribu kutumia nguvu kujitete na kuzidiwa ubavu na walinzi!
 
Wanasema alijaribu kutorosha Tanzanite mdomoni! Hatuungi mkono mauaji bora angekamatwa na kupewa kesi ya kuhujumu uchumi, ila akuna ajuaye labda marehemu alijaribu kutumia nguvu kujitete na kuzidiwa ubavu na walinzi!
Yeye si alikuwa mlinzi alizidiwa na walinzi wenzake?
 
Kosa linalo sababisha ni serekali yenyewe kumtangaza mtu tena kuonesha wapi mazao kaya pata.pili huyu mwenye mgodi huendeshaji wake unaweza kuwa huna ulinzi wa kutosha,tatu media zimetumia sana kufahamisha kumbe huyu jamaa mgodi wake unatema jana jiwe,leo jiwe.kwa nini manyani wasije.
 
Back
Top Bottom