Mfanyakazi TANESCO amefariki dunia baada ya kunaswa na umeme wakati akiondoa nyaya zilizokuwa zimekatika

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,510
1.jpg

Mfanyakazi wa Shirika la Umeme (TANESCO) Kibaha, Chande Kipae, amefariki dunia baada ya kunaswa na umeme wakati akiondoa nyaya za umeme zilizokuwa zimekatika.

Tukio hilo limetokea April 16 saa tisa jioni wakati Chande akiwa na mtoto wake Jumanne Chande wakielekea mjini kutafuta mahitaji ya familia.

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi umethibitisha kupokea mwili wa marehemu huyo na kwamba waliufanyia uchunguzi na kukabidhi kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Taarifa kutoka Shirika la Umeme TANESCO Mkoani Pwani, Madulu zilithibitisha kutokea kwa kifo cha mfanyakazi huyo huku ikidaiwa kwamba siku ya tukio aliomba ruhusa ofisini kwa ajili ya masuala yake binafsi.

Chanzo: Mpekuzi
 
Usiombeeeusiombeeekabisaaa
Kuonaaaaliekufa na umeme...kijanammoja aliitwakusaidia umeme kuwaka alipopandajuu sijuii alihisii anashikauchii jamaani alikuwaamweusii tiiiiiiinilikimbiaaa

Ushaanza tena kuumwa?
 
Taarifa kutoka Shirika la Umeme TANESCO Mkoani Pwani, Madulu zilithibitisha kutokea kwa kifo cha mfanyakazi huyo huku ikidaiwa kwamba siku ya tukio aliomba ruhusa ofisini kwa ajili ya masuala yake binafsi.

Haya matukio yangekuwa yanaondoka na regional managers huenda tungeokoa maisha ya watanzania wengi, Tanesco wazembe wa kiwango cha juu sana, ukireport juu ya tatizo fulani hawaji kulitatua unless liwe limesababisha kifo hapo ndipo watafanya kambi kwenye eno husika

Nyumbani kwa rafiki yangu Morogoro eneo la Kihonda kuna waya za umeme zimekaa kama bembea, na wakati mwingine wageni hudhani ni waya za kuanikia nguo, rafiki yangu anasema ameriport tatizo hilo Tanesco ni mwaka wa pili sasa unakwisha wanakwenda wanachungulia wanaondoka, imefika sasa hata akienda ofisini wanarushiana mpira kwamba mtu wa stores anakwamisha vifaa na wa stores anasema Engineer ndiye mzembe, Regional Manager anasema nenda kawaone wahusika down stairs
 
Usiombeeeusiombeeekabisaaa
Kuonaaaaliekufa na umeme...kijanammoja aliitwakusaidia umeme kuwaka alipopandajuu sijuii alihisii anashikauchii jamaani alikuwaamweusii tiiiiiiinilikimbiaaa
Mbona mkuu una mwandiko wa hovyoooo sanaaaa.
 
Haya matukio yangekuwa yanaondoka na regional managers huenda tungeokoa maisha ya watanzania wengi, Tanesco wazembe wa kiwango cha juu sana, ukireport juu ya tatizo fulani hawaji kulitatua unless liwe limesababisha kifo hapo ndipo watafanya kambi kwenye eno husika

Nyumbani kwa rafiki yangu Morogoro eneo la Kihonda kuna waya za umeme zimekaa kama bembea, na wakati mwingine wageni hudhani ni waya za kuanikia nguo, rafiki yangu anasema ameriport tatizo hilo Tanesco ni mwaka wa pili sasa unakwisha wanakwenda wanachungulia wanaondoka, imefika sasa hata akienda ofisini wanarushiana mpira kwamba mtu wa stores anakwamisha vifaa na wa stores anasema Engineer ndiye mzembe, Regional Manager anasema nenda kawaone wahusika down stairs
Na wewe umeamua kuwaacha tu
 
Mkuu ukitaka Tanesco waje wewe waambie kuna short ya umeme sehemu flani watakuja fasta sanaa..

Lakini ukiwaambia sijui nyaya ziko chini zimelegea ,sijui nguzo imeinama inataka kuanguka hawajii kwa uharaka wanategeana sanaaaa unless watakuambia kama umeme upo au lah ukisema upo umeme hawaji kabisaaa unless tatizo kubwaa litokee.
Hawa jamaa bangi sanaaa basi tu.
Ukiwa unafanya kazi mashirika ya umma haya akili sijui huwa zinakuaje.
 
Pole kwa wafiwa. Inamaana huyu mfanyakazi wa Tanesco alikuwa anafanya hii kazi ya marekebisho kama kazi ya nje ama?
Sijaelewa kwanini wamesema siku ya tukio aliomba ruhusa kwamba hatahudhuria kazini kwa shughuli binafsi, au marehemu anasingiziwa kuna kitu kunafichwa?
 
Kweli kabisaaa mkuu kuna kitu hapa hakipo sawa.
 
Tanesco wanatabia ya kupuuzia sana malalamiko ya wateja, nadhani uwezo wa viongozi wao wa kusupervise ni mdogo sana!, sijui wanakula maharage ya wapi.
 
Back
Top Bottom