Mfanyakazi/Mwajiriwa sasa kupewa TIN Number ili kutambulika kama mlipa kodi kupitia PAYE

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,459
29,153
Wakuu kwema?

Sasa kila Mwajiriwa atatakiwa kuwa na TIN, hii itatumika kumtambulisha kama mlipa kodi pale anapokatwa PAYE kwenye Mshahara wake.

IMG-20200818-WA0050.jpg
IMG-20200818-WA0051.jpg
 
Uzuri wake nini

Mfanyakazi anatambulika kama mlipa kodi kupitia TIN yake baadala ya mfumo wa zamani ambapo muajiri anatambulika kama ndio mlipa kodi.

Hili linaweza mletea nafuu pale anapotaka kufanya biashara nyingine au anapoagiza vitu kama magari anaweza kuclaim excemption kwa ushahidi kwamba yeye ni good tax payer. Mtazamo tu.
 
Taarifa muhimu kwa waajiri na waajiriwa wote nchini Tanzania kutoka TRA.

Tangazo hili ni kwa mujibu wa matakwa ya kifungu cha 22 cha Sheria ya usimamizi wa Kodi (Tax Administration Act, CAP 438 R. E 2019)
IMG_20200818_210605.jpg

IMG_20200818_210607.jpg
 
Hii ni moja ya atuwa kubwa Sana katika kumkomboa mfanyakazi na kuipa thamani KAZI yake. Mimi nataka kuamini SASA tutaelewana tena Sana. Ikumbukwe Kwa waajiri ni msumari wa Moto katika kidonda. Why SASA badala yakumtambuwa kama muwajiri ndie mlipa Kodi SASA serikali inamtambua muajiriwa kama mlipa Kodi na kuweza kuthamini KAZI yake Kwa kumrudishia kile amelilipa zaidi na kumrudishia muhusika pitia Tin number yake.

Ikumbukwe Kwa SASA waajiri wanajuwa au wanajimilikisha return za ziada ya Kodi pasipo warudishia wafanyakazi kwa kuwa tu pesa walilipa wao.

Mfumo mpya utaleta uwazi na uwajibikaji na huenda mfanyakazi kwa mara ya kwanza ataona faida ya kodi yake kwa kurudishiwa ziada yake na pia kupata exemption ya serikali. Ikumbukwe waajiri wanaifaidi hii exemption kwa kulalia mgongoni Kwa wafanyakazi Jambo sio Sawa.

Upande wa pili ni hatari maana sasa huenda mishara ya watu itakuwa ikijulikana na TRA jambo makampuni mengi yasingependa ijulikane. Hasa wale wanalamba mishara minono.

Kuna kila dalili huenda payee mara mfumo huu utaanza kutumika itaongezeka sana au kupungua ila kwa njia za udanganyifu.
 
Back
Top Bottom