Mfanyakazi CRDB afikishwa Mahakamani kwa kumuibia mteja zaidi ya Tsh milioni 100 na kuzitakatisha

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Messages
488
Points
1,000

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2018
488 1,000
WhatsApp-Image-2019-09-27-at-11.29.47.jpeg
Mfanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Ubungo, Andrew Babu (27) na wafanyabiashara watatu, wameshtakiwa kwa kula njama, kughushi Tembo kadi ya mteja, wizi wa zaidi ya Sh milioni 100 na kutakatisha fedha hizo.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, William Sige (52), Justina Boniphace (49) na Alli Tutupa (35) wote wanaishi jijini Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Mbando alidai kati ya Oktoba 2018 na Aprili 19, 2019 washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama kutenda kosa la wizi.

Katika shtaka jingine imedaiwa, Oktoba 29, mwaka jana katika benki ya CRDB tawi la Ubungo, ndani ya manispaa ya Ubungo, mshtakiwa Babu peke yake kwa nia ya kulaghai au kudanganya, alighushi sahihi ya Charles Kihamia katika fomu ya maombi ya Tembo card.

Pia mshtakiwa Babu anadaiwa, Novemba 6, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Babu anadaiwa Novemba 5, 2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika usajili wa kadi ya visa ya Tembo, kwa madhumuni ya kuonesha kuwa sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Inadaiwa Novemba 6,2018 alighushi sahihi ya Kihamia katika kitabu cha usajili wa uelekezaji kwenye fomu ya maombi kwa madhumuni ya kuonesha kuwa, sahihi hiyo imewekwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Mshtakiwa Babu pia anadaiwa, Oktoba 29, 2018 huko katika benki ya CRDB, alitoa fomu ya kughushi ya maombi ya Tembo kadi kwa ofisa wa banki hiyo aitwaye Omary Mduyah kwa dhumuni la kuonesha kuwa fomu hiyo imetolewa na kusainiwa na Kihamia huku akijua kuwa siyo kweli.

Katika shtaka la mwisho, imedaiwa kati ya Novemba 7,2018 na Aprili 29,2019 washtakiwa hao kupitia kadi ya gold ya Visa, walijipatia sh. 106,267,907/- kutoka kwa Charles Kihamia kupitia Visa gold card huku wakijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kughushi na wizi.

Hata hivyo wa washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 10, mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
 

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Messages
6,071
Points
2,000

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2016
6,071 2,000
If possible anyongwe mpaka kufa pale viwanja vya karume ..Waliwahi nichomolea hela zangu hawa mbuzi ...Nasema Tena bila aibu naomba anyongwe bila huruma mpaka pale Israel mtoa roho akichomoa roho yake bila huruma
mbaya zaidi ndio wanawagongea madem zenu, unawaakuta mlimani City pale Samaki Samaki wakiwinda, na wanakula kweli vitoto vizuri
 

abdi ally

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2018
Messages
1,335
Points
2,000

abdi ally

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2018
1,335 2,000
Mafala wanasema milion 100 kwa mtu tatu ndogo huku thamani yake kwa ujumla yeye na anavomiliki ni 2milion na anaishi kwa wazazi
Milion 100 kwa watu 3 Ni kubwa ila itakuwa ndogo Kama itatolewa kwa mafungu mafungu na hyo inetolewa kwa installment sio yote ndio maana watu wanasema Ni ndogo mkuu

Na pia unaweza ukapewa milion 50 Sasa kama. Huna plan nzuri n ndogo pia kwahyo pesa kuwa kubwa au ndogo Ni wewe mwenyewe unaiweka vp na unaichukuliaje lakin kwa hyo hela kwa bata Ni ndogo Sana Kuna hotel zipo tz Ni 15- 50M per day Sasa kwann isiwe ndogo
 

naiman64

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2013
Messages
4,790
Points
2,000

naiman64

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2013
4,790 2,000
Mkuu nilikaa miezi sita sijaenda bank kuchukua.mshahara wangu, jamaa akajibinafsisha bila wasiwasi nadhani alifikiri nimekufa, siku naibuka kila nikiuliza sipati ushirikiano kumbe bahati mbaya yeye ndiye ninayemuuliza tatizo langu, mwisho akasema ofisi walikuwa hawanipelekei mshahara, nikamjibu nipo Accounts tena salaries na mleta cheque anachukua kwangu baadae nikarudi na docs zote hadi Kwa meneja wake akaitwa akaonywa nikapewa pesa yangu, mwezi iliofuata kabeba tena nikamshtaki baadae sikumuona tena.maeneo yale na mshahara wangu nikawa naupata bila tatizo. Haya.matatizo mengi yanachangiwa na wafanyakazi ambao sio waaminifu, sasa Mimi haikuiwa CRDB ni nyingine kabisa
wanachofanya hao wafanyabiashara na wafanyakazi wa benki wanabeba pesa za wateja wenye pesa ndefu halafu hawana tabia ya kuwithdrawal mara kwa mara, wakishachukua pesa wanazizungusha kwenye biashara halafu baadae wanazirudisha
 

Forum statistics

Threads 1,343,415
Members 515,055
Posts 32,784,063
Top