Na Yusuf Aboud
ADELINA John Katunzi, hataweza kusahau na kusamehe mzungu David Human, ndani ya mgodi wa dhahabu wa GGM (Geita Gold Mine).
Anashikilia kuwa mzungu huyo alitumbukiza mkono ndani ya chupi yake na kugusa uke wake kwenye lango la kutokea mgodini humo, wilayani Geita.
Adelina alifukuzwa kazi wiki mbili toka afanyiwe operesheni kutokana na ugonjwa wa apendiksi (kidole tumbo). Operesheni ilifanyiwa hospitali ya Mwananchi jijini Mwanza.
Akijua hajajaza fomu za kudai mafao yake kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF), Adelina alikataa kurudisha kitambulisho cha kazi, ili awe anakitumia kuingia mgodini kufuatilia madai yake.
Ilikuwa katika kukurukakara za kutaka arejeshe kitambulisho, mkuu wa ulinzi, David Human aliishiwa subira, kwani angeweza kungoja mlinzi wa kike aje kumpekua Adelina.
Badala yake alitumbukiza mkono sehemu nyeti za mwanamke huyo kwa madai ya kutafuta kitambulisho, "kitendo kilichofanya nilie kwa sauti huku walinzi watatu wa lango kuu wakishuhudia," anasimulia Adelina.
Katika ushahidi wake mahakamani, unaoendana na ule wa mashahidi wengine watatu (walinzi) wa upande wa mashitaka, Adelina anadai alisukumwa na kubanwa kwenye ukuta, akakamatwa mikono, na Human akatumbukiza mkono kwenye chupi yake na kugusa sehemu zake nyeti.
Lakini polisi, katika maelezo yaliyosomwa mahakamani walidai kuwa Human alikamata "makalio, matiti na uke" wa Adelina. Mtetereko huu unasadikiwa kuathiri sana kesi hiyo.
Katika hukumu yake ya tarehe 18 Agosti 2008, hakimu Zabron M. Kesase wa mahakama ya wilaya Geita, anasema "...ni shahidi wa kwanza (Adelina) anayepaswa kulaumiwa kwa kusababisha yote haya."
Hakimu Kesase alisema katika hukumu, "Angekuwa (Adelina) amerejesha kitambulisho kwa wakubwa zake, yote haya yasingetokea. Hivyo namwona mshitakiwa hana hatia na namwachia huru."
Katika kesi hiyo Na. 147 ya 2007 hakimu ananukuu hati ya mashitaka inayosema mshitakiwa alimshika Adelina matiti, makalio na sehemu nyeti.
Hakimu anajenga hoja kwenye tofauti za kauli ya hati ya mashitaka na ushahidi uliotolewa mahakamani, kwamba hakuna hata mmoja, hata Adelina mwenyewe, aliyesema mshitakiwa alishika makalio au matiti ya Adelina.
Haikufahamika iwapo polisi waliandika kwa makusudi, hati ya mashitaka inayotofautiana na madai ya Adelina ili kujenga mashaka yawezayo kumsaidia mshitakiwa.
Adelina alifukuzwa kazi tarehe 5 Machi 2007. Barua ya kumfukuza ilisainiwa na Meneja Mark Jackson wa kampuni ya ATS ambayo inatoa huduma za chakula mgodini. Ingawa Adelina alikuwa analipwa na ATS, vitambulisho vyote vya wafanyakazi mgodini ni vya GGM.
Sababu za kumfukuza zinaelezwa kuwa ni "kampuni kukosa imani" naye. Basi.
"...unafahamishwa kwamba uongozi umeamua kukatisha mkataba wako wa ajira kuanzia leo tarehe 17/02/2007 baada ya kukosa imani na wewe kwenye kazi yako…" anaeleza Jackson.
Barua ilimtaka Adelina kurudisha vifaa vyote vya kampuni alivyokabidhiwa na kuahidiwa kulipwa haki zake anazostahili.
Adelina anakiri alirudisha vifaa vyote vya kampuni isipokua kitambulisho. "Nilikataa kurudisha kitambulisho kwa sababu nilikuwa nawadai mafao yangu kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF).
"Na pale mgodini huwezi kuingia bila kitambulisho; nilijua watanizuia kuingia kwa kuwa nawadai," anaeleza.
Baada ya Adelina kugoma kutoa kitambulisho, meneja Mark Jackson, anadaiwa kuwaamrisha walinzi watatu waliokuwa kwenye lango kuu wachukue kitambulisho kwa nguvu.
Walinzi hao, Richard Maganga, Niclaus Misenya na Amos Makongoro walikataa kutii amri ya Jackson kwa madai kuwa angekaguliwa na kushughulikiwa na mlinzi wa kike na siyo wao wanaume.
Kilichofuata ni Jackson kupiga simu kwa mkuu wa walinzi, David Human na Adelina akazuiwa kutoka nje ya lango.
Adelina anasimulia, "Alipokuja David akaniuliza, ‘wewe ndiye Adelina John?' Nikamjibu ndiye mimi. Akaniambia kwa ukali, ‘lete kitambulisho.' Nikamwambia siwapi mpaka mnilipe haki zangu zote."
Adelina anasema, wakati huo alikuwa ameweka kitambulisho kwenye matiti; ndipo alikihamisha na kukitumbukiza kwenye chupi kwa mbele.
"Alipoona nimeweka kitambulisho kwenye chupi akanikamata na kutumbukiza mkono; alishindwa kukitoa kitambulisho badala yake akanishika ukeni," anasimulia Adelina huku chozi likitiririka kutoka jicho lake la kulia.
Purukushani hizi ziliishia pale Adelina alipokubali kuingia kwenye gari la mgodi na kwenda moja kwa moja hadi ofisi ya mwanasheria wa GGM akiongozana na Human na meneja wa ATS.
Adelina anasema mwanasheria alimsihi akabidhi kitambulisho, pendekezo ambalo alikubali, lakini akamfafanulia kuwa anaweza kumshitaki aliyemwingiza mkono katika sehemu za nyeti.
Kwa mwaka wa nne sasa, mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 31, mtariki na mwenye watoto wawili, hajalipwa mafao yake.
Richard Maganga, mmoja wa mashahidi upande wa mashitaka na ambaye ushahidi wake ulifanana kabisa na ule wa Adelina, naye tayari amefukuzwa kazi tangu mwaka 2008. Alikuwa amefanya kazi ya ulinzi mgodini kwa miaka minane.
Ingawa alikuwa mlinzi, barua yake ya kufukuzwa ilimhusisha Maganga na wizi wa mafuta ya mashine/mtambo wa kunyanyulia mizigo.
"David alitulazimisha mimi na wenzangu wawili tumnyang'anye Adelina kitambulisho chake, lakini tulikataa," anaeleza Maganga nakukana tuhuma za wizi akihoji, "Kama ni wizi si wangenipeleka mahakamani?"
"Sasa Adelina alipopeleka kesi mahakamani nilitoa ushahidi kama nilivyoshuhudia. Ushahidi wangu ulizingatia kilichotendeka kama Adelina alivyoeleza. Bila shaka hilo ndilo lilinifukuzisha kazi," anasema Maganga.
Kama ilivyo kwa Adelina na Maganga, ndivyo ilivyo kwa Emmanuel Lesilwa. Alianza kazi 2004. Aliachishwa kazi 16/05/2008.
Anadai alifanyiwa operesheni ya apendiksi mwaka 2007, katika hospitali ya Mwananchi iliyoko mjini Mwanza, ambayo ndiyo inatibu wafanyakazi wa mgodi wa GGM.
Aliporudi kazini meneja wake, Felix Adolf alimwabia utendaji wake umeshuka na akamwachisha kazi hata kabla kidonda cha operesheni kupona.
Usalama kazini ni mdogo. Sababu za kufukuzwa au kuachishwa kazi ni dhaifu. Uelewa wa wafanyakazi jinsi ya kujitetea, kulinda na kupigania haki zao ni haba.
Source: MwanaHalisi