soskeneth
JF-Expert Member
- Jul 2, 2016
- 583
- 235
Sheria ya Ajira na Uhusiano kazininNA6/2004 na sheria ya Taasisi za kazi Na7 ya mwakan2007 zinamtafsiri mfanyakazi kuwa
Ni mtu yeyote aliyeingia katika mkataba wa ajira wa aina yoyote kumfanyia kazi mtu mwingine kwa ujira. Mtu huyo atakaye fanyiwa kazi asiwe mteja wa taaluma yoyote,biashara au kazi inayofanywa na mtu huyo.
Mfanyakazi pia ni mtu yeyote alitajwa kuwa mfanyakazi na waziri chini ya kifungu 98 (3) cha sheria tajwa.
Sheria zinamfafanua zaidi mfanyakazi kuwa ni mtu anayefanya kazi au anatoa huduma kwa mtu mwingine bila kuangalia aina gani ya mkataba iwapo vigezo vifuatavyo vifakuwepo:-
1. Mfanyakazi anakuwa chini ya uangalizi wa mtu mwingine
2. Muda wake unaangaliwa na mtu mwingine
3. Mtu husika ni sehemu ya shirika/Taasisi
4. Kufanya kazi kwa uwiano wa wa masaa 45 kwa mwezi kwa muda wa miezi mitatu
5. Mtu husika anamtegemea kiuchumi anaye mfanyia kazi.
6.mtu huyo anafanya kazi au kutoa huduma kwa mtu mmoja tu.
7. Mtu husika atapewa vifaa vya kazi na mtu anayemfanyia kazi.